Arsenal tokea mzunguko wa Pili uanze wamekuwa na mpira mzuri Ila matokeo mabaya

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Arsenal tokea mzunguko wa Pili uanze wamekuwa na mpira mzuri Ila matokeo mabaya hata hii game ya leo unaona kabisa Arsenal anapata goli na kushindwa kuzuia asifungwe

Japo lazima tumpongeze Sana mpinzani wake aliweza kucheza na kukabia chini kabisa akamruhusu Arsenal acheze Ila akamtafuta kwa kushtukiza na Brentford wao ndiyo wamekosa magoli ya wazi wazi kabisa Arsenal aliishika mechi Ila Safi yake ya ushambuliaji haikuwa sawa kabisa waliweza kuzuiwa vema na wapinzani wao

Pia amebakiwa na mechi ngumu mbele ambazo akipoteza na ku draw namna hii atamfanya man City aone ananafasi ya kumpiku nafasi ya juu

D740109B-4ACE-424E-B7E1-8151E2EC13EC.jpeg
 

Lukac

Mgeni
Nov 4, 2022
120
83
5
Arsenal nikama walilizika na kujua watapata bao mdaa wowote maana walikua mdaa mwingi kwenye goal la Brentford ni utulivu tu ambao hawakua nao na hata ukiangalia bao tu la Brentford ilikua vurugu nyingi ila bado arsenal ni timu ambayo ni ngumu sana kuondoka na point zote naamini kwa mpira wa man City ule laini laini arsenal anaweza kuchukua point zote kama sio sare ila City kumfunga arsenal sioni akiweza kufanya hivyo nafikili kesho City apambane kupata point 3 maana game na arsenal kwao itakua ngumu sana
 

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
Jama ndo nimejua Arsenal wana udhaifu kiasi gani upande wa back line kama wanakutana forward nzuri, kongole Brentford hawa jamaa ni wamba kweli kweli🔥

 

JohBwax

Mgeni
Nov 4, 2022
84
72
5
Football Gods are smiling tonight, Mancity anacheza soka leo. Arsenal kuna mahali mliwatukana wazee wa EPL sio bure
 

kamakawa

Mgeni
Nov 4, 2022
60
57
5
Mpira umechezwa muda mwingi golini mwa Bentrfod....sasa huyo jamaa nashangaa sijui hiyo kasi aalikuwa anaitumia wapi maana mipira mingi anapigiwa ya juu jamaa wanaruka nae
 

McRay

Mgeni
Nov 4, 2022
185
131
5
mi naona Brentford walikuw na mkakati mmoja tu leo, kulinda kulinda kulinda baaaaasi,...maana ukiona play style yao vile ilikuw unaona kabsa nin walitaka, ile mistari miwili ya ulinzi na kiungo ilikuwa karibu karibu saaan!! hawakutaka kabsa kutoka kweny eneo lao la nyuma!! Arsenal naweza sema walikosa mtu plan ya kufungua ule ukuta wa wale jamaa,...mtu kama G Jesus unammisi kweny game kama ya leo, Nketiah anakosa ukatili katika nafasi ngumu na chache anazopata!!