Premier League: Uzi maalumu wa matokeo, msimamo wa ligi, wafungaji n.k

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
Msimamo wa Ligi: Matokeo haya ni mubashara, yanabadilika jinsi mechi zinavyoendelea.



Mechi Zinazofuata: Matokeo haya ni mubashara, yanabadilika jinsi mechi zinavyoendelea.


Wafungaji bora wa Ligi: Matokeo haya ni mubashara, yanabadilika jinsi mechi zinavyoendelea.

 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Nafasi nne za juu katika msimamo wa EPL hadi sasa
Vipi chama lako lipo au mnasubiri viporo
 

Attachments

  • epl.PNG
    epl.PNG
    437.5 KB · Somwa: 1

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
FULL TIME
Liverpool 3-1 Newcastle
⚽
7': Shelvey
⚽
21': Jota
⚽
25': Mo Salah
⚽
87': Trent Alexander-Arnold
 

Attachments

  • liverpool.PNG
    liverpool.PNG
    527.5 KB · Somwa: 1

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Full Time
Wolves 0-0 Chelsea
Hakuna mbabe, Chelsea wanaambulia alama moja tu
 

Attachments

  • chelsea.PNG
    chelsea.PNG
    539 KB · Somwa: 0

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Ushindi mzito wa Man City unazidi kuwafanya wajikite zaidi kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya EPL
Wanafikisha alama 44 katika mechi zao 18
 

Attachments

  • man c.PNG
    man c.PNG
    632.7 KB · Somwa: 0

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
FULL TIME:
Tottenham Hotspurs 2-2 Liverpool
⚽13': Harry Kane
⚽35': Diogo Jota
⚽69': Andrew Robertson
⚽74': Son
Liverpool pungufu yatoa sare na spurs London.
 

Attachments

  • liver.PNG
    liver.PNG
    415.3 KB · Somwa: 0

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA LIVERPOOL, 2-2 DARAJANI.​

1641189965627.png
WENYEJI, Chelsea wametoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Liverpool ilitangulia kwa mabao ya washambuliaji wake tegemeo wa Kiafrika, Msenegal Sadio Mané dakika ya tisa na Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 26, kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa Mateo Kovacic dakika ya 42 na Christian Pulisic dakika ya 45.
Chelsea inafikisha pointi 43, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 21, wakati Liverpool inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 20 nafasi ya tatu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAICHAP TOTTENHAM 2-0 DARAJANI.​

1641456665875.png

WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea katika mchezo huo dhidi ya timu ya kocha wao wa zamani, Antonio Conte yalifungwa na Kai Havertz dakika ya tano na Ben Davies aliyejifunga dakika ya 34.
Timu hizo zitarudiana Januari 12 Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Arsenal na Liverpool katika fainali ya Carabao 2022.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
📝
DEAL DONE: Newcastle United imemtangaza Kieran Trippier kuwa mchezaji wao akitokea Atlético Madrid kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Trippier amejiunga na Newcastle kwa dau la £12m
Mabosi wa Newcastle wameanza kazi
😀

1641551592202.png
1641551625408.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAIKALISHA CHELSEA 1-0 ETIHAD​

1642397126842.png
BAO pekee la Kevin De Bruyne dakika ya 20 limetosha kuipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad.
Kwa ushindi huo, Man City wanafikisha pointi 56 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 13 zaidi ya Chelsea wanaofuatia baada ya timu zote kucheza mechi 22.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YATOA SARE NA BRIGHTON 1-1 THE AMEX​

AVvXsEgvPwp3VVzFtqntVoBfHn_UGqJRQAhBgbJEuqrcEa4sQJQbRMSfYsv5Sojvk8I90t7P0peBdg6YJyMwIw5W7V8eJVV5HUDHJA02_qr6BDZr1JtusltId_CO6XVh5oN5ZyHgvvoif0n77eixRocNryGGVlHnjMyg-3tArl13LmsCdGoWBsv1pTdgXhpg=w640-h406


TIMU ya Chelsea imetoa sare ya 1-1 na wenyeji, Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa The AMEX, Falmer, East Sussex.
Hakim Ziyech alianza kuwafungia wageni dakika ya 28, kabla ya Adam Webster kuwasawazishia wenyeji dakika ya 60 na sare hiyo ya nane ya msimu inazidi kuiondolea Chelsea matumaini ya ubingwa sasa kikosi cha kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kikiachwa pointi 12 na mabingwa watetezi, Manchester City.
Chelsea inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 23 nafasi ya tatu, nyuma ya Liverpool pointi 45 za mechi 21 na Man City pointi 56 za mechi 22, wakati Brighton imefikisha pointi 29 katika mechi ya 21 nafasi ya tisa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Rooney Atajwa Kuinoa Everton​

0_GettyImages-1236714424.jpg

MKONGWE wa Manchester United, Wayne Rooney anatajwa kuwa huenda akarithi mikoba ya Rafael Benitez
ndani ya Goodison Park.
Everton siku ya Jumapili ilimfuta kazi aliyekuwa kocha wake Rafael Benetiz baada ya timu hiyo kuendelea kufanya vibaya ndani ya Premier League.
Ushindi wa Norwich City wa mabao 2-1 dhidi ya Everton ndiyo ulipelekea kibarua cha kocha huyo kuota nyasi,
baada ya kocha huyo kudumu hapo kwa miezi sita tu.
Inaelezwa kuwa kocha huyo hakupewa fedha za kutosha kwaajili ya kufanya usajili kwani katika mechi 12 zao za
mwisho alipoteza tisa. Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuondolewa Benitez, Rooney ndiye ambaye kwa sasa anainoa Derby County ya Championship ndiye anatajwa kuwa na nafasi
kubwa ya kutua kwenye kikosi hicho.
Rooney ambaye aliwahi kuichezea Everton anapewa nafasi ya kwenda kukinoa kikosi hicho zaidi japo kuna makocha wengine pia wanatajwa. Makocha kama Duncan Ferguson (msaidiz sasa) ambaye aliwahi kuishikilia kwa muda huko naye anatajwa kupewa timu
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
FULL TIME
Leicester 2-3 Tottenham
⚽
24': Patson Daka
⚽
38': Harry Kane
⚽
76': Maddison
⚽
90+5': Steven Bergwijn
⚽
90+7': Steven Bergwijn
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA
Kocha mpya wa Watford Roy Hodgson ameanza kibarua chake cha kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Claudio Ranieri ambaye amefutwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na nyasi
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
MATOKEO
Man City 2-0 Brentford
Norwich 1-1 Crystal Palace
Tottenham 2-3 Southampton
Aston Villa 3-3 Leeds Utd
Mikeka vipi?
😅






 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Ujanja wa Southampton washtukiwa.​

UwanjaPIC

LONDON, ENGLAND. UNAAMBIWA kushinda mechi kunahitaji mbinu za kijanja. Na hilo linadaiwa kufanywa na Southampton kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Na hakika kikosi hicho cha St Mary’s mambo yao yamekuwa yakienda vizuri uwanjani tangu walipokuja na mbinu hiyo mpya.
Mfano mzuri ni kiwango chao cha wiki iliyopita, ambapo walipindua matokeo ya kichapo cha mabao 2-1 na kushinda 3-2 dhidi ya Tottenham.
Ni hivi, wachezaji wa Southampton wameanzisha desturi ya kujiangusha na kuhitaji matibabu ndani ya uwanja kati ya dakika 60 na 70 kwenye mechi zao msimu huu.
Na The Athletic limefanya utafiti na kugundua huo huo ni mpango unaofanywa makusudi na timu hiyo. Utafiti huo umeonyesha kwamba wachezaji wa Southampton waliojiangusha na kuhitaji kutibiwa kati ya dakika 60 na 70 ni 14 katika mechi zao 24 walizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Kila wakati wanapofanya hivyo, wachezaji wamekuwa wakikimbilia nje ya uwanja kupewa vinywaji vya kuongeza nguvu na kupata mapumziko kidogo. Bado haijathibitika kama mastaa wa Southampton wanajiumiza makusudi kusimamisha mchezo.
Vinywaji wanavyopewa vinaripotiwa kuwaongezea nguvu wachezaji, ambao wanaonekana kumaliza mechi dakika za mwisho kwa nguvu sana.
Kuthibitisha hilo, mchezaji Adam Armstrong amedaiwa kuumia mara nne tofauti ndani ya muda huo katika mechi tofauti kukamilisha mpango.
Kwenye mechi ya Spurs, Che Adams aliumia dakika 63, kabla ya Armando Broja naye kuumia na kutaka matibabu yanayochukua dakika kadhaa kwenye dakika 70 baada ya Son Heung-min kufunga bao na kuifanya Spurs kuongoza 2-1. Jambo hilo lilidaiwa kufanya mambo kuwa mazuri, ambapo mabao mawili ya dakika za mwisho kutoka kwa Mohamed Elyounoussi na Che Adams yaliisaidia Saints kupindua matokeo ya kushinda 3-2.
Daktari wa zamani wa Wolves, Phil Hayward aliiambia The Athletic: “Nina hakika wanasayari ya michezo watakuwa wametoa pendekezo la kufanya hivyo na kocha (Ralph) Hasenhuttl amelipitisha.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kane, Pochettino kuna kitu spesho.​

Kane PIC

LONDON, ENGLAND. STRAIKA, Harry Kane ameripotiwa kufungua milango ya kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino wakati huu bosi huyo wa Paris Saint-Germain akihusishwa na kibarua cha kwenda kuinoa Manchester United.
Kane, 28, aliwahi kufanya kazi na Pochettino huko Tottenham Hotspur kwa kipindi cha miaka mitano na wawili hao walitengeneza muunganiko mzuri wa kocha na mchezaji. Kwa pamoja waliifikisha Spurs fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na kwa misimu mfululizo imekuwa ikimaliza ndani ya Top Four kwenye Ligi Kuu England, kitu ambacho kwa Man United kimekuwa kigumu kwa siku za hivi karibuni tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu huko Old Trafford.
Pochettino bado ana mkataba PSG hadi Juni 2023, lakini kwa sasa anapewa nafasi kubwa ya kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa Man United mwisho wa msimu huu ambapo kwa sasa ipo chini ya kocha wa mpito, Ralf Rangnick.
Na iliripotiwa kwamba Pochettino atahitaji kuwa na huduma ya Kane huko Old Trafford kama atapewa mikoba ya kuwa kocha.
Gazeti la The Telegraph linaripoti kwamba Kane ni mfungaji mahiri wa ambaye ambaye Man United inamhitaji kuwa naye kwenye kikosi chao tangu ilipoachana na Robin van Persie, aliyetupia nyavuni mabao 26 katika msimu wake wa mwisho na Ferguson.
Na mtu wa karibu wa Kane alisema kwamba nahodha huyo wa England anasubiri kwa hamu kubwa nafasi ya kufanya kazi tena chini ya Pochettino. Kane alikaribia kujiunga na Manchester City kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi baada ya kufikia makubaliano binafsi, lakini mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy dau lake la kutaka alipwe Pauni 160 milioni lilikuwa kikwazo.