Ukweli usemwe mapema, tusifiche mambo. Kukua kwa soka letu kunahitaji misingi imara ya uongozi ndani ya chama cha soka.
Matunda ya soka tuliyonayo sasa ni matokeo ya uongozi imara wa TFF kipindi cha urais wa Tenga ambao kwa makusudi kabisa ulianza upya kwa kujenga misingi imara ya uongozi wa kisoka. Yule alikuwa mwamba haswaa. Na uongozi ule uliletwa na wapenda soka, wacheza soka wa zamani na wadau mbali mbali wa soka. Tenga bila kuonyesha tamaa, wakati bado wadau walikuwa wanamhitaji aliamua kung'atuka mara baada ya kipindi chake cha pili cha uongozi kwisha. Michezo ya rushwa na zengwe katika kuwania uongozi wa soka ilifutika kwa sehemu kubwa sana kupitia uongozi wa Tenga.
Kwa sasa TFF tuna Karia, ambapo kipindi chake cha pili cha uongozi kilitokea kwa utata mkubwa, mara baada ya wagombea wengine wote kuenguliwa kwa zengwe kubwa mnoo na Karia kubakia yeye mwenyewe.
Sasa uchaguzi wa TFF unakwenda kufanyika tena, sarakasi zile zile za miaka minne iliyopita za uongozi wa Saria zimerejea tena, ni mwendo wa mizengwe na rushwa tupu. Ni wazi hakuna mgombea atayepitishwa kugombea zaidi ya Karia mwenyewe.
Kwa mtazamo wangu, Karia hana mpango wowote wa kuondoka madarakani pale TFF, iwe sasa au hapo baadaye, uongozi wake hauko tayari hata kidogo kuruhusu uchaguzi huru na haki pale TFF. Namna pekee ya huu uchaguzi kuwa huru na haki ni uongozi wote wa Saria kutemeshwa bungo na asigombee kabisa ili kupisha watu wengine wapya kugombea.