PSG

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

He! Eti Messi chanzo Mbappe kuondoka​

MEssi PIC

PARIS, UFARANSA. USAJILI wa supastaa Lionel Messi huko Paris Saint-Germain umeripotiwa kuchochea uamuzi wa Kylian Mbappe kutaka kuachana na miamba hiyo ya Ligue 1, ripoti kutoka Ufaransa zimeeleza.
Bao la dakika za majeruhi la Mbappe lilifanya PSG kupata ushindi muhimu dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne iliyopita, ambapo Messi alikosa penalti baada ya kipa Thibaut Courtois kuokoa.
Straika, Mbappe mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu huko Parc des Princes na kumekuwa na ripoti kwamba ataelekea zake Bernabeu. Hata hivyo, ripoti nyingine inadai kwamba PSG imepanga kumfanya Mbappe kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ili alingane na masupastaa wengine kwenye kikosi hicho ni Messi na Neymar.
Na sasa akiwa amebakiza miezi minne ya mkataba wake huko Parc des Princes kumekuwa na maelezo kwamba mchezaji huyo anaweza kuondoka bure kwenda Los Blancos kama hakutakuwa na jitihada kubwa za PSG katika kumbakiza.
Kinachoelezwa ni kwamba uamuzi wa klabu kumchukua Messi kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi limetibua hali ya mambo kwenye vyumba vya kubadilishia vya klabu hiyo, ambapo amevunja ule uhusiano matata kwenye fowadi sambamba kati ya Mbappe na Neymar. Messi kwa sasa amekuwa na sauti kubwa huko kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kutokana na hadhi yake kwa wachezaji wengine.
Mbappe amefunga mabao 22 na kuasisti mara 16 msimu huu, akitengenezea nafasi ya kuwa staa muhimu kabisa kwenye kikosi hicho cha kocha Mauricio Pochettino na hakika bila ya mabao yake, timu hiyo ingekuwa inapata shida kushinda mechi zake.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Mbappe: Messi? Ballon d’Or sio ishu kwake​

Ballon PIC

PARIS UFARANSA. SUPASTAA, Kylian Mbappe amesema tuzo za Ballon d;Or za Lionel Messi ni namba tu, hazihusiani chochote na kiwango cha soka lake huko kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain. Messi aliachana na Barcelona kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana na kutua Parc des Princes kwa uhamisho wa bure kabisa.
Messi, anahesabika kama mmoja wa wanasoka bora wa muda wote duniani, akivunja rekodi kibao huko Hispania, lakini amekuwa na wakati mgumu tangu alipotua Ufaransa.
Aliasisti mara mbili kwenye ushindi wa mabao 3-1 iliyopata PSG dhidi ya Saint-Etienne Jumamosi iliyopita, lakini amefunga mara saba tu katika mechi 23 alizocheza msimu huu.
Messi amefunga mabao machache sana ukilinganisha na makali yake ndani ya muongo huu, lakini Mbappe alisema mafanikio yake ya huko nyuma hayana maana yoyote. Mbappe, ambaye alifunga mabao mawili, anaamini Messi atakuja kutamba tu. Mbappe alisema: “Ni mchezaji mahiri. Nafurahi kwa sababu zote tunafahamu anajaribu kuzoea maisha mapya, jiji jipya na klabu mpya. Hata kama umeshinda tuzo saba za Ballons d’Or, bado kuna maisha lazima uyazoee kwanza.”
Mabao mawili ya Mbappe aliyofunga Jumamosi yamemfanya afikie rekodi ya Zlatan Ibrahimovic ya mabao 156. Hata hivyo, bado ana safari ndefu ya kumfikia kinara wa mabao wa PSG, Edinson Cavani, ambaye amefunga mabao 200, huku Mfaransa huyo akihusishwa na mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Mkurugenzi wa PSG Leonardo kuhusu Sergio Ramos:
"Tulipomsajili, Ramos alikuwa sawa kimwili. Kwa bahati mbaya, tulichotarajia kukipata kutoka kwake hakijafanikiwa, Lakini tusubiri msimu bado haujaisha"
"Siku tutakavyosema hawezi kucheza tena, itakuwa wazi kwa kila mtu, Ila Sio kwasasa"
KUHUSU KYLIAN MBAPPE
"Kwakuwa hakuna timu iliyomsajili hadi sasa, tutajitahidi kwa namna yoyote kuhakikisha anabaki, tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hilo linatimia"
CHANZO: L'Equipé
Inaweza kuwa picha ya Watu 2 na watu wanasimama
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Baada ya PSG
🇫🇷
kithibitisha kuwa mlinzi wake wa kati Sergio Ramos kuwa ataukosa mchezo wa Uefa Champions League Jumatano hii dhidi ya Real Madrid
🇪🇸
, Kylian Mbappe nae yupo shakani kuucheza mchezo huo kutokana na majeraha aliyoyapata mazoezini
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi yanayosema 'ACCOR A!! LIVE LIMITLESS'
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Kwa mujibu wa Daniel Riolo wa RMC Sport, Neymar ni tatizo ndani ya PSG
Daniel amesema kuwa Neymar amefikia hatua ambayo huenda asifanye mazoezi tena, ana roho ya kulipiza kisasi dhidi ya timu hiyo
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi yanayosema 'QN 人 All ACCOR LIVE LIMITLESS 10'