Usajili

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Masoud Djuma kocha mpya Dodoma, msaidizi ni huyu​

Djuma pic

Dodoma. NI Rasmi sasa, aliyewahi kuwa Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma Irambona, ndiye Kocha mkuu mpya wa Dodoma Jiji.
Licha ya kwamba, Djuma bado hajawasili mjini Dodoma, ila Mwanaspoti limethibitisha wazi kwamba, akiwasili tu Dodoma atatambulishwa kuwa Kocha mpya baada ya kukubaliana kila kitu akiwa kwao nchini Burundi.
Djuma, anatarajiwa kutangazwa rasmi kesho Alhamisi, Saa sita mchana baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, akianza na kazi ya kuibadilisha timu hiyo kwa msimu uliobaki.
Kocha huyo atasaini mkataba wa miezi sita, ikiwa ni lengo la kuibakisha timu hiyo Ligi Kuu, ndipo mkataba utakapoongezwa baada ya kufikia lengo hilo.
Bosi wa kamati ya usajili wa wachezaji na makocha wa timu hiyo, Fredrick Mwakisambwe amesema kila kitu kinakwenda kama walivyopanga na wakitarajiwa kukamilisha dili hilo kesho Alhamisi kabla ya kocha huyo kuanza rasmi kuinoa timu hiyo, akianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
"Kila kitu kuhusu kinaenda vema kama tulivyopangilia, tunaamini kesho ndipo tutatangaza rasmi na kumtambulisha Kocha huyo, ili aanze kazi kuelekea mchezo wetu wa ugenini dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting" alisema Mwakisambwe.
Katika hatua nyingine, taarifa ya kuachana na Makata kama Kocha mkuu, imeacha wazi hatma ya msaidizi wake Renatus Shija kama ataendelea kuwa msaidizi ama vinginevyo.
Mwanaspoti linaweza kuthibitisha kwamba, Kocha huyo msaidizi pia naye hataendelea kuwa kwenye timu hiyo, nafasi yake ikitarajiwa kuzibwa na aliyekuwa Kocha wa Fountain Gate FC na Fountain Gate Princess kabla ya kujiuzulu wiki iliyopita, Mohammed Muya.
Muya aliwahi kuhudumu kwenye nafasi hiyo ya Kocha msaidizi, akiwa na Jamhuri Kiwhelo 'Julio' wakati timu hiyo ikiwa daraja la kwanza (sasa Championship).
Makocha wote wawili wanatarajiwa kutangazwa kesho Alhamisi mkatika ofisi za Halmashauri ya Jiji.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Sarpong amerudi tena RNFL​

Sarpong PIC

MSHAMBULIAJI wa Zamani wa Yanga, Mghana Michael Sarpong amejiunga rasmi na timu ya AS Kigali inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda (RNFL), akitokea Al Nahda Saudi FC ya Uarabuni.
Sarpong aliyeichezea Yanga msimu wa 2020-2021, kutua kwake AS Kigali kunamfanya kukutana na wachezaji wawili waliocheza wote Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Mghana Lamine Moro wanaokipiga ndani ya Klabu hiyo.
Hata hivyo sio kwa mara ya kwanza kwa Sarpong kucheza RNFL kwani kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa akiichezea Rayon Sports, moja ya timu yenye mashabiki wengi nchini Rwanda.
Baada ya kujiunga na timu hiyo, Sarpong amesema ataipambania timu na kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea.
“Nimekuja hapa kufanya kazi, nitajituma sana kwa kushirikiana na wenzangu ili tufikie malengo ya timu,” alisema Sarpong aliyekabidhiwa jezi namba 23.
Katika RNFL, AS Kigali ipo nafasi ya tano, baada ya kucheza mechi 19 na kuvuna pointi 31 ikiwa imeshinda nane, sare saba na kupoteza nne.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

FIFA YAIFUNGIA BIASHARA KUSAJILI, KATIBU AFUNGIWA MIAKA MITANO​



SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Biashara United kufanya usajili wa wachezaji wapya kuanzia dirisha dogo la Januari 2022 kwa kushindwa kumlipa mishahara mchezaji wake, Timoth Omwenga.
Beki huyo Mkenya alipeleka malalamiko yake FIFA na Biashara ikazuiwa kufanya usajili mpya hadi imalizane naye, lakini uongozi wa Klabu hiyo ukakaidi agizo hilo.
Hiyo imemponza Katibu wa Biashara United, Hajji Mtete kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano.