UEFA Champions League

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Kutokana na tatizo la kiufundi la programu ya mtoa huduma wa nje inayowaelekeza viongozi ni timu zipi zinafaa kuchezeana, hitilafu ilitokea katika droo ya hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League.
Kutokana na hili, droo imetangazwa kuwa batili na itafanywa upya saa kumi na moja jioni.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Mashindano ya champions leagues hatua ya 16 bora kuanza tena leo.
3zw39LPg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

PSG YAICHAPA REAL 1-0, MESSI AKOSA PENALTI.​

AVvXsEhQnQJciFg5dEs13Ye5BB0EM7FKXVdjjHUpjpEdY1KHp--Br3gWZpExQGK_0dhgAtyIgZAdaZznq0WOToveNb6m7pVgRE93DgbRvmA2vraWvmVnNfrbiTls5g5gvokpc-_wE00it2rvuzGhX6oY6XMnNuCw0Rn7F3TtSJpkWJgN27tdvRGYturmSkmZ=w640-h444

WENYEJI, Paris Saint-Germain wamepata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa.
Bao pekee la PSG limefungwa na Kylian Mbappe dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Muargentina Lionel Messi alikosa penalti baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa Thibaut Courtois.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki Dani Carvajal kumchezea rafu Mbappe kwenye boksi dakika ya 62.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAWAPIGA SPORTING 5-0 URENO.​

AVvXsEiBg1M9skruKmN6sD7fH2sPK6EtlUWu4B3Cd-EX9ghUjfAh9q-F0rNsxGspN2Od1qol_wVCCarhIxcGczesFlZL0PbOQPsMQlpxH12SKVDGm6menx7CTz5qbTjuTZnrw9qXLZusYesqMaQrs4dHwJRQNV4Nq_G5dUHBfGBA9rPVtJ0BgeqxLmPOMFuu=w640-h442

TIMU ya Manchester City imewaadhibu wenyeji, Sporting Lisbon kwa kuwachapa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa José Alvalade Jijini Lisbon, Ureno.
Mabao ya Man City yamefungwa na Riyad Mahrez dakika ya saba, Bernardo Silva dakika ya 17 na 44, Phil Foden dakika ya 32 na Raheem Sterling dakika ya 58.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YAICHAPA INTER MILAN 2-0 ITALIA.​

AVvXsEjJRDWf9PUQ7ao9qjv_0i6UWbqc7fMAI_dyNde6S3t1to3knOaqKIrxzfHV1Ov0wTdA49VgcrcjG1ryRPI76JEuo0Is2yw6sSFJCJKrr3luIb9I1oGnuc8q9FNbQ9-97Y1L8ebqe1dG8uG2GFAbHKIhDtVDG_T_-nwth-fcFQEniS3b6ZCAHp8v2RJJ=w640-h426

TIMU ya Liverpool imetanguliza mguu mmoja Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Inter Milan usiku wa Jumatano Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan nchini Italia.
Katika mchezo huo wa kwanza Hatua ya 16 Bora, mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 75 na Mohamed Salah dakika ya 83.
Mechi nyingine ya 16 Bora jana, wenyeji, Red Bull Salzburg wamelazimishwa sare ya 1 -1 na Bayern Munich Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Wals-Siezenheim.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Fc Bayern Munich katika Uefa Champions League msimu huu:
Barcelona 0-3 Bayern
Bayern 5-0 Dynamo Kyiv
Benfica 0-4 Bayern
Bayern 5-2 Benfica
Dynamo Kyiv 1-2 Bayern
Bayern 3-0 Barcelona
RB Salzburg 1-1 Bayern
Watoto wadogo RB Salzburg wamewazuia Fc Bayern
🇩🇪
kuondoka na ushindi hapo jana na kusitisha rekodi ya wajerumani hao kuendelea kushinda mechi nyingi mfululizo.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Mbappe ashangilia kuwapiga Madrid.​

Mbappe PIC


PARIS, UFARANSA. KYLIAN Mbappe ameshangilia kwa nguvu sana baada ya kuipiga bao la dakika za mwisho Real Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa timu 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa juzi Jumanne.
Na staa huyo wa Paris Saint-Germain kisha alikiri kwamba huenda akawagomea Real Madrid kwenda kujiunga nao bure kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu huu.
Mechi hiyo ilionekana kama ingemalizika kwa sare ya 0-0, hadi hapo Mbappe alipofanya maajabu yake kwenye dakika za majeruhi.
Mbappe, 23, amekuwa akihusishwa sana na Real Madrid hasa katika kipindi hiki ambacho mkataba wake huko PSG utafika tamati mwisho wa msimu. Lakini, mchezaji huyo hakuonyesha dalili yoyote ya kushusha kiwango chake wakati alipokumbana na kikosi hicho cha Los Blancos kinachonolewa na Carlo Ancelotti kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya mtoano juzi.
Baada ya Lionel Messi kukosa penalti, Mbappe alikuwa mtu wa mwisho kuamua matokeo ya mechi hiyo, akifunga kwenye dakika 93. Na baada ya kufunga, Mbappe hakujivunga kwenye kushangilia, alifanya hivyo kwa nguvu kubwa mbele ya mashabiki huko Parc des Princes.
Mbappe alitumia pia ukurasa wake wa Twitter kuandika baada ya mechi: “Ushindi wa raundi ya kwanza. Hii ni Paris.”
Kisha akaiambia Movistar: “Bado sijaamua hatima yangu. Naichezea PSG, moja ya klabu kubwa duniani. Mechi hii itaamua hatima yangu? Hapana.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Mourinho Aiponda PSG vs Madrid.​

767474-jose-mourinho-troubled-reuters.jpg

JOSE Mourinho, Kocha wa AS Roma, amesema hakufurahishwa na mchezao kati ya PSG dhidi ya Real Madrid, huku akidai kwamba hajamisi kuwa ndani ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mourinho kwa sasa anainoa Roma ambayo haipo kwenye michuano hiyo, huku ikishiriki Europa Conference League.
Jumanne ya wiki hii, PSG iliifunga Real Madrid bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Nimekuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya nikisimamia mechi zaidi ya 150, hivyo sina presha, kwa sasa siwezi
kuanza kulia eti sababu kwa timu yangu ipo Europa au Conference League.

“Sijafuatilia mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ila sikupenda mechi ile ya PSG na Real Madrid
hata kidogo, walau mechi ya Inter Milan na Liverpool ilikuwa ni bora na nzuri,” alisema Mourinho ambaye aliwahi kuinoa Real Madrid kuanzia 2010 hadi 2013.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CHELSEA YAICHAPA LILLE 2-0 LONDON​


WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na Kai Havertz dakika ya nane na Christian Pulisic dakika ya 63 na kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi watahitaji sare ugenini ili kwenda Robo Fainali.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Fainali UEFA kupigwa Ufaransa​

UEFA PIC

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la soka Ulaya, UEFA imeamua kuhamisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Wanaume ya UEFA 2021/22 kutoka Saint Petersburg hadi Stade de France huko Saint-Denis baada ya kufanya kikao leo, asubuhi.
UEFA iliitisha mkutano wa dharula jana, Alhamisi ili leo, Ijumaa kujadili mpango wa kuhamisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia uamuzi wa Russia kutangaza vita dhidi ya Ukraine. Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Mei 28, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho hilo baada ya kikao hicho cha dharula, inaeleza kuwa, "UEFA inapenda kutoa shukurani zake na shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kwa usaidizi wake binafsi na kujitolea kufanya mchezo wa kifahari wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kuhamishiwa Ufaransa."
"Pamoja na serikali ya Ufaransa, UEFA itaunga mkono kikamilifu juhudi za washikadau mbalimbali ili kuhakikisha utoaji wa uokoaji kwa wachezaji na familia zao nchini Ukraine ambao wanakabiliwa na mateso makubwa ya kibinadamu," taarifa hiyo ilieleza.
Katika mkutano huo kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kamati ya Utendaji ya UEFA pia iliamua kwamba klabu za Ukraine na Russia na timu zao za taifa zitatakiwa kucheza michezo ambayo itawakutanisha nje ya mataifa yao hadi taarifa nyingine itakapotolewa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Usiku wa Ulaya, kuna watu wanaaga huko​

UEFA PIC


PARIS UFARANSA. NA leo tena. Ni kuhusu mchakamshaha wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo usiku wa leo Jumanne na kesho Jumatano zitapigwa mechi za marudiano za hatua ya 16 bora.
Shughuli inawasubiri RB Salzburg kuona kile kitakachowatokea huko Allianz Arena wakati watakapokwenda kuwakabili Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kwenye mechi ya kwanza, Bayern Munich ililazimika kusawazisha dakika za mwisho kwenye sare ya 1-1, huku utaratibu wa msimu huu kwenye michuano hiyo ya Ulaya, bao la ugenini halina nguvu yoyote. Kipute hicho kitapigwa usiku wa leo Jumanne.
Mashabiki wa michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya watapata uhondo mwingine wakati Liverpool watakapojirusha uwanjani kwao Anfield kurudiana na Inter Milan.
Kwenye mechi ya kwanza, Liverpool ilipata ushindi wa mabao 2-0 uwanjani San Siro, hivyo kinachosubiriwa ni kuona kama Inter itaweza kupindua mechi ugenini ili kusonga hatua inayofuata ya michuano hiyo yenye upinzani mkubwa huko Ulaya. Wataweza?
Manchester City ikiwa kwenye kiwango bora kabisa itakuwa uwanjani Etihad kuwakaribisha Sporting CP kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ikitokea kuichapa Manchester United 4-1 kwenye Ligi Kuu England, Man City itarudi kwenye michuano ya Ulaya usiku wa kesho Jumatano kurudiana Sporting, ambapo kwenye mechi ya kwanza ilishinda mabao 5-0 ugenini. Labda itakee maajabu, lakini kwa kawaida tu, Man City itacheza kukamilisha ratiba kabla ya kutinga kwenye hatua inayofuata ya robo fainali.
Shughuli pevu zaidi kwa hiyo kesho itakuwa huko Bernabeu, ambapo mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid itakaposhuka uwanjani kuikaribisha Paris Saint-Germain iliyosheheni mastaa kibao kwenye kikosi chake.
PSG yenye mastaa matata kama Neymar, Lionel Messi na Kylian Mbappe watakwenda kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Parc des Princes. Macho ya wengi watakuwa huko Bernabeu kuona kama Carlo Ancelotti na chama lake la Los Blancos ataweza kupindua meza dhidi ya masupastaa hao wa Mauricio Pochettino.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LEWANDOWSKI AWEKA REKODI MPYA YA HAT TRICK ULAYA​

AVvXsEgUbs1Zycv0UZau8ofzfysbTG8l0XdRQfR571UFTPY1cWIEJWa9m7lFPTZ1ueazlb1GWBXgo12SUAWYeTMn-cUVsKNxiu4N-aIhv3msaT_xm_6N7ooG7ojsLuW4bzLBwVvAds3MAZngmLdC9u0Y3cFcZ5si11PFzkJRoL6aFnkMq9F4TPEHwUymYABh=w640-h484

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana akiiwezesha Bayern Munich kutinga Robo Fainali kwa ushindi wa 7-1 dhidi ya RB Salzburg.
Katika mchezo huo wa marudiano Hatua ya 16 Bora usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Lewandowski alitumia dakika ya 23 tu za mwanzo kufunga mabao yote matatu, akivunja rekodi iliyokwekwa Marco Simone ya kutumia dakika 24 kupiga hat-trick akiwa na AC Milan dhidi ya Rosenborg b mwaka 1996.
Lewandowski alifunga dakika ya 12 na 21 kwa penalti na lingine dakika ya 23, wakati mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Serge Gnabry dakika ya 31, Thomas Muller dakika ya 54 na 85 na Leroy Sané dakika ya 85, wakati bao pekee la RB Salzburg lilifungwa na Maurits Kjaergaard dakika ya 70.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YASINDIKIZWA ROBO FAINALI NA BAKORA​

AVvXsEgACyGaa5iXbJN77EmEmbpI0TSKxaMj5J_lzYcu7VlZw0vxSB69QRbe3m8tVmecpvC5IMsx8pYU8VPCQh8XnP4Y9_L6NUlaOKtTUe_BoD7tSxVi3GKMPRIhklLA7lwHr0Zd4Lir7QwJ3NHTHXh_-4Gj5bKNuWaHHLqGvwoNpZ2m5yPvqmnS0mONAydB=w640-h424

WENYEJI, Liverpool wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa 1-0 na Inter Milan ya Italia usiku wa jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool, England katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora.
Bao pekee la Inter jana lilifungwa na Lautaro Martinez dakika ya 61, kabla ya timu hiyo ya Milan kupata pigo kufuatia mshambuliaji wake, Alexis Sanchez kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 63 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Liverpool inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Milan, mabao ya Roberto Firmino na Mo Salah.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BENZEMA APIGA HAT TRICK REAL YAICHAPA PSG 3-1​

AVvXsEi7tTefqUnsC93hcM5aqCLYgsSxqnX27ORL1_nrRxiZe6kPZNxZIo4jDvWrsPh1zQx2Ig7Rh4cVYTE5uoLd5VLJ_SqpPdafUMoXI9vswfImypIcRBBq0mRK4R3R1bcXCCZ5-HCNW5KUYOF_PjqC5avBt6tSeoIJXe0eYdhl0ASpZSMmGPO8BtUqxBnK=w640-h428

WENYEJI, Real Madrid wametinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Paris Saint-Germain usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.
Mabao yote ya Real Madrid yamefungwa na mshambuliaji mkongwe Mfaransa, Karim Benzema dakika za 61,76 na 78 baada ya PSG kutangulia kwa bao la mshambuliaji Mfaransa pia, Kylian Mbappe dakika ya 39.
Real wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ufaransa, bao la Mbappe.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAN YAILAZA ATLETICO MADRID 1-0 ETIHAD​



BAO pekee la Kevin De Bruyne dakika ya 70 jana liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

LIVERPOOL YAICHAPA BENFICA 3-1 LISBON​


TIMU ya Liverpool imeendeleza ubabe baada ya jana kuwachapa wenyeji, Benfica mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa da Luz Jijini Lisbon, Ureno.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Ibrahima Konate dakika ya 17, Sadio Mane dakika ya 34 na Luis Diaz dakika ya 87, wakati la Benfica lilifungwa na Darwin Nunez dakika ya 49.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Ratiba ya mechi za leo za Uefa Champions League
🏆

Real Madrid
🇪🇸
vs. Chelsea
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

(Agg 3-1)
Fc Bayern Munich
🇩🇪
vs Villarreal
🇪🇸

(Agg 0-1)
Mechi zote ni saa 4:00 usiku
#UCL
278185346_5258321557561085_110853779636584452_n.jpg