Ni zaidi ya mwaka sasa, toka enzi za uzinduzi wa African Football League (AFL) tuliambiwa kuwa viti vyote vya uwanja wa Benjamin Mkapa vingeenda kubadilishwa kama sehemu ya matengenezo makubwa ya uwanja.
Cha ajabu viti vimeendelea kuchakaa na vingine kung'oka huku hakuna kilichofanyika mpaka sasa.
Baada ya tukio la mechi ya Simba vs CS Sfaxien, nimeshangaa kusikia eti Simba inatakiwa kulipa gharama za vile viti chakavu ambavyo nina uhakika vingine tayari vilikuwa vimeshang'oka. Hili jambo siyo sawa.
Inabidi tuhoji pesa yote ya marekebisho ya uwanja imeenda wapi mbona uwanja unaonekana bado uko vile vile zaidi ya running track ambayo sijawahi kuona ikitumika katika mashindano yoyote ya riadha? Running track imebaki kutumiwa na kina Harmonize, Dj Sinyorita na Dj Ally B wakiwa wanatumbuiza.
ZIADA 1: Sijawaelewa walinzi wa Uwanja wa Mkapa. Tukio la juzi na matukio mengine ya nyuma wanaonekana wako very disorganized, hawako fiti kimwili na ni kama wafanyakazi wasio na mafunzo, weledi wa kazi zao wala mfumo wa uongozi. Juzi walishindwa kabisa kucontrol situation ndogo kama ile ya watu wachache sana, wakabaki kukimbia kimbia kama wehu.
ZIADA 2: Uwanja wa Mkapa una security camera? Matukio kama ya juzi yakitokea, ni muhimu kutoa wazi video za tukio husika ili umma ujiridhishe chanzo na wahusika ni kina nani.
ZIADA 3: Wakati wa uzinduzi wa AFL, tuliambiwa Simba ilijitolea kulipia baadhi ya gharama za matengenezo ya uwanja ikiwemo pitch na vyumbani. Inakuwaje mdau wa karibu aliyefanya juhudi za kuheshimisha na kuutangaza uwanja, halafu linapotokea tukio ambalo lilikuwa nje ya uwezo wake achukuliwe kama mhalifu badala kulizungumza ili serikali ionyeshe inakumbuka mchango wake?