Wakati ligi kuu ikiwa inakaribia kumalizika kuna mengi ambayo yanazungumzwa haswa kugombea nafasi ya pili kati ya Azam vs Simba tutazame hiki walichokiandika Shaffih Dauda na kile ambacho amekisema Zaka Zakazi kisha tujadiliane hapa
SHAFFIH DAUDA KAANDIKA:
"Niliposema watu/kampuni nyingi zinatamani Simba imalize nafasi ya pili juu ya Azam FC ili ishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, sikuwa najizungumzia mimi kwamba ndio mnufaika pekee kibiashara bali kuna watu/kampuni/taasisi nyingi zitanufaika na Simba kwa sababu ya fan base yake kuliko Azam FC.
Ukifanya utafiti mdogo kwenye hizi kampuni za TV [Azam TV, DStv, StarTimes] ambazo zinanunua haki za matangazo kuonesha mashindano ya Afrika, ukiuliza kati ya Simba na Azam wangetamani timu gani imalize Ligi katika nafasi ya pili hakuna hata kampuni moja ya TV itakwambia Azam FC!
Kwa nini? Kwa sababu Azam ikimaliza nafasi ya pili na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika ni watu wangapi watalipia ving’amuzi vyao kutazama mechi ya Azam FC vs Petro de Luanda? Lakini vipi kwa Simba?
Kwa sababu hizohizo za kibiashara, hata Azam TV wanatamani sana Simba imalize Ligi ikiwa nafasi ya pili juu ya Azam FC kwa sababu wanajua itawalipa kwenye biashara yao na watapiga mpunga zaidi kupitia subscriptions ya ving’amuzi kuliko timu yao ikifuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bila shaka hata Simba ilipoifunga Azam FC [Azam 0-3 Simba], watu wa Azam TV walifurahi sana wakijua mbio za kuwania nafasi ya pili zimekwisha! Wakiamini biashara yao itachangamka ikifika msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ni kitu kizuri na kikubwa kwa Azam FC kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu ya kujitambulisha na kuweka alama kwenye soka la Afrika kama klabu lakini kibiashara hawauzi sokoni ukilinganisha na Simba."
ZAKA ZAKAZI ANASEMA:
"
SABABU 99 ZA KUKWAMA KWA AZAM FC
Huyu ni Shaffih Dauda, mchanbuzi nguli kabisa wa michezo, hasa mpira, hapa nchini.
Na hapa anaelezea matamanio yake kuelekea kumalizika kwa msimu.
Anasema angefurahi Simba kushika nafasi ya pili kwa sababu za kibiashara.
Naam, ukiacha uchambuzi, Shaffih ni mfanyabiashara mzuri sana wa mpira kupitia wachezaji. Na kama kuna watu ambao Tanzania inatakiwa kuwapa heshima kubwa, basi ni Shaffih.
Ana “connection” kubwa sana na mpira wa dunia…yeye ndiye aliyempeleka Ulaya Novatus Dismass, kutoka Azam FC.
Yeye ndiye aliyempeleka Marekani Cyprian Kachwele kutoka Azam FC.
Hapa Shaffih alifanya biashara kubwa sana. Na biashara hii aliifanya na Azam FC, siyo Simba…na hajawahi kufanya biashara kubwa kama hii na Simba.
Mtu mwingine angetegemea kumsikia Shaffih akisema kwamba kwa maendeleo ya mpira, Azam FC ingepaswa kushika nafasi ya pili, ili ipate nguvu zaidi ya kuzalisha akina Kachwele na yeye afanye biashara zaidi…lakini siyo hivyo.
Shaffih anaombea Simba iliyozuia biashara yake ya Ladaki Chasambi, ndiyo iwe ya pili, ili biashara ifanyike!
Na hii ni nafasi ya pili, hapo bado ubingwa. Unadhani hizo mbio za nafasi ya pili ndiyo zingekuwa za ubingwa…ingekuwaje?
Mimi nimpongeze sana kwa kuwa muwazi kwa sababu kuna wengine wengi sana wanawaza kama yeye lakini hawajatoka hadharani na kusema.
Miongoni mwao kuna wachambuzi kama yeye, kuna wafanyabiashara kama yeye, kuna wanasiasa, kuna wafanya maamuzi, wachungaji na mashehe na kadhalika.
Na kila mmoja katika hao ana sababu zake kwanini Azam FC haistahili kuwa ya pili…achilia mbali ubingwa.
Sababu hizi jumla zinakuwa 99 na kuyafanya maisha ya Azam FC kuwa magumu sana…halafu mwisho wa siku hawa hawa wanakuja kuuliza, Azam FC inakwama wap?
1. Sababu za kibiashara kama Shaffih
2. Sababu za kisiasa
3. Sababu za kidiplomasia
4. Sababu za kiuchumi
5. Sababu za kimazingira
6. Sababu za kijiografia
7. Sababu za kihistoria
8. Sababu za kiintelijensia
9. Sababu za kiusalama
10. Sababu za kiimani
11. Sababu za kimahusiano
12. Sababu za kiitikadi
13. Sababu za kimazoea
14. Sababu za kimataifa
15. Sababu za kiroho
16. Sababu kimiundombinu
17. Sababu zilizo nje ya uwezo
18. Sababu za kimbunga Hid
Wewe Maoni Yako Ni Yapi? Tujadiliane Hapa