Wanasimba Kauli ya CADENA Mmeichukuliaje?

Makoye Malonja

Mpiga Chabo
May 15, 2024
8
0
0
32
Geita
Kocha Yuko Sawa mabadiliko yanahitajika but sizani kama siku hiyo ingeshindikana kama wangekaa wakajadili kwamba manual asidake siku hiyo Kwa maana hiyo hata yye alihusika Kwa timu kupoteza point Kwa kichapo cha aibu ikiwezekana na yy achafue zake Tu
 

MR. VIP

Mgeni
May 17, 2024
22
3
5
KOCHA wa Makipa wa Simba Dani Cadena ametoa ushauri kwa Viongozi wa klabu hiyo. kwamba ili timu hiyo ibadilike inapaswa kuajiri watu wenye uzoefu, bila kuangalia majina yao, na leseni pekee.

Cadena ambaye hivi karibuni alionekana kuanza utaratibu wa kuwaaga mashabiki kwenye mechi za mwishoni, akiwapatia vifaa vyake, inaelezwa kwamba hana mpango wa kuendelea kusalia Simba endapo hakutafanyika mabadiliko.

Cadena alisema kwamba; “Viongozi waondoe watu wengi sio mimi tu bali kila mtu asiyekuwa na uwezo, Simba inahitaji watu wenye taaluma, uwezo mkubwa na uzoefu, sio tu kwa watu wenye majina makubwa, leseni au katoka eneo gani sio hivyo”

Hata hivyo pia kcha huyo wa Makipa alielezea jinsi ambavyo alikataza golikipa wa klabu hiyo Aishi Manula asicheze mchezo wa dabi, kwa sababu alikuwa hajapona vizuri, lakini kocha Mkuu wa kipindi hicho Robertinho akamtaka acheze hiyo mechi, ambayo Simba iliambulia kipigo cha aibu kutoka kwa watani zao 1-5.

“Siku mbili kabla ya mechi, katika kikao na viongozi wa bodi hakuna hata mmoja aliyeniuliza kuhusu hali ya utimamu wa mwili wa Aishi Manula, lakini Robertinho alisema Aishi Manula yuko fiti atacheza”

“Baadae nilienda kuongea na Manula nikamwambia mechi ya Kesho kama unataka kucheza utacheza, lakini najua haupo fiti, mimi ni kocha najua wachezaji wangu, lakini sikushauri acheze kwa sababu nilijua kitakachotokea, na kweli baada ya mechi tulipoteza kwa 1-5.

Ifahamike kwamba Mkataba wa Dani Cadena Simba unamalizika Juni 30, na hana mipango ya kuongeza mkataba mwingine hadi pale mabadiliko yatakapofanyika ndani ya klabu hiyo.
Uupo sahihi