Wajuvi wa cryptocurrency msaada wenu tafadhali

mhindi

Mgeni
Nov 29, 2021
17
6
5
Tanzania
Mfano nimedepost usd 50 kwenye crypto wallet nikanunua ethereum coins za thaman hiyo nikazi-hold,.. baadae ethereum coin zikashuka sana thaman sokoni zile usd 50 zikapukutika. Je, wallet yangu itasoma negative (- 50) ili soko ilikipanda zipande tena ama wallet itasoma zero kabisa yani hamna kitu account imeungua??
 
  • Like
Reactions: Muwekezaji

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam
Kwa bei ya sasa hivi ETH 1 ni sawa na 3798.09 USD. endapo ukanunua ETH za 50$ kwa exchange rate ya muda huu utapata 0.013 ETH. Sasa cha kwanza wallet yako haitakuja kusoma negative. Ila ikitokea Eth imeshuka thamani ili uweze kujua una dollar ngapi muda huo ni unachukua thamani ya 1 ETH in Dollar unazidisha na idadi ya eth unazomiliki wewe. mfano kwa sasa una eth 0.013 ukizidisha na price ya leo 3798.09 USD unapata 50$ ikitokea ETH ikashuka thamani mfano ikashuka hadi eth 1 ikawa inaworth 1200$ ili ujue investment yako inaworth kiasi gani ni utachukua 0.013 utazidisha mara 1200$ utapata 15.6$ na hiyo ndo itakua ile 50$ yako uliyonunua coin itakua imeshuka hadi hapo kwny 15.6$ also kama ikitokea ethereum 1 ikapanda thamani from 3798.09 usd to 4500$ investment yako ya 50$ kwa sasa itakua ni 58.5$. Cha msingi ni buy low and sell high. ikitokea umenunua price ikashuka keep holding your position maana ukiuza utapata hasara. hold your position subiri ipande uza ikipanda. Ila pia ikitokea thamani ya crypto uliyonunua ikashuka kidogo huwa nao huwa unakua wakati mzuri wa kununua tena ili ufanye kitu kianitwa Dollar Cost Averaging tutaongelea hili siku nyingine.
 
  • Like
Reactions: mhindi