Msimu Wa 2024/2025 Timu za Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
564
727
125
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almas Kasongo amesema kuanzia msimu ujao wa Ligi 2024/25 ni ruksa kwa timu ya Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar katika mechi zake na ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina inayoendeshwa na bodi hiyo.
Kasongo amesema katika kanuni iliyofanyiwa maboresho kuelekea msimu mpya ni hiyo ya matumizi ya viwanja Zanzibar kwenye Ligi Kuu.