Badala ya kuilipisha Simba, tuhoji zoezi la kubadili viti vya Uwanja wa Mkapa limeishia wapi?

Hammy36

Guest
Jan 17, 2023
63
61
25
Dar Es Salaam
Ni zaidi ya mwaka sasa, toka enzi za uzinduzi wa African Football League (AFL) tuliambiwa kuwa viti vyote vya uwanja wa Benjamin Mkapa vingeenda kubadilishwa kama sehemu ya matengenezo makubwa ya uwanja.

Cha ajabu viti vimeendelea kuchakaa na vingine kung'oka huku hakuna kilichofanyika mpaka sasa.

Baada ya tukio la mechi ya Simba vs CS Sfaxien, nimeshangaa kusikia eti Simba inatakiwa kulipa gharama za vile viti chakavu ambavyo nina uhakika vingine tayari vilikuwa vimeshang'oka. Hili jambo siyo sawa.

Inabidi tuhoji pesa yote ya marekebisho ya uwanja imeenda wapi mbona uwanja unaonekana bado uko vile vile zaidi ya running track ambayo sijawahi kuona ikitumika katika mashindano yoyote ya riadha? Running track imebaki kutumiwa na kina Harmonize, Dj Sinyorita na Dj Ally B wakiwa wanatumbuiza.

ZIADA 1: Sijawaelewa walinzi wa Uwanja wa Mkapa. Tukio la juzi na matukio mengine ya nyuma wanaonekana wako very disorganized, hawako fiti kimwili na ni kama wafanyakazi wasio na mafunzo, weledi wa kazi zao wala mfumo wa uongozi. Juzi walishindwa kabisa kucontrol situation ndogo kama ile ya watu wachache sana, wakabaki kukimbia kimbia kama wehu.

ZIADA 2: Uwanja wa Mkapa una security camera? Matukio kama ya juzi yakitokea, ni muhimu kutoa wazi video za tukio husika ili umma ujiridhishe chanzo na wahusika ni kina nani.

ZIADA 3: Wakati wa uzinduzi wa AFL, tuliambiwa Simba ilijitolea kulipia baadhi ya gharama za matengenezo ya uwanja ikiwemo pitch na vyumbani. Inakuwaje mdau wa karibu aliyefanya juhudi za kuheshimisha na kuutangaza uwanja, halafu linapotokea tukio ambalo lilikuwa nje ya uwezo wake achukuliwe kama mhalifu badala kulizungumza ili serikali ionyeshe inakumbuka mchango wake?
 
  • Like
Reactions: Johnroman

D SQUARED

Mgeni
Jun 11, 2024
7
4
5
BADO NAPENDA UGALI

hili swala ni la taifa ukiliongelea vibaya umekwisha ila twende mbele tuludi nyuma Tz wizi ni mwingi qmmq utasikia viti vya benchi la ufundi ndo vilistahili kubadilishwa ila sio real🙄🙄😒😒😒😒😌
 
Enck Jr

Mgeni
Oct 22, 2024
21
1
5
Singida
Simba wanazingua wakati ni watoto wadog sana ndo wanafanyag kazi za kuvunja vit na kuabisha taifaa hawajielew kat ya kocha na mashabik ndo maan wanavunja vit Yanga damu
 
King h himself

Mpiga Chabo
Dec 18, 2024
3
0
0
Ni zaidi ya mwaka sasa, toka enzi za uzinduzi wa African Football League (AFL) tuliambiwa kuwa viti vyote vya uwanja wa Benjamin Mkapa vingeenda kubadilishwa kama sehemu ya matengenezo makubwa ya uwanja.

Cha ajabu viti vimeendelea kuchakaa na vingine kung'oka huku hakuna kilichofanyika mpaka sasa.

Baada ya tukio la mechi ya Simba vs CS Sfaxien, nimeshangaa kusikia eti Simba inatakiwa kulipa gharama za vile viti chakavu ambavyo nina uhakika vingine tayari vilikuwa vimeshang'oka. Hili jambo siyo sawa.

Inabidi tuhoji pesa yote ya marekebisho ya uwanja imeenda wapi mbona uwanja unaonekana bado uko vile vile zaidi ya running track ambayo sijawahi kuona ikitumika katika mashindano yoyote ya riadha? Running track imebaki kutumiwa na kina Harmonize, Dj Sinyorita na Dj Ally B wakiwa wanatumbuiza.

ZIADA 1: Sijawaelewa walinzi wa Uwanja wa Mkapa. Tukio la juzi na matukio mengine ya nyuma wanaonekana wako very disorganized, hawako fiti kimwili na ni kama wafanyakazi wasio na mafunzo, weledi wa kazi zao wala mfumo wa uongozi. Juzi walishindwa kabisa kucontrol situation ndogo kama ile ya watu wachache sana, wakabaki kukimbia kimbia kama wehu.

ZIADA 2: Uwanja wa Mkapa una security camera? Matukio kama ya juzi yakitokea, ni muhimu kutoa wazi video za tukio husika ili umma ujiridhishe chanzo na wahusika ni kina nani.

ZIADA 3: Wakati wa uzinduzi wa AFL, tuliambiwa Simba ilijitolea kulipia baadhi ya gharama za matengenezo ya uwanja ikiwemo pitch na vyumbani. Inakuwaje mdau wa karibu aliyefanya juhudi za kuheshimisha na kuutangaza uwanja, halafu linapotokea tukio ambalo lilikuwa nje ya uwezo wake achukuliwe kama mhalifu badala kulizungumza ili serikali ionyeshe inakumbuka mchango wake?
True kbxa
 
buteng'e

Mpiga Chabo
Dec 19, 2024
4
0
0
Me napenda tu kushauri serekali ni mda Sasa wakuamka na kufanya kitu ambacho nikizuri na kuiesimisha nchii yetyu wakati tunaenda kuoewa mwenyeji wa afcon 2027 ko inabidi wapa bane iri waweze kuboresha uwanja wa Benjamin mkapa
 
Jun 13, 2024
5
1
5
Suala sio Simba kung'oa viti, suala hapo ni wasimamizi wa huo uwanja hawatimizi wajibu wao wanasubilia tukio linatokea wanatoka hadharani timu iliyofonya uharibifu itawajibika, je, matengenezo Yao ya muda wote huwa yanafanyika wapi mpaka mechi za ligi kuu hazichezeshwi kwenye huo uwanja. Kazi zao ni zipi sasa.
 
Tyseem

Mgeni
May 22, 2024
8
3
5
Sasa ndo muda wa simba na yanga kutafuta viwanja vyao wenyewe kuepuka hizi lawama zisizo na nywele wala upala🦁