Conte: Nyota Tuliowasajili Januari Hamna Kitu
KOCHA Antonio Conte amedai kuwa sera ya usajili ya Tottenham inadhoofisha kikosi, huku akiweka wazi kuwa wachezaji waliowasajili wakati wa dirisha la Januari wamekwenda kukiharibu zaidi kikosi chao badala ya kukiboresha.
Muitaliano huyo amedai kuwa timu yake sasa ina nafasi ya asilimia moja tu kumaliza top 4 katika Premier, Tottenham wanaivaa Man City leo Jumamosi ugenini wakitoka kupoteza mechi tatu mfululizo za Premier.
Katika usajili wa Januari, Spurs waliwaongeza viungo Dejan Kulusevski na Rodrigo Bentancur kutoka Juventus, huku Tanguy Ndombele, Bryan Gil, Dele Alli na Giovani Lo Celso wakiondoka โBadala ya kukiboresha kikosi, tumekidhoofisha,โ alisema.
โBentancur na Kulusevski ni wazuri kwa Tottenham siku zijazo, kwa sababu Tottenham wanatafuta wachezaji makinda, wanaweza kukua na kuendelea, siyo wachezaji walio tayari. Hili ni tatizo. Nimegundua sasa kwamba haya ndiyo maono ya klabu.โ