Ulaghai wa Sarafu za Kidijitali na Jinsi ya Kuepuka Sehemu ya Kwanza

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam

1. Ulaghai wa Utoaji Awali wa Sarafu (Initial Coin Offerings)​

Initial-coin-offering.jpg


Utoaji Awali wa Sarafu (ICOs) ni njia ambayo kampuni nyingi za blockchain hutumia ili kuchanga fedha. Ni mbinu iliyoundwa kuakisi Utoaji wa Awali wa Umma (IPO) kwa mujibu wa soko la hisa. Tofauti na IPOs, ICOs haina udhibiti na huendeshwa kimataifa. Pia, kampuni zinazohusika katika ICOs hazitakiwi kutoa maelezo yoyote ya mapato yao na hali yake ya kibiashara. Nyingi ya kammpuni hizi pia hazina maelezo haya.

Katika miaka michache iliyopita, wawekezaji wameweka takriban dola bilioni 10 kwa ICOs. Katika 2017, Block.one iliweza kuchangisha zaidi ya dola bilioni 4 kutoka kwa wawekezaji. Hii ni robo ya kiasi ambacho Alibaba walizalisha kutokana na IPO yake katika 2014. Telegram, program maarufu ya ujumbe, iliweza kuchangisha zaidi ya dola bilioni 1.7 katika ICO.

Kwa bahati mbaya, watu wengi waliowekeza fedha zao katika baadhi ya ICOs walipoteza fedha hizo. Isitoshe, hivi karibuni kampuni ya Block.one ililazimishwa kutatua maswala na Tume ya Kudhibiti Ubadilishanaji wa Hisa ya Marekani (SEC) kwa kufanya kushiriki mauzo ya hisa bila udhibiti.

Sababu inayofanya ICOs kuwa ulaghai ni kwamba hatua za kuzindua huwa rahisi sana. Mtu yeyote anaweza kutumia vielelezo vingi vya ICO ambavyo vinapatikana mtandaoni na kuwadanganya watu. Kwa sababu hii, mwaka 2017, kampuni iitwayo Useless Coin iliweza kupokea zaidi ya dola elfu 54 kutoka kwa wawekezaji. Katika tovuti yake, kampuni hii ilikuwa iliwaambia wawekezaji kwamba ingetumia mapato hayo “kununua vitu fulani.”

Ili kujikinga na ulaghai wa ICO, tunapendekeza kwamba usijihusishe kabisa na shughuli kama hizo. Puuza mitandao inayoonekana kuvutia, timu ya watu wanaoonekana wema kwenye wavuti wao, na bidhaa bandia wanazouza.