Tanzania na Ukuaji wa Soko la Ubashiri Mitandaoni.

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
tangazopiic

MICHEZO ya kubashiri mitandaoni ni tasnia mpya nchini Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika. Licha ya upya wake, hii ni miongoni mwa tasnia inayokua kwa kasi zaidi hapa nchini.
Michezo ya kubahatisha mtandaoni inahusisha kubashiri matokeo ya michezo, kucheza kasino, michezo ya poka, roulette au michezo ya video za mitandaoni na michezo mingine. Lakini wateja wengi nchini Tanzania hujihusisha zaidi na ubashiri wa matokeo ya michezo na kasino za mitandaoni.
Kushinda pesa kwenye bahati nasibu kunaweza kubadilisha maisha yako kwa namna nyingi. Zipo hadithi nyingi nzuri na zenye kuhamasisha kuhusu washindi wa michezo ya kubashiri mtandaoni ambao wametumia pesa zao vizuri na kubadilisha maisha yao na ya wale wanaowazunguka.
“Wanasema kwamba pesa hainunui furaha. Mimi katu sikubaliani na jambo hilo, kuna kipi kinaleta furaha zaidi ya ukweli kwamba kiasi cha shilingi 4,000 tu zimeweza kubadili maisha yangu kutoka kuwa mtu ninayedharaulika sana mpaka kuwa mtu ninayeheshimika zaidi?”, anasimulia ndugu Anthony Manongi, mshindi wa pesa nyingi kwenye kasino ya mtandaoni.
Ndugu Manongi ni mfano dhahiri wa washindi wengi wa pesa nyingi katika michezo ya kubashiri ambao pesa hazikuwabadilisha kwa ubaya.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Tovuti ya Roulette, Soko la Michezo ya Kubahatisha Tanzania.​

Mojawapo ya sababu zinazochangia zaidi kuongezeka kwa michezo ya kubashiri mitandaoni ni ukuaji wa utandawazi na teknolojia nchini Tanzania.
Mwishoni mwa miaka ya 1990, Tanzania, kama nchi nyingine za Kiafrika iliruhusu bahati nasibu kwenye michezo na matumizi ya juu ya utumiaji wa mitandao nchini yaliambatana na kuhama kwa upepo wa namna ya kucheza michezo ya kubashiri kutoka madukani mpaka kwenye mtandao.
Badala ya kupanga foleni katika majumba ya kuchezeshea michezo ya bahati nasibu au kasino za madukani, siku hizi wateja wa kubashiri Tanzania wanaweza kumaliza hamu zao kwa urahisi tu kupitia sehemu nyingi kama vile ukurasa huuambao ni mojawapo ya tovuti za kuhusu roulette na michezo ya kasino bila ya kupata bugudha yoyote.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kubashiri Mtandaoni na Teknolojia ya Miamala ya Pesa kwa Njia ya Simu.​

Ukuaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi umekua ni mojawapo ya fursa adhimu kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa na huduma zao kwa urahisi zaidi. Mojawapo ya sekta zinazonufaika zaidi kwa kupitia teknolojia hii ni ubashiri wa mtandaoni.
Miamala ya pesa kwa njia ya simu imekuwa ni njia ya malipo katika kampuni nyingi za kubashiri mtandaoni. kama ilivyoelezwa hapo awali, michezo ya kubahatisha imekua kwa kasi zaidi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, ongezeko la matumizi ya mitandao pamoja na huduma za kifedha za simu.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Michezo Maarufu zaidi ya Kubashiri Mtandaoni.​

Ingawa kubashiri matokeo ya michezo ndio sehemu maarufu zaidi, sekta hii ya kubashiri mtandaoni inahusisha michezo mingine mashuhuri, rahisi na pengine yenye nafasi kubwa zaidi ya ushindi kuliko kubashiri matokeo ya michezo. Ifuatayo ni michezo ya mtandaoni ambayo inapatikana zaidi kwa mazingira ya Tanzania:

  • Roulette
Roulette ni mojawapo ya michezo ya mezani inayochezwa zaidi katika kasino za mtandaoni na madukani nchini Tanzania. Kuna aina nyingi sana za roulette duniani kote lakini zinazochezwa zaidi Tanzania ni:

  1. Roulette ya Ulaya
Hii ni mojawapo ya Roulette maarufu zaidi hasa kutokana na urahisi wa kushinda kwa wateja. Gurudumu la aina hii ya roulette limegawanywa katika vijisanduku vyenye namba kuanzia 1 hadi 37, vyekundu na vyeusi. Ili kushinda katika roulette hii unaweka dau kwenye namba ambapo anatabiri mpira utaangukia wakati gurudumu litakapoacha kuzunguka. Pia, unaweza kuweka dau kwenye rangi ambayo unafikiri mpira utaangukia.
  1. Roulette ya Ufaransa
Mchezo wa roulette ya Ufaransa una gurudumu sawa na la roulette ya Ulaya kwani nayo ina vijisanduku 37. Namba 1 hadi 36 zina rangi nyeusi au nyekundu na sehemu moja ya sifuri ina rangi ya kijani.



  1. Roulette ya Marekani
    Roulette ya Marekani ni tofauti kidogo na roulette nyingine kwani yenyewe inajumuisha namba 38, 1-36 (kijani na nyekundu), 0 (kijani), 00 (kijani). Sheria zinabakia sawa na uchezaji ni sawa na ule wa aina nyingine.

  • Kasino za Mtandaoni
Licha ya kuwa na kasino nyingi za mtaani kote nchini pia kuna idadi kubwa na ya kuridhisha ya tovuti za kasino zilizoidhinishwa.

Kasino ya mtandaoni ina faida nyingi kulinganisha na kasino za madukani. Faida mojawapo ni kuwa kasino ya mtandaoni ni kuwa mchezaji anao uhuru wa kucheza hata akiwa nyumbani bila kulazimika kutafuta jumba la kasino. Ili uweze kucheza kamari katika kasino ya madukani itakubidi utembelee kasino iliyo karibu na wewe, na ukweli ni kwamba sio mara zote utakua katika mazingira hayo. Lakini pia nchini Tanzania kasino zinapatikana kwa uchache sana hasa katika miji mikubwa tu kama Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Arusha na Mwanza!

Faida nyingine ya kasino ya mtandaoni ni uwepo wa njia nyingi mbalimbali za kuweka na kutoa pesa. Kasino nyingi za mtandaoni nchini hupokea malipo na kutoa pesa kutumia njia kama vile:

  1. Visa
  2. Mastercard
  3. Malipo ya njia ya simu
  4. Skrill na
  5. Bitcoin

 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Sio Burudani Pekee.​

Moja ya kadhia kubwa wanayokumbana nayo wateja wa kampuni zinazojihusisha na michezo ya kubashiri ni ile dhana ya wengi kuwa kubashiri ni jambo la kupoteza muda tu na ni kazi inayofanywa na watu waliopoteza ramani maishani!
Sio kweli kwamba kila anayejishughulisha na ubashiri mtandaoni hana ajira. Ikumbukwe kuwa Tanzania inapitia ukuaji wa haraka sana wa miji, hali inayopelekea ajira nyingi zaidi ambazo zinachangia ukuaji wa mapato yanayoweza kutumika kwa shughuli za burudani ikiwemo kubashiri mtandaoni.
Kama ilivyo katika starehe nyingine, watu wasio na ajira hawakatazwi kujihusisha na masuala ya ubashiri wa mtandaoni. Tofauti ya starehe nyingine na hii ni kuwa hapa mchezaji haishii kupoteza pesa lakini anaweza kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa kama akiwa na nidhamu ya namna ya kucheza.
Zaidi ya watu 30,000 nchini Tanzania wameajiriwa katika makampuni yanayojihusisha na michezo ya kubashiri mtandaoni. Hii ina maana kwamba michezo ya kubahatisha inakuwa chanzo muhimu cha ajira. Sekta hii kwa sasa inachangia zaidi ya 3% ya pato la taifa kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Changamoto za Soko la Ubashiri Mtandaoni​

Licha ya kutambuliwa rasmi na serikali nchini Tanzania, sekta ya ya ubashiri mtandaoni inakabiliwa na vikwazo vingi katika ukuaji wake. Changamoto moja kubwa inayoikumba tasnia hii ni pamoja na kuibuka kwa kasino nyingi ambazo baadhi yake hazina ubora hali inayopelekea kasino nyingi kupoteza umaarufu miongoni mwa wateja wao. Hata hivyo, baadhi ya tovuti za roulette kama zilivyoorodheshwa katika ukurasa huu zimezidi kuwa bora na kuwavutia sana wateja.
Lakini pia kwa vile kasino za mtandaoni zinapatikana zaidi, pia kuna ongezeko kubwa la uraibu kwa wateja wa michezo ya kubashiri mtandaoni. Ni muhimu kwa wateja kujifunza juu ya dhana za uwajibikaji na kucheza kistaarabu ili kuepusha dhana mbaya zinazozunguka ubashiri wa mtandaoni kwani nayo ni starehe kama zilivyo starehe nyingine. Na zaidi ya yote, ikifanyika vizuri kwa ustaarabu ni chanzo cha mapato kwa wachezaji.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kuepuka Uraibu wa Michezo ya Kubashiri Mtandaoni​

“Daah, mimi nimejaribu kupunguza kucheza michezo ya kubahatisha kwa muda wa miaka 6 sasa ila nimeshindwa, ni kama nimekuwa teja kwani nikipata hela yote tu ninachezea mpaka nimepoteza familia yangu yaani mke na mtoto, kwa kweli mpaka pesa ya kula tulikuwa tunakosa kabisa. Nimejaribu kupunguza ila nimeshindwa!” – Jonasi Kagori
Je, wewe binafsi umeshapatwa na hali kama hii au mtu wako wa karibu ana hali kama hii? Unagundua umeshakuwa na uraibu au uteja wa kitu fulani pale ambapo unashindwa kuacha kukifanya au kukitumia kitu hicho hata kama kinakupatia hasara au kukuumiza kama ilivyokuwa kwa ndugu Kagori.

Haya ni mapendekezo yetu ya kanuni za kuzifuata ili uweze kufurahia michezo ya kubashiri mitandaoni huku ukiwajibika:
  • Michezo ya kubahatisha ni ya kujifurahisha, si njia pekee ya kujipata pesa;
  • Hakikisha kwamba unacheza wakati ukiwa umetulia na kuwa na amani;
  • Jipe muda wa mapumziko ya kawaida;
  • Amua mapema jinsi ambavyo hasara zako zinavyoweza kuwa ni kubwa;
  • Kamwe usicheze ukiwa umelewa au ukiwa na ushawishi wa vitu vingine;
  • Kamwe usicheze ukiwa na huzuni au mfadhaiko;
  • Kabla ya kuanza kucheza, amua ni kiasi gani cha kushinda ambacho utamaliza kwenye mchezo;
  • Usiongeze kikomo cha juu cha pesa za kutumia kwenye ubashiri wa mitandaoni ambacho umeamua kukiweka wewe mwenyewe; na
  • Amua mapema juu ya kiwango chako cha kila mwezi cha kutumia kwenye michezo ya kubashiri mitandaoni. Bila ya kujali kiwango chako cha kawaida cha miamala ya kutumia kubashiri, unaweza kuweka kiasi cha chini kama kikomo chako binafsi.
Kwa msaada zaidi na ushauri kuhusu michezo ya kubashiri mtandaoni, tafadhali tembelea BeGambleAware na GamStop.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Hitimisho​

Kwa ongezeko la vijana ambao wanapenda kujihusisha na ubashiri mtandaoni pamoja na ukuaji wa miji tutegemee kuona kampuni nyingi za kubashiri mtandaoni zikiibuka nchini Tanzania.

Ni jukumu la mamlaka za Serikali, hususani Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuhakikisha sekta hii inadhibitiwa vyema ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa haihusishi watoto walio chini ya umri wa miaka 18.