MAPINDUZI CUP 2022.

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Makundi ya michuano ya Mapinduzi Cup 2022 itakayoanza kutimua vumbi tarehe 2/1/2022 huko Visiwani Zanzibar.
KUNDI, A.
1. Azam FC
2. Namungo FC
3. Yosso Boys
4. Meli 4 City
KUNDI, B
1. Young Africans SC.
2. Taifa Jang'ombe.
3. KMKM.
KUNDI, C
1. Simba SC
2. Selem View
3. Mlandege
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

NAMUNGO YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI 2022.​

1641189356670.png
TIMU ya Namungo FC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Meli 4 City katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Namungo leo yamefungwa na Ali Saleh aliyefunga dakika ya 21 na Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 80 kwa penalti, wakati la Meli 4 City limefungwa na Hussein Mwinyi dakika ya 90 na ushei.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Kikosi cha Azam Fc kimeelekea Zanzibar siku ya Jumapili tayari kwa michuano ya Mapinduzi Cup. Azam FC itacheza na Meli 4 City Jumanne.
1641190793623.png
1641190829590.png
1641190918507.png
1641190956614.png
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mechi za leo;
Selem View vs Mlandege FC ( Saa kumi na robo jioni)
Taifa Jang'ombe vs KMKM (Saa mbili na robo usiku)
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

KMKM YASHINDA, MLANDEGE YATOA DROO MAPINDUZI.​

1641281177169.png


TIMU ya KMKM imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Taifa Jang'ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi B usiku wa Jumatatu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya KMKM yamefungwa na Eliasa Suleiman dakika ya 34 na la penalti la Abrahman Othman dakika ya 45 na ushei, wakati la Taifa limefungwa na Yasir Masoud dakika ya 40.
Mechi iliyotangulia ya Kundi C baina ya Selem View na Mlandege ilimalizika kwa sare ya bila mabao.
Michuano hiyo itaendelea Jumanne kwa mechi mbili pia, Namungo na Yosso Boys Saa 10:05 jioni na Azam FC dhidi ya Meli 4 City Saa 2:15 usiku zote za Kundi A hapo hapo Uwanja wa Amaan.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mechi za leo;
Namungo vs Yosso Boys (Saa 10:05 jioni )
Azam FC vs Meli 4 City (Saa 2:15 usiku)
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CHILUNDA AING’ARISHA AZAM FC KOMBE LA MAPINDUZI.​

1641365344827.png

BAO pekee la mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda limeipa mwanzo mzuri Azam FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Meli 5 City katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jumanne Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mechi iliyotangulia jioni, timu nyingine ya Bara, Namungo ilishinda pia 2-0 dhidi ya wenyeji wengine, Yosso Boys, Kundi A pia hapo hapo Uwanja wa Amaan.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita kufuatia kuilaza Meli 4 City katika mchezo wa kwanza Jumapili.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

NAMUNGO FC YAENDELEZA VIPIGO KOMBE LA MAPINDUZI.​

1641366526889.png

TIMU ya Namungo imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuwachapa wenyeji, Yosso Boys 2-0 katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita kufuatia kuilaza Meli 4 City katika mchezo wa kwanza Jumapili.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA YAANZA VYEMA MAPINDUZI, YASHINDA 2-0.​

1641404567150.png
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Selem View katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Simba yamefungwa na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 25 na kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 53.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MABINGWA YANGA SC WATOA ONYO KOMBE LA MAPINDUZI.​

1641457105343.png
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Taifa Jang’ombe usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ebenezer Ma Olongi Makambo dakika ya 33 na kiungo mpya, Dennis Nkane dakika ya 53.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mechi za leo; Mapinduzi Cup
Yosso Boys vs Meli 4 City (Saa 10:15 Jioni)
Azam Fc vs Namungo FC ( Saa 2:15 usiku)
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 KOMBE LA MAPINDUZI.​

1641549004470.png
BAO pekee la kiungo Mkenya, Kenneth Muguna dakika ya 67 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mechi iliyotangulia, ya Kundi A pia, Meli 4 City imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Yosso Boys hapo hapo Uwanja wa Amaan, mabao ya Hussein Mwinyi dakika ya 18, Said Omar dakika ya 45' na Ali Mmanga dakika ya 81.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Mechi za leo Mapinduzi Cup:
Yanga Sc vs. KMKM
Saa 10:15 jioni
Simba Sc vs. Mlandege
Saa 2:15 usiku
Mechi ipi unaisubiri kwa hamu kubwa?
😅

1641551138776.png 1641551186818.png
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI​

MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi licha ya sare ya 2-2 na wenyeji, KMKM jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Yanga ambayo mara zote ilitangulia yalifungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo dakika ya 45 na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah dakika ya 81, wakati ya KMKM yamefungwa na Adam Ibrahim Abdallah dakika ya 54 na Kheri Makame Jecha dakika ya 90 na ushei.
Kwa matokeo hayo, timu zote zinamaliza mechi za Kundi B na pointi nne kila moja baada ya mechi mbili, lakini Yanga wanakwenda Nusu Fainali kwa kuwazidi wastani wa mabao KMKM wameruhusu mabao moja zaidi ya mabingwa hao watetezi.
1641632396901.png
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SIMBA NAYO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI.​

1641632480358.png
MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi licha ya sare ya 0-0 na wenyeji, Mlandege FC jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Simba inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake nne, mbili zaidi ya Mlandege hivyo inatinga Nusu Fainali na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi A Jumatatu.
Mechi iliyotangulia, mabingwa watetezi, Yanga SC wametinga Nusu Fainali pia licha ya sare ya 2-2 na wenyeji wengine, KMKM hapo hapo Uwanja wa Amaan.
Yanga wamekwenda Nusu Fainali kwa kuwazidi KMKM wastani wa mabao tu baada ya timu zote kuvuna pointi nne.
Tayari Kundi A zote Azam na Namungo zimefuzu Nusu Fainali baada ya kila timu kukusanya pointi nne.
Namungo imekamilisha mechi zake, wakati Azam FC wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya Yosso Boys kesho.
Mshindi wa kwanza wa Kundi A atamenyana na mshindi wa kwanza wa Kundi B, ambaye ni Yanga wakati mshindi wa pili wa Kundi B atamenyana na mshindi wa kwanza wa Kundi C, ambaye ni Simba.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

AZAM FC YAIFUATA YANGA KIBABE NUSU FAINALI MAPINDUZI.​

1641718644241.png

TIMU ya Azam FC imekamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wenyeji, Yosso Boys jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo mawili dakika ya 40 kwa penalti na 66, beki Mghana Daniel Amoah dakika ya 51, kiungo mzawa, Ismail Aziz Kada dakika ya 57 na Munzil Abdallah aliyejifunga dakika ya 74, wakati bao pekee la Yosso Boys limefungwa na Daudi Francis Hiluka dakika ya 19.
Kwa ushindi huo, Azam FC inamaliza na pointi tisa kileleni mwa Kundi A, na sasa itamenyana na washindi wa Kundi B na mabingwa watetezi, Yanga katika Nusu Fainali, wakati washindi wa pili wa Kundi A, Namungo FC watacheza na washindi wa Kundi C, Simba SC mechi zote zitachezwa Jumatatu na Fainali itafuatia Alhamisi.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mechi za leo; Mapinduzi cup
Yanga Sports Club vs Azam Football Club (Amani Stadium, Zanzibar saa 10:15 jioni)

Simba Sports Club vs Namungo Football Club (Amani Stadium, Zanzibar saa 2:15 usiku)