Umeuonaje Mchezo? Azam 0️⃣ Simba Sc 3️⃣

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
278
395
25

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamepoteza pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda katika mchezo wa mzunguko wa pili uliokuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Azam FC 0-3 Simba.

Ni Sadio Kanoute alipachika bao la ufunguzi dakika ya 63 kamba ya pili ni Fabrice Ngoma dakika ya 77 na ile ya tatu ni Duchu dakika ya 89.

Azam FC walikuwa na nafasi yakufunga kipindi cha kwanza walikosa penalti kupitia kwa Feisal Salum aliyegongesha mwamba kipindi cha kwanza.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC.

 
Last edited:
  • Like
Reactions: kingkiller

vyt

Mgeni
May 9, 2024
1
1
5
Ilikuwa poa kizuri Simba kumsaidia yanga kupata ubingwa mapema
Ila Azam nao sio timu inayotegemeka miaka yote wakiendelea hivi watabaki nafsi ya tatu kila msimu
 
  • Like
Reactions: Kijiweni

Star Weldo

Mgeni
May 9, 2024
1
1
5
Kiukweli mgunda apewe team aongoze uwenda sisi wananchi dar Yanga Africa 💚💛 tunawaza kupata changamoto tena kwenye michezo ya Darby
Mgunda awe kocha mkuu wamwamini anakitu
 
  • Like
Reactions: Kijiweni