Hizi hadaa ambazo uongozi wa Yanga pamoja na GSM wanaendelea kufanya kuhusiana na ujenzi wa uwanja wa Yanga pale Jangwani ni geresha tu ambazo hazitakuja kuzaa matunda yoyote zaidi ya kuwapotezea muda wapenzi, mashabiki na wanachama wa Deportivo de Utopolo.
Pale Jangwani ni sehemu ya mkondo wa maji, hakuna Shirika au Kampuni yoyote ya Bima itaenda kukubali kudhamini mradi wa uwanja wa mpira eneo lile na bila Bima hakuna Benki itaenda kutoa pesa zake kuufadhili. Tukifikia hapo hata uende kuhonga wanasiasa na watendaji wa halmashauri ni kazi bure tu. Ukiona Shirika la Bima la Taifa (NIC) wamekubali kufadhili mradi huu, jua haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kama ambavyo wanapoteza pesa za umma kwa kutoa pesa za wachezaji wa mwezi kwa katimu kasiko na mbele wala nyuma.
Namhusia CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) aanze mapema kutupia jicho kali mradi wa Bonde la Msimbazi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ili kujihakikishia kuwa pesa za serikali zilienda kufanya yale yaliyokusudiwa badala ya kufadhili ndoto za alinacha za Deportivo de Utopolo.
Eneo lote ambalo zamani lilikuwa ni Uwanja wa Kaunda inabidi lichukuliwe na Serikali kwa ajili ya kupitisha maji na jengo lao libomolewe ili zijengwe kingo za kuzuia maji pamoja na bustani kama ambavyo mradi wa Bonde unavyotaka. Kama mko serious kwenye kutatua changamoto za mafuriko hatutakiwi kucheka na kima. Msituchanganye na hadaa zenu za uzinduzi wa jengo la miaka 40 iliyopita na viongozi wa Serikali waache kutumika katika hizi danganya toto.
Povu ruksa.