Usajili

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mshambuliaji wa Azam Fc Paul Peter amerejea klabuni hapo akitokea Mbeya Kwanza Fc alipokuwa kwa mkopo wa muda mfupi.
1641878574903.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MHESA AREJEA MTIBWA SUGAR BAADA YA NUSU MSIMU RUVU.​

1642082867800.png
KIUNGO Ismail Aidan Mhesa amerejea klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro baada ya nusu msimu ya kuwa na Ruvu Shooting ya Pwani, huo ukiwa mwendelezo wa mkakati wa kocha Salum Mayanga kuijenga upya timu hiyo iliyopoteza makali yake.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RUVU SHOOTING YASAJILI SABA WAPYA KUIMARISHA KIKOSI LIGI KUU.​

1642082980670.png
KLABU ya Ruvu Shooting ya Pwani imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji saba wapya kuelekea sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Hao ni kipa Benedict Tinocco, beki Iddi Mfaume Mobby kutoka Geita Gold, winga Haroun Chanongo na mshambuliaji Abalkassim Suleiman kutoka Mtibwa Sugar.
Wengine ni kiungo Hussein Suleiman ‘Chuse’ kutoka Mbao FC ya Mwanza, beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Jaffar Mohamed kutoka Namungo FC na mshambuliaji Hamad Rajab Majimengi kutoka Coastal Union ya Tanga.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KIIZA ‘DIEGO’ ALIYEWIKA SIMBA NA YANGA ATUA KAGERA SUGAR​

1642083091503.png
TIMU ya Kagera Sugar imesajili washambuliaji wawili wapya katika dirisha hili dogo kuimarisha kikosi chake kuelekea sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hao ni mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyewika klabu za Yanga na Simba za Dar es Salaam na Freddy Cossmas Lewis aliyewahi kucheza Mwadui FC ya Shinyanga wawili hao wote wakihamia Misenyi, Bukoba Vijijini mkoani Kagera kama wachezaji huru.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

HATIMAYE CHAMA AREJEA RASMI SIMBA SC​

1642167322000.png
KLABU ya Simba imetangaza rasmi kumrejesha kiungo wake Mzambia, Clatous Chotta Chama baada ya nusu msimu tangu aondoke kwenda RS Berkane ya Morocco.
Agosti mwaka jana Simba ilimuuza Chama RS Berkane kwa dau la Sh. Bilioni 1.5, lakini ndani ya nusu mwaka Mzambia huyo ameshindwa kumshawishi kocha Mkongo, Florent Ibengé.
Chama mwenye umri wa miaka 30 sasa, aliibukia Nchanga Rangers FC mwaka 2013 kabla ya kwenda ZESCO United hadi 2017 alipohamia Ittihad ya Misri, alikocheza kwa msimu mmoja kabla ya kurejea Zambia kujiunga na Lusaka Dynamos na mwaka 2018 akajiunga na Simba.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

CHICO USHINDI WA KUBANZA MCHEZAJI MPYA YANGA SC​

1642399128135.png
KLABU ya Yanga imemtambulisha winga Mkongo, Chico Ushindi Wa Kubanza kuwa klabu ya TP Mazembe ya kwao, Kinshasa kuwa mchezaji wake mpya wa sita dirisha hili dogo ambalo limefungwa jana Saa 6:00 usiku.
Ushindi anakuwa mgeni wa kwanza dirisha hili dogo baada ya awali kusajiliwa wageni watano, ambao ni kipa Abdultwalib Mshery, beki beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ kutoka KMKM ya Zanzibar, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, winga Dennis Nkane kutoka Biashara United na mshambuliaji Crispin Ngushi kutoka Mbeya Kwanza.
1642399200561.png
Pamoja na Ushindi mwenye umri wa miaka 26, Yanga pia imemtambulisha Mbrazil, Milton Nienov kuwa kocha wake mpya wa makipa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Singida United Salita Gentil Kambale amejiunga na Kitayosce inayoshiriki Championship
🇹🇿

1642401422246.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MTIBWA SUGAR YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA MGANDA​

AVvXsEg8iS2YnUx43H6WxtaB1W41Xv9fABdJzz-BM-uDYg8MnE8LGgSFkpKO3VHcUYWQ0nwZMLJi7_zGJUHs7PCsuYjOzSk04sq-chf8CH3qjrTknudMcpm9U1helVKnjAmTeGNE9SSawW1ZPR-iO6o3eV_ZhMTdX1g9qbS8NyvWq95yn8GY55gPrWESYxRZ=w640-h640


MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mtibwa Sugar wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili mshambuliaji, Brian Mayanja kutoka Polisi ya kwao, Uganda.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Klabu ya Biashara Utd ya Mara
🇹🇿
imemtangaza Vivier Bahati
🇧🇮
kuwa kocha wao mkuu kwa kipindi cha miezi sita.
Vivier amejiunga Biashara Utd akitokea Azam Fc ambako alikuwa kocha Msaidizi chini ya George Lwandamina kabla hawajafutwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na amesimama
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

OSCAR MAASAI ATUA MTIBWA SUGAR KWA MKOPO​

AVvXsEhQs-WdhWM_lD69JpWsF6O391lTeEezXwOEmoQEllQzT2pF0xUmnhiYJooFkHUGZ64mZnP1316ZWJMC78Jindnp5QxqYqp7eDYjrT9TbPNhnhpr6p5vZCKApMdH_-DSP8q7tJ8Pc5MiEs2CnBnIbdderf-NqcAk5DtRI25nCLWl18AvmveOY_tLS8-_=s16000

BEKI Oscar Masai amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu kutoka Azam FC baada ya awali msimu huu kucheza kwa mkopo pia Geita Gold.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SHAABAN KISIGA ‘MALONE’ ATUA MBEYA CITY.​

AVvXsEgyhq0SxhYEBX79-m2R7o3cTJYPc3azXg3F1ayVADJGZI88R4pPmNOS8hAmeZmPkTlGBqGWerFqZDwSBbLtObFQkw59keSFhFfrKm6T10zh6KJ6cPENh5Q8JXfyuStl62hIEltYTHQeb1xDO5D7C1d8DzSF2Eia7RDcGR-1UExS1zFKFTcJFfcpO-PS=w640-h502

KIUNGO mkongwe, Shaaban Kisiga ‘Malone’ ni miongoni mwa wachezaji wapya saba waliosajiliwa na klabu ya Mbeya City katika dirisha dogo kwa ajili ya sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Wengine ni kipa Deogratius Munishi ‘Duda’, mabeki Juhudi Kibanda, Hamad Waziri na Faisal Mganga, viungo Jamal Issa na mshambuliaji Joseph Ssemuja.
AVvXsEiHIpz0t4zULh0DuowDnEIuxED3ITF5WAy6OGYeADOQSiigQbr9CkOJbcz7dtm4DVbPaCsv7Leecmy-AjALQMO2TQblr3lAr3g2IDFo03NmcqKGq5Eb1R_tYAcQi54yRmITUNx-Jiwn88bKxazTWF5EdftQpwggKuKqksSgw7FhKI8uyk3bBAQhsRfZ=w640-h640
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TP Mazembe Wamfuata Msuva Dar.​

MSUVA-003.jpg

UONGOZI wa Klabu ya TP Mazembe, umefunguka kuhitaji kumsajili winga Mtanzania, Simon Msuva anayekipiga Wydad Casablanca ya Morocco, huku ukiweka wazi mipango yao ya kuhitaji kukirudisha kikosi chao katika mafanikioya kimataifa kunako michuano ya Afrika.
Msuva licha ya timu yake ya Wydad Casablanca kuendelea kucheza katika mashindano mbalimbali, lakini winga huyo yupo Tanzania akiendelea kujifua, huku ikielezwa kwa sasa hayupo kwenye maelewano mazuri na mabosi wake hao kutoka Morocco.
Bosi mmoja kutoka TP Mazembe ambaye hakutaka kutajwa jina lake, ameliambia Spoti Xtra kwamba, wapo kwenye mikakati ya kuhitaji kumsajili Msuva, huku akisema malengo yao ni kuja hapa nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na muhusika ambaye wanaamini kama watamsajili basi atawasaidia hususan katika michuano ya kimataifa.
“Ni kweli Msuva ni moja kati ya wachezaji ambao tumekuwa tukiwahitaji kwa muda mrefu kabla hajajiunga na Wydad Casablanca, lakini shida kubwa kwa kuwa alikuwa anacheza Morocco ilikuwa rahisi kwa yeye kuhamia
alipo sasa, lakini kwa hiki ambacho kinaendelea kati yake na timu tunaamini ni muda wetu wa kufanya naye mazungumzo.
“Tunaangalia uwezekano wa sisi kuja Tanzania kwa ajili ya mazungumzo na mchezaji mwenyewe tuone
itakuwaje.
“Msuva ni mchezaji mzuri na mkubwa, hivi sasa tunahitaji kuirudisha timu katika ubora wa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na tunamuona Msuva akiwa katika hadhi hiyo,” alisema bosi huyo.
Spoti Xtra lilipomtafuta Mratibu wa TP Mazembe, Jean Kazadi, kuzungumzia dili hilo, alisema: “Uongozi upo kazini katika kuhakikisha TP Mazembe inasajili wachezaji wazuri.
“Kuhusu Msuva sikatai kuzungumza kuwa tayari tumezungumza naye au tupo katika mazungumzo naye, lakini unatakiwa kufahamu kuwa TP Mazembe inamuhitaji kutokana na uwezo mkubwa alionao.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BEKI MZANZIBARI, SEBBO AONGEZA MIAKA MIWILI AZAM FC.​

AVvXsEgWFal_8uU_2VzCTgMsSJchP1H-LCxC2kqGCuWAooPSkGKWs2gNlG8CgZNQChZuwH5KnXHGlawUK0RhbII-i3tYGP4epDoj-pI-1qCksoKnDWUEbqmt81b6mhlBN9BKAT7RxSaopKEpULVrKx1dt6MjAt8JpwvuL9K9kTJ9Ib8OOcEgx_y3DzxZ8ey_=w640-h542

BEKI Mzanzibari, Abdallah Kheri 'Sebbo' ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea Azam FC.
Sebbo amesaini mkataba huo leo mbele ya Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na sasa ataendelea kupiga kazi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa na familia yake hadi mwaka 2024.
Aidha, Azam pia imeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser, kuwa Kocha Msaidizi mpya, chini ya Msomali mwenzake, Abdihamid Moallin.
AVvXsEjZrYqEJTLrxz6aJ5i0cl5AyAywffffnTKIXGZdt-aYobg3U2ZzmJYqAM9bLhENVik7g_CJsjw49wVOyRbWw3zodY1nUXsISXNhOrVHdUc5U9PsjueRPLHPEusWLgwHMYXo6qQ7rmmPcQ-1pt8dz1fEmxKniaq5ns7msznW-T7L6HnnG2_b_E-nxOKa=w640-h440

Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U-23), kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia.
Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu.
Omary, mzaliwa wa Somalia aliyekulia England na kuchukua uraia wa huko, pia alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Somalia kuanzia mwaka jana hadi sasa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAWATIA PINGU YOSSO WAKE HADI 2025.​

AVvXsEg4oPUOw_v4Uk3nlefkiW_NR8B6mgdocQBsLWZCxFXrMuXeQBtJKYPmrF3_hyEwjGPzLTgWH_eamZRbGj-KRor0OvkyQZXk7B-P6HoH8Qc2M_Rk8Y2el5a0PwlNV005SN4WlRTFKh1pqyWBYqAXKFuLYFYf0L7o_qQwGkJ47GuUr9aX5lSsFVe-hRAB=w640-h426


KLABU ya Azam FC imewaongezea mikataba wachezaji wake chipukizi wawili, Pascal Msindo na Tepsie Evance wa mwaka mmoja kila mmoja juu ya mikataba yao ya awali.
Taarifa ya Azam FC imesema kwamba mikataba yao ya awali ilikuwa inaisha mwaka 2024, lakini kwa nyongeza waliyoifanya leo, ina maana kwamba wataendelea kupiga kazi Chamazi hadi mwaka 2025.
Wachezaji hawa ni zao la akademi yetu waliyojiunga nayo mwaka 2016.
AVvXsEhWt-roN-Epaa7ZAbjVUhgPP8Vs92LA9nnv0xQQe2axxtUrB1dxM4gqdxRfa8puDesRaPuu2AK3HFjCJvluqOgAMggdXsTIOBIh0LDFDiT4TYYbsX6jA8SYAG6YFBwUxPo2bPOx3girrRTHnXMYeTZFapwyFyGC_lFWTDfVx5iXWlOIz1mkul3_WJzF=w640-h426

AVvXsEhE9-6N_saIUFRECwttZvXWztTM8AdlZEAvYIeH3ZXd_jFXBkjHRelvmaPVvmWLDt5Y5ubJoDcSt5hZfaUlGKdJ8jBHMWQI0EaUzdnWQJKT5E7wp60n88ibsKER5WEvQbWMGOdG7Rk5_oKpalKw8WpDsdVvRZQ7pgP9rkXPVbPeMC8_F3eSQTz162Wo=w640-h426
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Msuva afunguka kuhusu wapi atacheza msimu ujao.​

MSUVA-003.jpg

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa watulivu na muda ukifika ndiyo ataweka wazi kila kitu kuhusu anachopitia kwa sasa kwenye soka.

Msuva alifunguka kuwa akili yake kwa sasa anaielekeza kwenye kufanya mazoezi zaidi ili kuendelea kuwa fiti na ndiyo maana amekuwa mgumu kuzungumza na vyombo vya habari kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Msuva alisema yeye ndiye anajua kila kitu kuhusu wapi atacheza msimu ujao na nini kinaendelea juu ya masuala yake ya kimkataba na klabu ya Wydad Casablanca na wakati wa kuweka wazi ukifika atasema na watu wanapaswa kuwa watulivu.

“Watanzania watulie tu kwa sasa, mimi nitasema muda ukifika nini kinaendelea kwangu, kwa sasa akili yangu naelekeza zaidi kwenye kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa fiti zaidi,” alisema Msuva.

Msuva yupo nchini takribani miezi miwili sasa, ikidaiwa ameondoka Wydad Casablanca kwa sasa, anahitaji kulipwa maslahi yake ya kimkataba ikiwemo fedha za usajili, huku taarifa zikiibuka kuwa TP Mazembe wapo wanawinda saini yake pia.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Inonga arudisha mkwanja Yanga, amkimbia Mayele Airport.​

Inonga PIC

MSIMU huu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba walimsajili kibabe beki wa kati, Henock Inonga Baka ‘Varane’ kutoka DC Motema Pembe ya Ligi Kuu DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa Inonga ulikuwa wa kibabe kutokana na wapinzani wao, Yanga, awali kumalizana kwa kiasi kikubwa na mchezaji huyo, lakini mwisho wa Simba wakapindua meza na kumnyakua beki huyo.
Inonga amefanya mahojiano maalumu na Mwanaspoti akizungumzia picha hilo jinsi lilivyokuwa mpaka kuachana na Yanga kwenda kukipiga katika kikosi cha Simba alichonacho hadi sasa.

KUTUA YANGA
Kabla ya kutua katika kikosi cha Simba mwanzoni mwa msimu huu, Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuhusishwa na kumtaka Inonga ambaye alikuwa anakuja kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi.
Inonga anasema kabla ya kuhitajika na Simba, Yanga walikuwa wa kwanza kumtafuta na kuna mmoja wa viongozi aliongea naye tena na mazungumzo yalifika mbali kwa kukubaliana kila kitu.
Anasema akiwa katika hatua za mwisho kufanya uamuzi Yanga alipokea simu kutoka kwa kiongozi mwingine wa juu wa Simba ambaye naye alimueleza kuhitajika katika timu hiyo huku wakimuwekea maslahi makubwa mezani kuliko yale ya Yanga.
“Nikiwa katika tafakari ya kufanya uamuzi tena muda huo nikiwa nimepima mpaka Uviko 19 na pesa iliyotumwa na Yanga, nilifanya mawasiliano na wachezaji wa DR Congo waliokuwa hapa nchini,” anasema Inonga na kukiri kwamba baada ya kufika nchini alilazimika kurejesha fedha za Yanga walizomtumia kulipia gharama za kupima Uviko. Kuhusu tiketi ambayo Yanga walikuwa wamemtumia anasema kwamba hakulazimika kuilipa kwavile hakuitumia, alisafiria tiketi ya Simba kuja Dar es Salaam. “Katika kufanya mawasiliano wenzangu waliokuwapo hapo na hata waliowahi kucheza waliniambia Simba ni bora kuliko Yanga kwa wakati ule, kwa hiyo nilibadili uamuzi na kuamua kutua Msimbazi.”
Inonga anasema Yanga walifanya kila kitu kwa ajili yake na walikuwa wanamsubiri nchini ili kuja kumalizana nao kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
“Dah! Nadhani ilikuwa imepangwa tu nije kucheza Simba kwani nilifika mpaka uwanja wa ndege wa Kinshasa ili nije Tanzania, lakini hilo lilishindikana na nilibadili uamuzi na kuja siku nyingine kwa ajili ya Simba,” anasema.
“Sikuweza kupokea wala kuwasiliana tena na Yanga baada ya siku niliyotakiwa kuja nchini kwa ajili yao kushindwa kufanya hivyo na nadhani wao walikuja kuona tu natambulishwa Simba.
“Haukuwa uamuzi rahisi kwani nilifika mpaka uwanja wa ndege, ila kutokana na sababu za msingi niliamua tu kubadili ule wa awali na kufanya uamuzi ya pili kuja katika kikosi cha Simba.”

AMKIMBIA MAYELE
Inonga anasema wakati anatakiwa kuja Tanzania kujiunga na Yanga walikuwa na tiketi sawa za ndege na Fiston Mayele na wote walikutana uwanja wa ndege kabla ya kuingia ndani.
Anasema wakati mwenzake akimtangulia ndani kukaguliwa ndipo alipobadili uamuzi baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa msimamizi wake pamoja na Simba kwani walijua angetua na Mayele biashara ingemalizikia Jangwani.
“Kama unakumbuka ile mechi ya Yanga nilicheza kwa ushindani mkubwa dhidi yake na kuhakikisha hawezi kuleta hatari yoyote langoni kwani ni straika mzuri mwenye uwezo wa kufunga,” anasema Inonga.
“Mbali ya hivyo tumejuana tangu Congo kwa maana hiyo lazima kulikuwa na ushindani kati yetu kila mmoja akitaka kuisadia timu yake kushinda, lakini mbali ya masihara yetu pale uwanjani pamoja na ushindani mwisho wa mechi tuliongea na maisha mengine kuendelea.”

MWANASPOTI LAMUIBUA
Inonga anasema alifika nchini kwa usiri mkubwa siku mbili mbele baada ya ile ambayo alikubaliana na Yanga, ambapo alikwenda kuwekwa katika jengo moja katikati ya jiji na hakuna aliyekuwa anafahamu juu ya uwepo wake nchini.

inonga pic

“Tena umenikumbusha yaani ninyi Mwanaspoti mliniandika kwenye gazeti lenu sijui taarifa mlipata wapi kama nimekuja nchini kwa ajili ya Simba na kuachana na Yanga,” anasema beki huyo.
“Unajua kwa nini nimekumbuka hilo. Wakati nasaini Simba niliambiwa kuna mwandishi huku (Tanzania) nimeongea naye huku naonyeshwa gazeti lenu mbele kukiwa na picha yangu. Mkaona haitoshi siku nyingine mkanifuata na hospitali kunipiga picha kabisa.
“Hongereni mlifanya kazi nzuri kwani jambo langu lilikuwa na usiri mkubwa ndani yake.”
Anasema baada ya kutua Simba kuna malengo alijiwekea na kati ya hayo kuna yaliyotimia kama kutamani kuwepo katika kikosi cha kwanza na kucheza mara kwa mara ili kutoa mchango katika timu.
“Baada ya kutua Simba nimejifunza vitu vingi kama mazingira mapya na vitu mbalimbali ambavyo katika maisha yangu ya soka kule Congo sikuwa nakutana navyo kama ilivyo, hapa nchini kumekuwa na mzuka mkubwa wa mashabiki wa soka katika kila uwanja ambao Simba tunakwenda kucheza. Ligi ina ushindani wa kutosha hakuna timu ndogo inayokubali kufungwa kwa urahisi.
“Baada ya kutua Simba kuna vitu kama faida katika maisha yangu nimefanikiwa hata yale ya nje ya uwanja pengine kama nisingekuwa katika klabu hii kubwa labda nisingeyafikia mafanikio hayo.”

WAKONGO YANGA
“Nimeishi na wachezaji wa DR Congo katika timu nyingine ni nadra kuona wachache wanaishi vizuri, ila uwepo wa wengi katika timu moja kwa kiasi kikubwa kuna changamoto inaweza kutokea katikati yenu,” anasema.
“Ukitaka kuamini hili ambalo nalieleza kaa chini na Mukoko Tonombe muulize hili ambalo nasema anaweza kukueleza vizuri ndio maana nami nilifanya uamuzi baadaye ingawa Yanga ni timu kubwa Afrika.”

BEKI BORA DR CONGO
Kwenye tuzo za Ligi Kuu ya DR Congo msimu uliopita Inonga alichaguliwa beki bora wa msimu kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika kikosi cha DC Motema Pembe na mpaka kuitwa timu ya taifa kwa wachezaji wa ligi ya ndani.
Inonga anasema miongoni mwa deni alilokuwa nalo ni hilo Simba wamevutiwa na kiwango chake bora mpaka kutumia nguvu ya kutosha ili kumsainisha mkataba kukipigania kikosi hicho kwenye mashindano yote.
“Kama nilifanikiwa kucheza Congo na kuwa mchezaji bora natakiwa kulifanya hilo hapa kwani nikiweza kucheza katika kiwango cha juu sio mafanikio yangu binafsi, bali nitaisaidia timu kufikia malengo,” anasema.
“Nataka kucheza katika kiwango cha juu katika kila mechi kwani hiyo ndio silaha ya timu yangu kufanya vizuri na ndipo nitaendelea kuaminiwa na kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara hayo mengine yatakuja tu.”

HADI KIPA FRESHI
Inonga anasema katika uwanja anaweza kucheza nafasi zote hadi kipa na hicho ni kipaji alichonacho tangu utotoni akicheza soka ambalo halikuwa la ushindani. “Katika makuzi yangu na maisha ya soka nimecheza kwenye nafasi zote uwanjani na ikitokea siku tumepata shida inayolazimisha mchezaji akae kipa nafasi ya Aishi Manula kama nipo uwanjani naenda kucheza tena vizuri bila shida,” anasema.
“Watu wengi hawafahamu kama naweza kucheza kwenye nafasi nyingi uwanjani kwani ukiangalia katika timu ya DC Motema Pemba na FC Renaissance nimecheza katika nafasi nyingi tofauti mbali ya beki wa kati tu.”

MATAJI MENGI
Inonga anasema kutokana na ukubwa Simba ulivyo alivyoambiwa kabla ya kusajiliwa pamoja na malengo ya timu hiyo, wanastahili kupata mataji mengi kwenye mashindano tofauti.
Anasema Simba ni aina ya timu yenye malengo makubwa na inataka mataji mengi katika kila kombe walilopo wakitamani kulichukua ili kuonyesha ukubwa wao.
“Hatukuanza msimu vizuri kwa kukosa Ngao ya Jamii, lakini tumechukua Mapinduzi na tumepanga kufanya hivyo kubebea Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho (ASFC) na kufanya vizuri zaidi katika Kombe la Shirikisho Afrika,” anasema.
“Hakuna siri kubwa zaidi ya kwetu wachezaji kujituma kama nilivyosema hapo awali ili tuweze kuchukua mataji hayo kwani sio kazi rahisi, tunatakiwa kupambana na kujituma zaidi ya wakati huu.
“Tunaomba mashabiki wetu waendelee kuwa nasi katika kila mashindano ambayo tutakuwepo ili kufanikisha jambo hilo la kuchukua mataji kwani ni ya wachezaji wenzangu ni hiyo.”

KWA NINI VARANE?
Inonga anazungumzia kwa nini amepachikwa jina la utani la beki wa kati wa Manchester United, Raphael Varane na mashabiki wa soka nchini DR Congo. “Hata nashindwa kuelewa unajua ilikuwaje? Msimu uliopita ndio nililipata hilo jina kutokana na kazi ambayo nilifanya uwanjani katika kila mechi mashabiki wakaanza kuniambia nacheza kama Varane,” anasema Inonga.
“Jina likaanza kukua kama utani vile wachezaji wenzangu ndani ya timu katika mazoezi wakaacha kuniita jina langu na kuniita Varane, mara likaanza kuwa kubwa kwa mashabiki nao wakawa wananiita hivyo.
“Nilishangaa kuna baadhi ya mechi mwanzoni kabla ya jina hili la Varane kuchanganya nikiokoa shambulizi, basi mashabiki kule jukwaani hunishangilia kwa kuniita jina hilo jipya.
“Mwisho wa siku hata katika mahojiano mbalimbali ya mashabiki wakaacha kuniita jina langu na kutumia hilo la Varane kutokana na ambavyo nacheza kufananishwa na beki huyo na jina hili lipo mpaka sasa Congo na ni maarufu.”
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

JICHO LA MWEWE: Kichekesho mikataba ya Mwamnyeto na Onyango​

Mwamnyeto PIC

KWAMBA mabeki wawili mahiri wa Simba na Yanga, Joash Onyango na Bakari Mwamnyeto mikataba yao inakaribia ‘kukata roho’ mwishoni mwa msimu huu na haionekani kuwa habari kubwa sana kwa viongozi, mashabiki na vyombo vya habari nchini. Ulaya ingeweza kuwa habari kubwa.
Onyango na Mwamnyeto, ni mabeki mahiri kama walivyo, hauwezi kudhani ndani ya miezi mitatu tu mikataba yao inafika mwisho. Klabu zao hazina wasiwasi. Kuna sababu kubwa inayochekesha ndani yake. Hauwezi kuiona kwa nje. Watani hawajakabiliana pabaya kama ilivyo kawaida yao.
Kila mmoja hana wasiwasi na wizi wa mwenzake. Nadhani Simba wanaamini Yanga hawana haja sana na Onyango. Kisa? Yanga ina mabeki wawili mahiri kwa sasa. Mwamnyeto na Dickson Job aliyeondokea kuwa kipenzi cha Wanayanga kama ilivyo kwa Mwamnyeto.
Zaidi ya hilo, Yanga wana Yannick Bangala ambaye licha ya kuwa kiungo mahiri, lakini ana uwezo mkubwa wa kurudi nyuma zaidi na kucheza kama beki wa kati. Amekuwa akifanya hivyo mara nyingi. Simba hawawezi kuumiza kichwa sana kuvamiwa kwa Onyango.
Inavyoonekana Yanga nao hawana wasiwasi na wizi kutoka kwa wapinzani wao. Kisa? Wanaamini wapinzani wao wametulia kwa mastaa wao wawili wa kati. Onyango na Henock Inonga. Hii ni hadithi ya kila mtu abaki na mchezaji wake. Hakuna kuibiana.
Jaribu kufikiri namna ambavyo Yanga walienda kasi na Mwamnyeto wakati akiwa na Coastal Union. Ni kwa sababu Simba pia walikuwa wanamtaka mlinzi huyo mahiri wa timu ya taifa. Wakati huo wote walikuwa wanasaka walinzi wa kati. Bila ule upinzani hali ingekuwa kama sasa. Mwamnyeto alipata dili zuri.
Pia inaonekana kama vile wachezaji wenyewe huenda wasitake rabsha ya kuhatarisha nafasi zao wakijaribu kuhamia kwingine. Kwa mfano, Mwamnyeto anaweza kuuvunja ukuta wa Inonga na Onyango na kisha akacheza na mmoja kati yao? Nani angependa kujihatarisha kukaa benchi bila ya sababu.
Lakini inawezekana hali ya hewa imetulia kwa sababu nafasi wanazocheza wachezaji huwa hawabadiliki mara kwa mara. Kuanzia kwa kipa hadi walinzi wa kati, kama timu imetulia ni nadra sana kuletewa wapinzani wa kweli.
Kuna nafasi ambazo wakubwa huwa zinawasumbua na maongezi yangekuwa mengi nyakati hizi katika vyombo vya habari. Mfano namna ambavyo Clatous Chama alipokuwa akielekea katika siku za mwisho za mkataba wake Msimbazi. Hali ilikuwa tete. Kisa? Yanga hawakuwa na mchezaji wa aina yake.
Sio kwamba hawakuwa na mchezaji wa aina yake lakini pia hawakuridhika na wachezaji wa nafasi yake katika timu yao. Kelele zilikuwa nyingi na mpaka Simba walipohaha kumbakisha kwa mkataba mpya walikuwa wamechoka kweli kweli. Mithili ya mwanadamu aliyekimbilia kilomita 42.
Kama unabisha katika hili jaribu kufikiria kama mkataba wa Fiston Mayele ungekuwa umebakiza miezi mitatu kama huu wa Mwamnyeto. Jinsi ambavyo washambuliaji wa Simba hawapo katika fomu basi jasho lingewatoka mabosi wa Jangwani. Tungesoma tu vichwa vya habari ‘Mayele amalizana na Simba’.
Ni simulizi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomari Kapombe. Yanga walikuwa hawajatulia katika nafasi zao na tuliona kasheshe nzito kuelekea miezi michache ya mwisho ya mikataba yao. Ni tofauti na hali ilivyo sasa kwa Onyango na Mwamnyeto. Viongozi wamejikuta wakipumua zaidi.
Nadhani ipo pia kwa Shomari Kibwana na Yassin Mustapha. Yanga hawana wasiwasi sana kwa sababu wanajua Simba ina Kapombe na Tshabalala ambao
wana mikataba mipya klabuni hapo. Vinginevyo wangekuwa wanakimbizana mida hii.
Kwa Onyango na Mwamnyeto pia kuna jambo jingine nyuma ya pazia. Achilia mbali wachezaji wenyewe kutotamaniwa na wapinzani lakini kuna ukweli wachezaji wenyewe hawatazami fursa nje ya mipaka ya Tanzania. Wameridhika na walipo.
Onyango katika umri wa miaka 29 inaonekana Tanzania amefika mwisho. Tukumbuke kwanza kwa yeye kuwa Simba ni anacheza timu ya ugenini. Kwao ni Kenya na hauwezi kumlaumu kutosogea kwingine kwa sababu tayari analipwa pesa nyingi kuliko klabu za Kenya ambavyo zingemudu kumlipa.
Mwamnyeto kama ilivyo kwa mastaa wetu, inaonekana wazo hilo halipo. Vinginevyo hizi zilikuwa nyakati za kuondoka katika klabu zetu kiulaini zaidi.
Klabu zetu zinaweza kukugeuza mfungwa kama una mkataba. Unapomaliza mkataba inakuwa fursa nzuri.
Kwa wachezaji wetu kama hakutakuwa na ujanja wa ziada kutoka kwa watani au Azam basi unalazimika kuendelea kuwepo. Hakuna soko jingine nje ya hapo. Ni wachezaji wachache wanaoweza kutazama soko jingine nje ya hapo na kutumia kile kinachoitwa Bosman Rule.
Kwa klabu inakuwa nafuu. Ni nyakati ambazo hawajuti kumpa mchezaji mkataba mfupi. Mkataba wa miaka miwili ni kosa kubwa la kiufundi, lakini hauwezi kuligundua kosa lenyewe kama unajiweka katika nafasi ya kuendelea kumbakisha Mwamnyeto kiulaini.
Labda tungehitaji soko jingine kubwa la ndani kwa wachezaji wetu mahiri. Vinginevyo sio kitu cha faida sana kwa kina Onyango. Jaribu kuangalia nchi nyingine zilizoendelea kisoka ambazo pia zina uchumi mkubwa.
Waingereza wana Chelsea, Man City, Manchester United, Arsenal na Liverpool. Sasa wameongezeka Newcastle United. Wote hawa wanakidhi matakwa ya mastaa wao.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Adebayor Akubali Kusaini Simba​

Adebayor-6.jpg

WAKATI Simba SC ikiambulia pointi moja mbele ya US Gendarmerie juzi Jumapili, ilifanya umafia kwa kuzungumza na wakala wa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Victorien Adebayor ili kumsajili.
Adebayor ni kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Gendarmarie ambaye katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane msimu huu alifunga mabao mawili.
Katika mchezo huo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika uliomalizika kwa sare ya 1-1, Adebayor aliwasumbua sana walinzi wa Simba akitumia vizuri mguu wake wa kushoto.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema: “Tayari tumeanza kufanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji Adebayor.
“Tumesikia anacheza hapa kwa mkopo, huyu ni mchezaji wa kucheza timu kubwa kama Simba na siyo kwenda Ulaya.
“Nitajitahidi kumshauri Rais wa Heshima wa Klabu (Mohammed Dewji) avunje benki ili tuipate saini yake.”
Kwa upande wa Adebayor mwenyewe akizungumza juu ya uwezekano wa kutua Simba, alisema: “Hakuna ambaye anaweza kukataa kucheza kwenye klabu kubwa kama Simba.
“Nipo tayari na kama bahati kwangu, kwa sababu Simba ni moja kati ya klabu kubwa Afrika, ni heshima na bahatikwangu kutakiwa na klabu hiyo.”
Adebayor ambaye ni raia wa Nigeria, anacheza US Gendarmarie kwa mkopo akitokea HB Koge ya Denmark. Aliwahi pia kucheza ENPPI ya Misri.
Nyota huyo kwa sasa thamani yake imepanda hadi kufikia dola za marekani 200,000 ambazo ni zaidi ya milioni 468 za Kitanzania.