Nimeshituka kuona seleman matola anaendelea kuwa ni sehemu ya benchi la ufundi kama kocha msaidizi. Sina mashaka na uwezo wa matola , Sina wivu naye , ila simba wangehitaji mabadiliko wangebadili kabisa huu mfumo, what so special kwa matola , makocha karibu nane wameondolewa matola akiwa ni sehemu ya benchi,kwani hakuna makocha wengine wazawa ambao wanaoijua Simba vizuri, ambao watakuwa msaada kwa kocha mpya, ukimsikiliza aliye kuwa kocha wa makipa Simba anadai even video analysit wa timu ni MUNGU mtu pale , kile ni kipimo Cha kuwa Kuna shida kwenye timu kuanzia kwenye management hadi kwa wachezaji, kilichotokea kwa kuwaondoa inonga na chama kuwa sehemu ya timu kinahitajika hata kwenye benchi la ufundi , otherwise tunadanganyana, kwa hali hii Kabla ya Christmas huyu kocha wa Simba hatakuwa sehemu ya timu