
MICHEZO ya kubashiri mitandaoni ni tasnia mpya nchini Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika. Licha ya upya wake, hii ni miongoni mwa tasnia inayokua kwa kasi zaidi hapa nchini.
Michezo ya kubahatisha mtandaoni inahusisha kubashiri matokeo ya michezo, kucheza kasino, michezo ya poka, roulette au michezo ya video za mitandaoni na michezo mingine. Lakini wateja wengi nchini Tanzania hujihusisha zaidi na ubashiri wa matokeo ya michezo na kasino za mitandaoni.
Kushinda pesa kwenye bahati nasibu kunaweza kubadilisha maisha yako kwa namna nyingi. Zipo hadithi nyingi nzuri na zenye kuhamasisha kuhusu washindi wa michezo ya kubashiri mtandaoni ambao wametumia pesa zao vizuri na kubadilisha maisha yao na ya wale wanaowazunguka.
“Wanasema kwamba pesa hainunui furaha. Mimi katu sikubaliani na jambo hilo, kuna kipi kinaleta furaha zaidi ya ukweli kwamba kiasi cha shilingi 4,000 tu zimeweza kubadili maisha yangu kutoka kuwa mtu ninayedharaulika sana mpaka kuwa mtu ninayeheshimika zaidi?”, anasimulia ndugu Anthony Manongi, mshindi wa pesa nyingi kwenye kasino ya mtandaoni.
Ndugu Manongi ni mfano dhahiri wa washindi wengi wa pesa nyingi katika michezo ya kubashiri ambao pesa hazikuwabadilisha kwa ubaya.