Tanzania ingenunua Bitcoin za milioni 200 mwaka 2011 leo tungekua mbali

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
47
9
26
Dar es Salaam
Hesabu hazidanganyi..

Mwaka 2011 bei ya Bitcoin ilikua around 1usd per coin. Sasa tuchukulie nchi ya Tz ingetoa walau 200mil na kununua bitcoin (badala ya kumnunulia DED au DC v8 la kutembelea)..

200mil ni sawa na 86,956 usd (tuchukulie 1usd ni 2,300 Tsh).

Kwa bei ya 1usd per bitcoin maana yake Tanzania ingekua na umiliki wa bitcoins 86,956 kwa sasa!!

Sasa bei ya bitcoin moja kwa sasa ni around 60,000 usd.

Kwa bitcoin 86,956 ina maana leo hii Tz ingekua dola za marekani 86,956 x 60,000 = 5,217,391,304.35 cash!!

Sasa hizo ni USD tuzi badili ziwe Tsh...

5,217,391,304.35 x 2,300tsh = 12,000,000,000,000 Tsh!

Mimi sio mhasibu lakini nadhani hapo inasomeka trillion kumi na mbili net!

Kama nchi tungekua na 12trillion ina maana leo...

1. Tusingekua tunapitisha bakuli kwa mabeberu kuomba msaada wa kujenga stiglazi goji.

2. Tusingekua tunahangaika kuomba misaada kujengewa miradi ya maji.

3. Reli ingejengwa bila kungoja misaada

4. Tusingengojea misaada ili kujenga vyoo mashuleni.

Nk nk nk!

NB: Lazima tufikirie dunia inaenda kasi kweli kweli!