Viongozi wa Simba ndio wanaiua timu bila wao kujua kwa kufanya usajili wa kizamani mwishowe wanapoteza wachezaji je nini kifanyike?

DeviMitupio

Mgeni
May 27, 2024
9
4
5
Kila nikiamka nakutana na habari mbaya za Simba tu bila kuelewa zinatoka wapi na je Viongozi kazi yao nini? Utaratibu wa kusajili kwasasa umebadilika na kuwa wa kisasa zaidi yaani uwazi na ukweli hakuna tena umafia wala njia za mkato kama ilivyo zamani ila naona viongozi wa Simba wameshikilia zama za kale.

Hawataki kwenda kisasa kufuata sheria na utaratibu maalumu wa kupata mchezaji hivyo basi inapelekea kupata wachezaji wabovu na wale wazuri wakipoteza kila kukicha kwa kushindwa kesi .

Tulianza kwa Lameck Lawi na sasa mbaya zaidi imefika Awesu Awesu ambae mchezaji mzuri sana toka KMC wameshinda kesi na kumrejesha kwenye klabu yao. Bila kusahau wale waliowekwa vizuizini na TFF .

Tuwashauri awa viongozi walioshikilia uzamani na ukale kwenye kuendesha klabu ili kuinusuru klabu hii ya Simba Sports Club na soka la Tanzania kwa ujumla .
 
  • Like
Reactions: amy

Contawaman

Mgeni
Jul 21, 2024
6
2
5
Viongozi wasimba wanazingua yaani wachezaji wanne wazawa wakesi ukianza na lameck lawi,valentino mashaka,awesu awesu na kagoma wanakuwa wanafanya mambo yakitoto😡😡