Baada Ya Taarifa Ya Hukumu Na Yale Ambayo Yanaendelea Wana YANGA Msimamo Wenu Ukoje?

Credo

Mpiga Chabo
Jul 17, 2024
1
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.
Wazee wote makolo na hatuwatakii kwenye timu yetu wanapenda chokochoko
 

Fred

Mpiga Chabo
Jun 3, 2024
8
0
0
Ila tanzania umaskin na ufukara tunautaka wemyew
Hersi mpaka afrika imeona laz yake waka mpitisha kuwa rais wa vilabu alaf kuna vizee vilivyo goma kufa vinasumbua
Weeee
Kuna mtu ambaye hatak raha kama wanazopata wananchi
Yan leo nimejua hata wahuni nao wanazeekaga
 

sevemoi

Mpiga Chabo
Jul 17, 2024
1
0
0
The issue is clear kuwa sindano inapotakiwa kukutibu inauma, kama kweli wamekiuka katiba hawana budi kuachia ngazi Kisha wafanye kile katiba inataka, uongozi wa yanga ukiacha na ujenzi wa timu imara na yenye ubora kiwanjani ila Kuna mambo yaweza kuwa yamefichwa na matokeo hayo imagine migogoro ya mikataba na maslahi yaliyopelekea kuwa na vifungo mara kadhaa vya shirikisho la soka so Kwa hili pia sishangai. Lisemwalo lipo kama halipo.......
je maswala ya mpira yanapelekwa mahakamani?