Manchester United

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
Mechi ya Manchester inayofuata



Taarifa za Club



Wachezaji wa Manchester

Screenshot-2021-12-07-at-11.10.44.jpgScreenshot 2021-12-07 at 11.10.57.png
 
  • Like
Reactions: Njugu

Njugu

Mgeni
Dec 2, 2021
33
7
5
Dar es salaam
Mchezo huu wa Jumamosi kwenye Uwanja wa Carrow Road unazikutanisha Norwich City na Manchester United, timu hizo mbili zenye malengo tofauti kabisa katika msimu wa Ligi Kuu ya 2021/2022.

Lengo kuu la Canaries ni kutaka kisalia katika ligi, wakati Mashetani Wekundu wanatazamia kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Norwich City wamekwama mkiani mwa jedwali wakiwa na pointi kumi pekee mfukoni, na haishangazi kwamba wacheza kamari hao wanawaona kama watu duni kwenye mpambano wa Jumamosi.

Williams, Byram, Zimmermann, na Rashica wote wako nje kutokana na majeraha, huku Normann akiwa na shaka kubwa.

Man Utd, kwa upande mwingine, ilishinda Crystal Palace kwenye mechi ya kwanza ya Ralph Rangnick kama meneja mpya. Mason Greenwood anapaswa kurejeshwa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kufunga bao la ushindi wikendi, huku Raphael Varane na Paul Pogba wakisalia kwenye chumba cha matibabu. Kwa kuwa beki muhimu Luke Shaw amepona jeraha lake, tunajaribiwa kuweka pesa zetu kwa malipo ya Ralph Rangnick.

Ubashiri wangu.
Norwich 1- Manchester united 3
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
“Amenieleza kuwa amekaa Man United kwa miaka saba, anahisi ni wakati mwafaka wa mabadiliko na kwenda mahali pengine
Hii inaeleweka. Nijuavyo mimi hakuna ofa kutoka kwa vilabu vingine, hivyo atabaki.”
-Rangnick kuhusu Martial
1640611479692.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CAVANI ATOKEA BENCHI KUINUSURU KIPIGO MAN UNITED​

1640673234874.png

MSHAMBULIAJI mkongwe wa Uruguay, Edison Cavani ametokea benchi usiku wa Jumatatu na kuifungia bao la kusawazisha Manchester United ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Newcastle United Uwanja wa St James' Park.
Cavani alifunga bao hilo dakika ya 71 baada ya kuingia mwanzoni tu mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa England, Mason Greenwood.
Newcastle ilitangulia kwa bao la mapema tu, dakika ya saba la kiungo Mfaransa, Allan Saint-Maximin.
Mashetani Wekundu walikuwa kando la ligi kwa siku 16 kutokana na kukabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji waliokuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Kwa sare hiyo, Man United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 17 ikiwa nafasi ya saba, wakati Newcastle ya kocha Muingereza, Eddie Howe imetimiza pointi ya 11 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MAN UNITED YAICHAPA BURNLEY 3-0 OLD TRAFFORD.​

1640937323701.png

WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya nane, Ben Mee aliyejifunga dakika ya 27 katika harakati za kuokoa krosi ya Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo aliyekamilishwa shangwe za ushindi dakika ya 35.
Kwa ushindi huo, Manchester United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya sita, wakati Burnley inabaki na pointi zake 11 za mechi 16 sasa katika nafasi ya 18.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Kama ulidhani kila mtu anaona umuhimu wa Cristiano Ronaldo ndani ya Manchester Utd, umekwama
Mambo yapo tofauti kwa Mchambuzi wa Sky Sport Paul Merson ambaye amesema anaamini Edinson Cavani anapaswa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo
"Kwa upande wa timu ya [Manchester United], ninaamini sana Cristiano Ronaldo anafaa kuachwa"
"Najua haiwezi kutokea, lakini Edinson Cavani anapaswa kuchukua nafasi yake mbele akiwa na Jadon Sancho, Marcus Rashford pamoja na Mason Greenwood"
"Kuna kitu hakiko sawa hapo. Nadhani kuna mengi yanayoendelea nyuma ya pazia na haionekani kuwa nzuri kwao"
"Sidhani kama wanaweza kumaliza Ligi wakiwa ndani ya Top Four"
Unakubaliana na kauli za Mchambuzi?
1641191744969.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

WOLVES YAICHAPA MAN UNITED 1-0 OLD TRAFFORD.​

1641283341036.png

WENYEJI, Manchester United wamechapwa 1-0 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu Uwanja wa Old Trafford, bao pekee la Joao Moutinho dakika ya 82.
Nahodha wa leo, Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kichwa Manchester United mwishoni mwa mchezo ambao lingekuwa la kusawazisha, lakini akaambiwa alikuwa ameotea.
Kwa ushindi huo, Wolves inafikisha pointi 28 katika nafasi ya nane, sasa inazidiwa tatu na Manchester United wanaoshika nafasi y saba baada ya wote kucheza mechi 19.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
WENYEJI, Manchester United wamefanikiwa kwenda Raundi ya Nne Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Aston Villa bao la kiungo Scott McTominay dakika ya nane akimalizia pasi ya Mbrazil, Frederico Rodrigues de Paula Santos 'Fred' usiku wa jana Uwanja wa Venue Old Trafford Jijini Manchester.
1641878698563.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BRUNO APIGA MBILI LAKINI MAN U YADROO​

1642397320859.png
WENYEJI, Aston Villa usiku jana wamelazimishwa sare ya 2-2 na Manchester United Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
Mabao ya Man United yalifungwa na Bruno Fernandes yote dakika ya sita na 67, wakati ya Aston Villa yalifungwa na Jacob Ramsey dakika ya 77 na mchezaji mpyam Philippe Coutinho dakika ya 81.
United wanafikisha pointi 32 katika mchezo wa 20 sasa wakiwa nafasi ya saba, wakati Villa inatimiza pointi 23 mechi 20 pia nafasi ya 13.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN UNITED YAWACHAPA BRENTFORD 3-1 MIDDLESEX.​

AVvXsEgMjMOXgTWzOqNIO2WFcr0zMARMHCBARuV8GYjySS2CZ6FaVd7b1pIMHNpcj3VVr-_Q1b7C2in7K3GIWOOtVPJKssZSTSOH4o8KYcILH5amvnc1UAXjRFFBfWrHZepSYuyRertTUm1Ky59-btn-CykaAvc-9rxq8wXtHVyKfTvJTeMHphRwz6BmlGZr=w640-h418

TIMU ya Manchester United imewazima wenyeji, Brentford kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Brentford Community mjini Brentford, Middlesex.
Mabao ya Man United yamefungwa na Anthony Elanga dakika ya 55, Mason Greenwood dakika ya 62 na Marcus Rashford dakika ya 77 akimaliza ukame wa mabao uliomuandama kwa muda mrefu, wakati bao pekee la Brentford limefungwa na Ivan Toney dakika ya 85.
Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya saba ikizidiwa wastani wa mabao tu na Arsenal ambayo pia mechi moja mkononi, wakati Brentford inabaki na pointi zake 23 za mechi 22 katika nafasi ya 14.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Man United Yajitoa kwa Haaland.​


Erling-Haaland.jpg

Manchester United imejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili Erling Haaland baada ya nyota kuripotiwa kupendelea Real Madrid.
Haaland anavutiwa na Meneja mpya wa Man United lakini matarajio ya klabu hiyo ambayo ipo kwenye kipindi cha mpito pamoja na kuwa hatarini kukosa UEFA msimu ujao kunazima ndoto za kujiunga nayo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN UNITED YAICHAPA WEST HAM 1-0.​

AVvXsEhEKvJhlEe5t3v04yluahE0FD7k1SZvASgHCjKLkMt2pnly09i8Ug9UgooyPs7iHPXwxyUcg5vrN0gKN6MDC-2EjViJouZJGc17n29hn0IMh9-tu3BiKDm3xNkVQRQbXHzN9bD94_bwS6W3ipaU3drc1DKQSBeG7lEh7DTf78p3iVUykwQKgw1F433M=w640-h428

TIMU ya Manchester United imewatandika wenyeji, West Ham 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Bao pekee la Manchester United katika mchezo huo likefungwa na mshambuliaji Marcus Rashford dakika ya 90 na
Kwa ushindi huo, kikosi cha kocha Mjerumani, Ralf Rangnick kinafikisha pointi 38 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya nne kikiizidi pointi moja West Ham ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Antony Martial Asepa Zake Sevilla.​


Anthony-Martial-to-Sevilla.jpg

Klabu ya Sevilla ya Hispania imefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Antony Martial.
Nyota huyo amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha United na amekuwa akishinikiza kuondoka ndani ya miamba hiyo.
Sevilla wamekubali kulipa mshahara wote wa mchezaji huyo hadi mwezi juni na atasafiri leo kuelekea Hispania kukamilisha taratibu za kujiunga na miamba hiyo iluiyowahi kuja nchini kupepetana na mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Golikipa wa Manchester United David De Gea ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya EPL
Hii ni mara ya kwanza kwa Golikipa kushinda tuzo hiyo tangu mwaka 2016.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na amesimama


 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BURNLEY YAIONDOA MAN UNITED ‘TOP FOUR’​

AVvXsEiwIAEGFpyeEKf-zcyPEYG16opcHYUht2LJkMEuGeJOWxAlpa82wq9K-1k6c_U2LqLkunz7zgmZguzyJbTD086N1RHbBTAldsWQvaUlTJZlQdq5EQ8vTHucT4Tc2VaPvzWMgFivI0ADFiOszTIo5MgIw5_BqYXNk62VtAVurizyqrmpRfRLQL_OVBAP=w640-h438


TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
Kiungo Mfaransa, Paul Pogba alianza kuifungia Man United dakika ya 18, kabla ya mshambuliaji wa England, Jay Rodriguez kuisawazishia Burnley dakika ya 47.
Kwa matokeo hayo, Man United inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 23 na kuteremka kwa nafasi moja hadi ya tano, wakati Burnley inayofikisha pointi 14 katika mchezo wa 20 inaendelea kushika mkia.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial
🇫🇷
ambaye kwasasa anaitumikia Sevilla kwa mkopo amekiri kuwa alikataa ofa za vilabu vya Juventus pamoja na Fc Barcelona kwasababu alitaka nafasi ya kucheza mara kwa mara kama anavyotaka.


Man Utd news: Anthony Martial grilled by Sevilla boss after disappointing  debut | Football | Sport | Express.co.uk
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI.​

AVvXsEgW9O0Pzl-OTiecz0Y4nneAlQx_p_Adm1hAl5zoX2CU2IHqYOvoXY_hoPeJwuVT47SL4hrYYhGcHh0zl0QzS8vF3de9JHnR07wuJk-oLBoeDkg89lOSrByxAZxQf_K706FmcsteDjvHKZxIa1Wg2htzfMVYUiXSyy_blNSc4B7GOziShekDPbtsj5jW=w640-h428

WENYEJI, Manchester United wameazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwnaja wa Old Tafford, Manchester.
]Jadon Sancho alianza kuifungia Man Unitef dakika ya 21 Uwanja wa Old Trafford, kabla ya Che Adams kuisawazishia Southampton dakika ya 48.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

De Gea: Ninahisi Man U Tumerogwa.​

de-gea.jpg

Kipa David De Gea sasa anadai kuwa klabu yake ya Mancheseter United huenda imerogwa. Man United imekuwa katika mahangaiko tangu kocha matata Sir Alex Ferguson kustaafu mwaka 2013 na mara ya mwisho kushinda taji lolote ni 2017.
Klabu hiyo ilitarajiwa kupigania taji la EPL msimu huu lakini sasa hata kumaliza katika bano la nne bora inaonekana kuwa mtihani mgumu. Mlinda lango David De Gea sasa anadai kuwa huenda Manchester United ililaaniwa, klabu hiyo inapoendelea kupitia mahangaiko msimu huu.
Ndoto ya Man United kuokoa msimu wao huenda isitimie klabu hiyo sasa ikipeleka nguvu zake kujihakikishia nafasi ya nne bora katika Ligi Kuu ya Uingereza, lakini hilo pia kwa sasa linaonekana kuwa mtihani mgumu.
Klabu hiyo ilianza msimu ikiwa na matumaini ya kupigania taji la EPL, lakini imedhihirika wazi kuwa United huenda wakamaliza msimu mwingine bila kushinda taji lolote na De Gea anasema huenda wamerogwa.
“Ninadhani mtu alituroga. Ukweli ni kwamba sielewe kinachoendelea, sielewi kabisa,” De Gea alisema katika mahojiano na gazeti moja la Uhispania la El Pais.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RONALDO, BRUNO WAFUNGA MAN U YASHINDA 2-0.​

AVvXsEi2VPgAEAev9Lml63tSE8W0T7Qx8U99S0JA3jkC7nhE9n3i8Q_4xZQ6guQGL8qD9MBnK1L9-VpfTr4jEvxzzowjoAcf0-fM4_-2N-yxrcW4TaDTM0CFPv8_6DZn5TFc_LJdLBN9m8rjV4FI-VD1OYZbx_kTlvSMSQKIXpRegRQLFSu-73ht9d67gtJg=w640-h446

WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yote yamefungwa na washambuliaji wake Wareno, Cristiano Ronaldo dakika ya 51 na Bruno Fernandes dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Brighton ilimaliza pungufu kufuatia beki wake wa kati, Lewis Dunk kutolwaa kwa nyekundu dakika ya 81 kwa kumchezea rafu Anthony Elanga dakika ya 81.
Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 25 na kupanda nafasi ya nne, wakati Brighton inabaki na pointi zake 33 za mechi 24 sasa katika nafasi ya tisa.