UEFA Champions League

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BENZEMA AIPELEKA REAL NUSU FAINALI, BAYERN OUT​


WENYEJI, Real Madrid wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa mabao 3-2 na waliokuwa mabingwa watetezi, Chelsea usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dakika ya 15, Antonio Rudiger dakika ya 51 na Timo Werner dakika ya 75, wakati ya Real Madrid yalifungwa na Rodrygo dakika ya 80 na Karim Benzema dakika ya 96.
Baada ya The Blues kumaliza wanaongoza 3-1, mechi iliongezewa dakika 30, kwa sababu matokeo ya jumla yalikuwa 4-4.
Real wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya kuwachapa mabingwa hao wa msimu uliopita 3-1 kwenye mechi ya kwanza Jumatano iliyopita Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mechi nyingine ya jana, wenyeji Bayern Munich wametupwa nje baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Villarreal, hivyo kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia kuchapwa 1-0 Hispania kwenye mechi ya kwanza.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAITOA, ATLETICO SASA KUIVAA REAL​


TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Atletico Madrid usiku wa Jumatano Uwanja wa Wanda Metropolitano Jijini Madrid, Hispania.
Man City wananufaika na ushindi mwembamba wa nyumbani, 1-0 wiki iliyopita bao pekee la Kevun De Bruyne dakika ya 70 na sasa watamenyana na Real Madrid iliyowatoa mabingwa watetezi, Chelsea.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

FIRMINO AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA​


WENYEJI, Liverpool wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya sare ya 3-3 na Benfica ya Ureno usiku wa Jumatano katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Uwanja wa Anfield, Liverpool, England.
Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-4 kufuatia kuwachapa 2-1 Benfica kwao wiki iliyopita.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Ibrahima Konate dakika ya 21 na Roberto Firmino mawili, dakika ya 55 na 65, wakati ya Benfica yamefungwa na Goncalo Ramos dakika ya 32, Roman Yaremchuk dakika ya 73 na Darwin Nunez dakika ya 81.
Sasa Liverpool itakutana na Villarreal ya Hispania iliyoitoa Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla la mabao 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na sare y 1-1 Ujerumani juzi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAICHAPA REAL MADRID 4-3 ETIHAD​


WENYEJI, Manchester City jana wamepata ushindi wa 4-3 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad, Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya pili, Gabriel Jesus dakika ya 11, Phil Foden dakika ya 53 na Bernardo Silva dakika ya 74.
Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 33 akimalizia pasi ya Mfaransa mwenzake, beki Ferland Mendy dakika ya 33 na la penalti ya Panenka dakika ya 82 na lingine Vinícius Júnior dakika ya 55.
Timu hizo zitarudiana Mei 4 Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid.