Achana na Jack Ma' ama Mukeshi Ambani ambao kwa miaka ya hivi kwa nyakati tofauti walitambulika kama watu tajiri zaidi barani Asia, kwasasa wote hawapo kwenye kiti hicho.
Kiti hiko kwasasa kina Mfalme Mpya aitwae Guatam Adani ambaye kwa hesabu za Forbes kufikia 03 Februari 2022 alikuwa na utajiri wa kiasi cha $ 90.1bln akiwa ndiyo tajiri namba moja barani Asia kwasasa.
Billionea huyo ambaye ni mwanzilishi na mwanahisa mkubwa wa kampuni ya Adani Group aliyoianzisha mwaka 1988, kwasasa kampuni hiyo ina kampuni tanzu sita zilizojiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Bombay (BSE) na kampuni hizo kwa mwaka 2021 zilifanya vema na kumfanya Adani utajiri wake kuongezeka.
Kampuni yake ya Adani Green Energy kwa mwaka 2021 ilifanya vema zaidi kwani hisa zake zilipanda kwa 77%, kufikia mwaka 2008 utajiri wa Adani ulikuwa $ 9.3bln lakini kufikia Aprili 2021 ulipanda na kufikia $ 50.5 bln Forbes walipotoa orodha mabillionea duniani.
Ikumbukwe tu Guatam Adani aliachana na masomo ya Chuo Kikuu na kujikita zaidi kwenye biashara mwishoni mwa miaka ya 1980, kampuni yake inafanya biashara mbalimbali hasa za ujenzi, uzalishaji nishati pia inamiliki hisa 74% za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mumbai ambapo hisa hizo ilizipata Septemba 2020.