Ukiangalia "efficiency" ya Jean Baleke alipoingia Simba kwa maana ya matumizi sahihi ya nafasi za kufunga magoli, utakubaliana na mimi kuwa jamaa alikuwa suluhisho la matatizo ya ufungaji yaliyokuwa yanaikabili Simba. Jamaa alipokuja alikuwa anafunga magoli magumu sana bila kutumia nguvu. Alionekana ni striker wa asili aliyezaliwa kufunga magoli.
Tulipokuwa tunamlinganisha na Fiston Mayele, wengine tulikiri kuwa Baleke alikosa uwezo wa kukokota mpira au kumkimbiza beki mmoja au wawili na kufunga kama alivyokuwa anafanya Mayele mara kadhaa. Msimu wake wa kwanza ulipoisha, Baleke alionekana kama aliyafanyia kazi mapungufu yake hayo, msimu wa pili alionekana akijaribu kukokota mipira au kupiga chenga mbili tatu ila sina kumbukumbu ya goli lolote alilofunga la namna hiyo.
Tuyaache hayo. Kilichobadilika kikubwa ni uwezo kupungua sana wa Baleke kutumia nafasi alizokuwa anapata tofauti na kipindi alipokuja. Baleke pia hakuonyesha kama jambo hilo lilikuwa linamuumiza. Mshambuliaji wa asili hawezi kukubaliana na nafasi zile alizokuwa anakosa. Baleke alipitia kipindi kirefu cha ukame hadi ikatushtua tukaona bora atupishe. Leo hii anahusishwa na kujiunga na Yanga. Hili linafikirisha sana.
Kina Juma Shaaban na Bangala walihusishwa na kuihujumu Yanga katika derby na walipoachwa kuna watu walitegemea Simba wamchukue walau Bangala kutibu tatizo sugu lililokuwa linaikabili timu ila hawakumchukua hata mmoja wao na mimi nilielewa kwa nini Simba ilisita kufanya hivyo maana ingethibitisha zile fununu za hujuma.
Kaondoka Inonga ambaye ni mmoja wa wachezaji ambao walichangia Simba kutofanya vizuri awamu ya pili ya msimu ulioisha. Inonga alibadilika mbele ya macho yetu na makosa yake yaliyoigharimu sana Simba hakuonekana kuyajutia.
Hao ndiyo wakongoman.