Umeshasahau Saidoo alipokwenda kwa makolo alikua mpya mlimzaa tena cyo bhas chama nae amezaliwa upya ila mama yake simjuiSalaam Wakuu..
Nashangazwa na hizi kelele za midundiko na kukata viuno tunazopigiwa na wajuaji wa mitaa ya Twiga na Jangwani pale Kariakoo.
Hawa wanashangilia leo kumsajili Chama, yule yule ambaye miaka yote walikuwa wakituaminisha ni mchezaji wa mechi ndogo.
Ina maana huyu Chawa amegeuka ghafla kuwa mchezaji wa mechi kubwa baada ya kuhamia kwao?
Huyu Chama waliyekuwa wakituambia kila siku hana nguvu, leo amezipata hizo nguvu baada ya kuhamia Jangwani?
Nawashauri mtulie, mjitafakari vizuri mkijiuliza mko sawa kichwani?
Tukutane uwanjani na huyo Chama wenu mpya ili tuone kama atakuwa na nguvu za ghafla, na atgeuka kuwa mchezaji wa mechi kubwa ghafla.