Kuna mambo makuu mawili.
1. Wachezaji wanajiamini sana chini ya kocha Mgunda, na wana imani naye na hili utaona jinsi wanavyojituma kuhakikisha hawamuangushi kocha aliyewapa imani. Ni wakati sahihi wakuamini wazawa na kumuachia timu Mgunda, aongezewe tuu technical benchi nzuri ikiwemo ya analysis coach wakuzijua vizuri mechi za Simba ndani na nje ya nchi.
2. Inaonekana pamoja na kumuamini Mgunda wachezaji wamepata psychology advise nzuri. Ni vyema sana viongozi ku invest kwenye psychology ya wachezaji na kumtafuta mtu sahihi kwenye hii sehemu, leo utaona kila mchezaji alikuwa mchezoni achilia makosa madogo madogo tuliyoyaona kwa forward wings lakini wengine wote walikuwa mchezoni kwa dakika zote tisini na za mwamuzi. Ni vizuri kuendelea kuweka hii temper kwa timu yetu kuhakikisha wachezaji mentally wanakuwa uwanjani na sii kwa mashabiki au viongozi etc.
Asante!