TOVUTI UNAZOWEZA KUUZA NA KUNUNUA CRYPTO (Sehemu ya Kwanza)

JimNicklaus

Administrator
Staff member
Nov 30, 2021
13
2
5
Dar Es Salaam
Niaje wadau leo nawasogezea jukwaa mojawapo unaloweza kuuza na kununua Sarafu za kidijitali (Cryptocurrencies) kwa urahisi zaidi.

LOCALBITCOIN

Jukwaa hili unaweza kununua na kuuza cryptocurrency kupitia mawakala wanaopatikana humo. Sarafu unazoweza kununua kupitia mtandao huu kwa sasa ni Bitcoin. Cha msingi cha kuzingatia unapotaka kuweka oda yako ya kuuza au kununua ni chagua muuzaji au mnunuaji ambaye ameshafanya miamala mingi zaidi na pia akiwa na maoni mazuri kutoka kwa watu aliofanya nao biashara. Ili uweze kuruhusiwa na kuongezewa kiwango cha kuuza au kununua cryptocurrency kupitia jukwaa hili inabidi uthibitishe akaunti yako na mahali unapoishi kwa kutumia kitambulisho chochote kilichotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Kitambulisho cha Taifa, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria. Na upande wa kuthibitisha mahali unapoishi unaweza tumia kumbukumbu za mialamala yako ya kibenk (Bank Statement).

Kwa swali lolote ulilonalo au changamoto yoyote unaweza uliza chini kwenye comments.