KLABU ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Cameroon, Lionel Ateba kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitatu.
Nyota huyo kutoka klabu ya USM Alger ya Algeria anajiunga na Simba kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji huku viongozi wa timu hiyo wakitakiwa kukata jina moja kwenye orodha ya wachezaji wa kigeni.
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, alisema mchezaji huyo amekuja kuongeza makali kwenye kikosi chao kuelekea kwenye Ligi Kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hata hivyo rekodi za hivi karibuni za nyota huyo bado hazijahakisi kile ambacho Simba inakihitaji ndani ya klabu hiyo.
Nyota huyo alijiunga na USM Alger, Januari mwaka huu ambapo amecheza michezo 12 ya Ligi Kuu akitumia dakika 754 na kufunga bao moja huku akisaidia kupatikana mabao mawili.
Inaelezwa ujio wa nyota huyo ni mapendekezo na kocha wa klabu hiyo, Fadlu davids ambaye alitaka viongozi kuongeza mshambuliaji mwingine haraka iwezekanavyo.
Kutua kwa nyota huyo kunamaanisha sasa mshambuliaji Fred Michael na golikipa Ayoub Lakred ambaye yupo nje akiuguza majeraha mmoja wapo atampisha Mcameroon huyo kwenye orodha ya wachezaji wa kimataifa watakaoutumiwa msimu huu.
Fred haonekani kupewa kipaumbele sana na kocha Fadlu, lakini takwimu zake kwenye mechi chache za Ligi Kuu alizocheza msimu uliopita zinampa nafasi ya kubaki mbele ya Lakred.
Msimu uliopita Fred aliingia kwenye timu wakati wa dirisha dogo na kufanikiwa kufunga mabao saba licha ya mara kwa mara kutokea benchi.