MASHABIKI WA YANGA WAKIJIFARIJI
"Watu wanasema hivyo kutokana na hoja wengi wanayojaribu kujenga...
Hatukufungwa na Zalan tumefungwa na Timu ambayo kimashindano hakuna timu ya Tanzania inaweza kuifunga kwa Sasa (Al Hilal).
Tumetoa sare tasa ambayo kwetu ni kama ushindi kwani kule tukifunga goli moja tu tunasonga mbele dhidi ya Timu ambayo kimashindano hakuna timu ya Tanzania inayoifunga, tunalia nini?
Kama ni kulia walie Barcelona au Juventus ambao wametumia fedha ya kutosha na bado Club Brudge inasonga 16 bora inawaacha.
Halafu kwa upande wa Mashindano haya ya Shirikisho Yanga ndio Club ya Tanzania iliyofika hatua ya makundi mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote hapa nchini. Lolote linaweza kutokea kule Tunisia na hata tukishindwa msimu huu tumepiga hatua moja mbele"
