TIMU ZOTE ZA LIGI KUU (NBC)

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
SIMBA baada ya juzi kuichapa Mtibwa Sugar mabao 5-0 kocha mkuu, Juma Mgunda ametaja nyota wake wapya wa ushindi kuwa ni Moses Phiri, Augustine Okrah, Pape Sakho, Clatous Chama na Habib Kyombo.

"Wakati nipo klabu nyingine kabla ya hii miaka miwili nyuma nilihitaji kumsajili kwa sababu alinivutia sana kutokana na aina ya uchezaji wake ila bahati mbaya sikufanikiwa kwa hilo." alisema Marchand.
Kocha huyo pia aliongeza mbali na Mayele ila pia anawafahamu Tuisila Kisinda na Jesus Moloko japo Yanga ina wachezaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali kwahiyo ni lazima wajiandae vizuri kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.

1667378479722.png
 
Last edited:

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
KOCHA MKUU WA CLUB AFRICAIN AMUHOFIA MEYEYE
1667378804247.png
Kocha wa Club Africain, Bertrand Marchand anasema moja ya staa wa Yanga anayemuhofia kwenye mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika ni Fiston Mayele.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Marchand amesema Mayele ni mchezaji mzuri ambaye anamfahamu kwa muda mrefu tangu akiitumikia AS Vita ya huko DR Congo.
Nyota huyu wa Yanga, Mayele ndiye anaongoza kwa mabao kwenye Kombe la Afrika baada ya kutupia mabao saba katika hatua zilizopita dhidi ya Zalan kutoka Sudan Kusini na Al Hilal ya Sudan.
 
Last edited:

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
YANGA YAENDELEA KUWA KAMA MSHUMAA NJEE KIDOGO TU WAZIMIKA
1667462649656.png

Yanga yatoa tena na sare dhidi ya Club Africain kwa mkapa, ni baada ya kutolewa katika mashindano ya club bigwa waliokutana na AlHilaly kwa sare ya 1-1 nyumbani na ugenini 1-0 na kupelekea kuangukia mashindano ya kombe la Shirikisho, ambayo mshindano hayo wameanzia nyumbani na kumalizika kwa sare ya 0-0.
Yanga bado wanapata tabu kupata matokeo katika uwanja wao wa nyumbani (Benjamini Mkapa) wanapokutana na timu za njee pamoja na kuwa na wachezaji wakubwa ndani ya kikosi.
Mashabiki wamlalamikia kocha ANAFELI WAPI? NA WACHEZAJI WOTE WENYE UWEZO MKUBWA ANAO.???
 
Last edited:

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
MASHABIKI WA YANGA WAKIJIFARIJI
"Watu wanasema hivyo kutokana na hoja wengi wanayojaribu kujenga...

Hatukufungwa na Zalan tumefungwa na Timu ambayo kimashindano hakuna timu ya Tanzania inaweza kuifunga kwa Sasa (Al Hilal).

Tumetoa sare tasa ambayo kwetu ni kama ushindi kwani kule tukifunga goli moja tu tunasonga mbele dhidi ya Timu ambayo kimashindano hakuna timu ya Tanzania inayoifunga, tunalia nini?

Kama ni kulia walie Barcelona au Juventus ambao wametumia fedha ya kutosha na bado Club Brudge inasonga 16 bora inawaacha.

Halafu kwa upande wa Mashindano haya ya Shirikisho Yanga ndio Club ya Tanzania iliyofika hatua ya makundi mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote hapa nchini. Lolote linaweza kutokea kule Tunisia na hata tukishindwa msimu huu tumepiga hatua moja mbele"
b75ed3bd-b07a-4e70-b319-8efd2a2a3799.jpg