Game ilikuwa nzuri, lile biriyani la Simba nimeliona kuanzia robo ya mwisho ya kipindi Cha pili, triangular stretching relaxed passes, wachezaji wametulia, japo kulikuwa na ishara za kipato kutaka kuleta ujivuni, ila Simba walikuwa better zaidi ya azam. Though huyu mukwala Kwa mbaaali nkimtazama namuona ana ufreddy kouablan hivi Yani ajitathmini sana.
Kuhusu azam, changamoto ipo forward line Yao, Sina Imani na nassor saadun ambaye baadhi ya wengi walikuwa wakimtazama kama anaweza ingia kambani mara mbili Jana, Bado anahitaji game time ya kutosha na ajifue zaidi, pia Kwa Ile Left back ya azam(pascal msindo) what a perfect performance Kwa dogo
licha ya umri ila ana kitu ndani yake, upande wa kuunda mashambulizi azam walifinywa sana, na hii ilichagizwa na pressing za hapo Kwa hapo za Simba tunaona Kuna nyakati Simba wakipoteza tu fasta pressing inaanzia hukohuko juu,hii ikawanyima uhuru azam FC na kuforce mpira kukimbiziwa fullbacks zilizokuwa na uwezo mkubwa wa kupanda kusapoti na kushuka kuzuia, niliona mzigo mkubwa mabegani mwao, hata Kuna kipindi midfield ikawa inachechema kutokana na Simba kukichafua sana pale, ila big up Kwa majaribio kadhaa ya azam licha ya kutofua dafu.
Game ilikuwa poa sana kiukweli pongezi Kwa wachezaji wote.
Pongezi Kwa makocha, Jana ni ilikuwa mwenye mbinu imara ndo mshindi, ni meeting ya kwanza ya kocha taoussi na fadlu, hivyo wanakitu Cha kujihoji kuelekea game zao, ila all in all "Ubaya u.b.w.e.l.a"