UKWELI WOTE KUHUSU CHAMA NA MO DEWJI KUMGOMEA PESA ANAYOTAKA
Inaelezwa kwamba dili la Kiungo wa Zambia Clatous Chama kujiunga na Yanga linakaribia kukamilika, kutokana na upande wa Simba kushindwa kumtimizia mahitaji yake aliyoyataja kwenye mkataba wake mpya.
Ukweli mchungu kwa baadhi ya mashabiki wa Simba ni kwamba, wakati wowote Mzambia huyo dili la kwenda Yanga linaweza kukamilika baada ya mazungumzo kati yake na mabosi wa Wekundu wa Msimbazi kuingia utata.
Chama alikuwa anataka ongezeko la mshahara, pesa ya usajili, na nyumba nzuri ya kuishi, ili aweze kuongeza mkataba wa miaka miwili tena lakini Uongozi wa Simba unaona Chama, hasitahili kuongezwa mkataba wa miaka miwili.
Lakini pia Rais wa Heshima na muwekezaji wa Simba SC, Mohammed Dewji, MO amemuambia Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Salim Try Again kwamba hawezi kutoa pesa za usajili kwa mchezaji huyo.
Kinachosubiriwa kwa sasa tu, ni upande wa pili kukamilisha taratibu zote za usajili, huku pande wa Chama nao bado unajishauri kusaini mkataba huo na Yanga.
Itakumbukwa kuwa Chama ni mchezaji pendwa wa Simba ila kwa miaka ya hivi kaibuni matukio yake ya utovu wa nidhamu, yamekuwa yakiwachanganya zaidi mashabiki na kufikia hatua wengine kutaka asipewe mkataba mpya.
Simba ni kama wamechoka kumvumilia Chama, na wapo tayarii kumpa mkono wa kwaheri labda Bosi wa timu hiyo abadilishe mawazo kabla ya nyota huyo kusinya mkataba na Yanga.
Upande wa Luis Muquissone bado Uongozi wa klabu hiyo upo njia panda, kumbakiza kwa msimu ujao au wamuache andoke, baadhi ya Viongozi inaelezwa kuwa wanashawishi sana Luis abaki na apewe muda wa kucheza lakini wengine wanasema aachwe apishe wachezaji wengine.
Vipi wanasimba aende?