Nchi wanazotoka wachezaji, hulka na tabia zao ( zingatia haya kipindi cha usajili)

Hammy36

Administrator
Jan 17, 2023
56
54
5
Dar Es Salaam
1. GHANA
Kuna wachezaji wana vipaji vikubwa lakini ni wapenda starehe na wavivu mno. Ukimsajili Mghana tegemea utendaji kazi wa hovyo, kusumbuka makocha na Kambi ya team. Ni wazuri kwenye kuingia mikataba ili wakusumbue uvunje mkataba wapige hela waende zao.

Mfano: Morison, Okrah, Asamoh, Afiz Konkon.

2 CONGO
Hawa wana vipaji na wanakujaga na njaa ila wakipata hela na umaarufu wanamsumbua mno na Team zinashindwana nao. Ukisajili Mkongoman kama ana kipaji akianza umaarufu muuze fasta hawafugiki hawa.

Mfano: Inonga, Mayele, Djuma Shaban, Bangala.


3.Nigeria
Hawa ni matapeli wanaokuja huku ni wale wa Chandimu tu. Wachezaji wenye vipaji kutoka Nigeria Hawezai kuja kucheza Tanzania.

4. SENEGAL
Hawa ni waungwana mno. Wao wanaamini wanapaswa kucheza Europe, wanaokosa nafasi huja huku kujionesha na wakipata nafasi hutumikia vyema. Ukipata Msenegal msajili fasta.

5. IVORY COAST, MALI, CAMEROON, BURKNABE
Hawa ni waungwana, wana vipaji na bidii kwenye kazi yao. Wao tumaini lao ni kucheza France wakikosa fursa hiyo huja huku kupambana hasa na wana malezi Bora mpira, Wanachohitaji ni love ya mashabiki wako hata tayari kucheza Bure.

Mfano: Kipre Junior, Azizi ki, Yao, Kanoute, Onana, Fredi, Pacome n.k

6 Zambia, Kenya, Uganda, Rwanda
Hawa waswahili kama local players tu. Wana vipaji vya kawaida mno japo hutokea wachache na wengi ndoto zao ni kucheza Tanzania.

ONGEZEA NCHI NYINGINE HAPA KWENYE COMMENTS