Sababu Zinazonifanya Niamini Simba Hatachukua Ubingwa NBCPL 2024/2025

Bakari

Mgeni
May 27, 2024
27
31
5
(1) HAKUNA MABADILIKO YA UONGOZI, nilipoona Try again amejiudhuru na Mo dewji kuja kumtambulisha tena kuwa mjumbe hii ilinifanya nione kabisa hakuna serious yoyote bali wajomba wanapumnzishana tu ili kulinda masilahi yao binafs katika timu, kwani ikumbukwe Mo dewji alimuachia kiti try again na sasa amaerudi tena, kwa mwenendo huo wanasimba wasitegemee makombe kama uongozi uliopita na uliopo umeshindwa kabisa kuwapa hata kombe la kufutia machozi, uongozi bora unachangia pakubwa sana katika maendeleo ya timu.

(2)SAKATA LA USAJILI WA LAWI NA CHAMA, boss aliporudi Simba aliwaambia wanasimba kuwa" amerudi na nguvu mpya na kasi" pia kwa hiyo wanasimba wanapaswa kuandaa furaha tu lakini usajili wa mchezaji lawi kutoka coastal union umekuja kutia doa na kuonekana Simba sc ni janja janja tu haina hele na bosi kaja na maneno badala ya kutoa kibunda na ndiyo hivyo kwa Chama , walisema kuwa wanaachana na chama wakati hawajapata mbadala baada ya kusikia chama anakwenda upande wa pili wameenda kumpigia magoti na kumuongezea dau , hii tafsiri yake ni kuwa "there is a lack of seriousness"

(3)BOSS KUFANYA PRESS KWENYE MITANDAO KAMA INSTAGRA, Simba sc ni timu kubwa yaani ni brand kubwa na ina mashabiki wa kutosha na hao mashabiki wanataka kumuona boss wao au tajiri wao wa timu akiongea nini kuhusu timu yao, wanataka kuona vyombo vya habari vikifanya mahojiano na boss wao na siyo boss kukaa geto kisha kuanza kutoa maneno yake tena ya kuchagua viongozi watakao unda bodi ya timu , kwa muonekano huu inaonesha kabisa Simba sc inachezewa na baadhi ya watu wachache wanaojiona simba ni ya kwao, kwa madharau kama haya kwa masahabiki tusitegemee kuona Simba sc ikichukua ubingwa wa Nbcpl 2024/2025.

(4)MGAWANYIKO WA VIONGOZI NDANI YA CLUB, za ndani kabisa kuna baadhi ya viongozi hawajapendezwa na mrejeo wa Mo dewji na kupanga swahiba wake Try again kuwa mjumbe, sasa kwa bomu kama hili tusitegemee kuona matunda ya timu aua timu kupata vikombe maana hakuna maelewano kwa viongozi hakuna vita mbaya kama ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nyumba moja ni rahisi sana kuvunja nyumba

(5)USAJILI WA WACHEZAJI PASIPO NA PENDEKEZO LA KOCHA, Timu haina kocha mpaka sasa lakini inafanya usajili swali je ni nani anayesajili na kutoa mapendekezo kuwa mchezaji fulani asajiliwe?
hakuna cha skauti wala mgunda ni viongozi ndiyo wanasajili kwa kutumia uzoefu waliokuwa wanaufanya toka mwanzo lakini kwa sasa ukiwauliza watakuambia tunatumia skauti na kocha mgunda ukija nyuma ya pazia kuna ujanja mwingi sana unafanyika.
tukumbuke timu ilishawahi kwenda pre season bila ya kocha na baadhi ya wachezaji walikuja nyuma nyuma tena kwa kulazimishwa hata msimu wa 2024/25 hiki kitatokea na kwa muundo huu tusiegemee kuona Simba sc ikichukua kombe lolote ndani ya ligi.
 
Engineer ELL

Mpiga Chabo
Jun 24, 2024
1
0
0
Mashabiki na wanachama ni wakati wenu kupaza sauti sasa ikumbukwe Simba sport club sio timu ya mtu binafsi kwamba viongozi waliopo madarakan hatuwezi kuwatoa ni timu ya wananchi kama yoyote mwenye vigezo anaweza kuwepo pale na kuendesha club kama waliopo hawana vigezo hivyo wakae pembeni kupisha wengine club ni kubwa kuliko wao watafute club nyingine au business nyingine...... 💪🥰🥰
 
Sir tenge

Mgeni
Jun 5, 2024
11
4
5
Mashabiki na wanachama ni wakati wenu kupaza sauti sasa ikumbukwe Simba sport club sio timu ya mtu binafsi kwamba viongozi waliopo madarakan hatuwezi kuwatoa ni timu ya wananchi kama yoyote mwenye vigezo anaweza kuwepo pale na kuendesha club kama waliopo hawana vigezo hivyo wakae pembeni kupisha wengine club ni kubwa

Mashabiki na wanachama ni wakati wenu kupaza sauti sasa ikumbukwe Simba sport club sio timu ya mtu binafsi kwamba viongozi waliopo madarakan hatuwezi kuwatoa ni timu ya wananchi kama yoyote mwenye vigezo anaweza kuwepo pale na kuendesha club kama waliopo hawana vigezo hivyo wakae pembeni kupisha wengine club ni kubwa kuliko wao watafute club nyingine au business nyingine...... 💪🥰🥰
Hakuna wa kukaa pale kaka coz tayari wameshaanda ulinzi kwa ajiri yao ndio maana unaona anatoka kujikosha kwa wanachama halafu baadae anarudi tena
Mashabiki na wanachama ni wakati wenu kupaza sauti sasa ikumbukwe Simba sport club sio timu ya mtu binafsi kwamba viongozi waliopo madarakan hatuwezi kuwatoa ni timu ya wananchi kama yoyote mwenye vigezo anaweza kuwepo pale na kuendesha club kama waliopo hawana vigezo hivyo wakae pembeni kupisha wengine club ni kubwa kuliko wao watafute club nyingine au business nyingine...... 💪🥰🥰
Acha kujiumiza akili kaka,Siasa,biashara na maslahi binafsi ndio vinavyosababisha timu ifikie hapa,,wakisharidhika na kufaidika ndio wataaanza kusikiliza wanachama na mashabiki wanataka nini
 
Eddy de Jr

Mgeni
May 9, 2024
81
14
5
Kama vipi mashabiki GEN Z tuandamane coz hawa wazee naona kama vile wako nyuma ya wakati coz wanafanya mambo kwa mtindo wa kizamani sana.