Baada ya kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, wawakilishi wa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Simba itakutana na bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Mamelodi Sundowns Womens ya Afrika Kusini leo Novemba, 9, 2022.
Akizungumza Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula alisema kuwa ni shauku yake ya kutaka kufika fainali na kuchukua ubingwa.
“Kila timu imejipanga vizuri, tutacheza na Mamelodi, moja ya timu imara na zenye uzoefu wa kutosha lakini tunaendelea kujipanga ili tufanye vizuri na kutinga fainali,” alisema Lukula.
Ikiwa hii ndo mara ya kwanza Simba Queen kushiriki mashindano hayo ikiwa ni msimu wake wa pili huku mpinzani wao, Mamelodi akishiriki kwa mara ya pili baada ya kubeba ubingwa mwaka jana nchini Misri.
Simba Queen walikua kundi A na match yao ya wisho walikipiga na timu ya Buffalloes ambayo iliisha kwa ushindi wa 2-0 na kushika namba 2 , huku AS FAR kushika nafasi ya 1 kwenye kundi na wote kupata nafasi ya kufika nusu fainal Simba mpinzani wake akiwa ni Mamelodi Sundowns, waliowapiga TP Mazembe ya Congo goli 4-0 kwenye mchezo wa mwisho wakiwa kundi B.