Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) litafanya droo rasmi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF TotalEnergies 2024/25 na Kombe la Shirikisho la CAF TotalEnergies jijini Doha, Qatar leo Alhamisi tarehe 20 Februari.
Droo hiyo itafanyika katika studio za kisasa za beIN SPORTS na itaonyeshwa moja kwa moja kupitia chaneli rasmi ya YouTube ya CAF, CAF TV. Wachezaji wanne wa zamani wa Afrika watashiriki kama wasaidizi wa droo: Wael Gomaa (Misri), Rabah Madjer (Algeria), Rainford Kalaba (Zambia) na Ben Malango (DR Congo).
Kwa Tanzania inawakilishwa na Simba SC katika kombe la Shirikisho Afrika ambapo anaweza kukutana na Timu kati ya AL MASRY ya MISRI , ASEC MIMOSAS ya Ivory Coast au Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Unatamani Simba apangwe na Nani Leo?