Muenendo wa Hisa za Bank ya CRDB

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam
Mnamo 15 Dis 2021 Benki ya CRDB PLC ilisaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) na washirika weke kibiashara NorFund kutoka Norway na IFU kutoka Denmark kufungua kampuni tanzu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika hafla iliyofanyika katika Hoteli Fleuve De Congo, Jijini Kinshasa.

Kuanzishwa kwa kampuni tanzu ya Benki ya CRDB DRC ni mwendelezo wa mkakati wa Benki hiyo kubwa nchini katika kujitanua nchi za Afrira Mashariki na zilizo Kusini mwa Afrika. CRDB Congo inatarajiwa kuanza kutoa huduma zake nchini humo ifikapo mwezi Mei 2022.

Tayari CRDB Bank PLC ipo Burundi, na inaendelea kutanua wigo wa huduma zake katika Ukanda huu, DRC kwasasa ina wakazi wanaokadiriwa kufikia 80mln mwaka 2020.

CRDB Bank ilijirodhesha kunako Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE) mwaka 2009 ni imekuwa ni kampuni inayofanya vizuri sokoni na kuvutia wawekezaji, vilevile ni kampuni ambayo faida yake imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Kwasasa hisa moja ya CRDB inauzwa TZS 260, mnamo 31 Disemba 2019 hisa moja ya Benki hiyo ilikuwa inauzwa TZS 95 lakini kutokana na kufanya vizuri imekuwa ikipanda siku hadi siku. Kufikia 30 Septemba 2021, CRDB ilikuwa imepata faida ya TZS 167 bln huku robo ya mwisho ya mwaka ikitegemewa kufanya vizuri.
 
  • Like
Reactions: JimNicklaus