Triple C bado ni mchezaji mzuri sana na kwa timu inayohitaji makombe ama kuwa na kiu ya mafanikio haiwezi kumtema mchezaji kama Chama.
Maneno ya mashabiki kuwa Simba iachane na Chama akaangalie maisha mahali pengine ni maneno ya watu ambao wamejiunga kwenye tasnia ya soka miaka ya hivi karibuni baada ya kukosa burudani nyingine.
Maana miaka ya nyuma mbali na footbal tuliweza kuupenda sana mchezo wa ngumi, enzi hizo mpambano ulikuwa kati ya marehemu Stanley Mabesi vs marehemu Charles Libondo Mawe.Ilifikia hatua hadi paka akawa anavuka kwenye ulingo jamaa walivyokuwa wanapaniana.
Baadae akaja Rashid Matumla vs mkurya mmoja nimemsahau jina, aisee ilikuwa back to back, achilia mbali ngumi za ridhaa tuliweza kuwaona akina Makoye Isangura, Mzonge Hassan, Michael Yombayomba, Benjamin Mwangata nk.
Sasa vijana hawa wa siku hizi wakipenda kidogo basi mchezaji akizingua wanamtukana, leo Ahmed Ally ametoa taarifa akisema viongozi wanapambana kuongea na Chama lakini lolote watarajie, ina maana hata Thank you itakuwepo.
Ushauri wangu kwa viongozi wa Simba:
Katika maisha ya mpira, vilabu kugombea mchezaji ni jambo la kawaida sana, huyu Triple C ambaye ameiletea mafanikio makubwa Simba kwa sasa moyo na akili yake haitaki tena kutumikia Simba.
Akikumbuka namna anavyolalamikiwa hachezi vizuri vs na Yanga, akikumbuka anavyosimamishwa na wakati mwingine anatukaniwa wazazi wake na kubwa zaidi akiwakumbuka washkaji zake Jonas Mkude na Haji Manara anaona bora awafuate huko.
Mpango wa Chama kwenda kwa hao wanaomshawishi ulianza kipindi kile aliposimamishwa kwa kutofautiana na Benchika.
Kiufupi Chama kakubali kushawishiwa na Haji Manara na Manara amepewa ofa ya kuzunguka bara lote la ulaya kwa kazi nzuri anayowafanyia wanayanga dhidi ya Simba.
Sasa viongozi wa Simba msiogope kuwaambia wana Simba kuwa Chama hana tena mapenzi na sisi, wana Simba wameshakubali matokeo.
Simba iliwahi kukumbwa na misukosuko kama hiyo ya kuondokewa na wachezaji wazuri aina ya Chama.
Nani hamkumbuki Deo Njohole alivyotufanyia? Nani hamkumbuki marehemu Method Mogella 'Fundi' ambaye Chama hamfikii kabisa kiungo huyo wa chini, nani hajui sakata la marehemu Hamis Gaga ama Gagarino, mnakumbuka ishu ya Victor Costa Nyumba? Nani hakumbuki ishu ya Juma Kaseja.
Hata Yanga tumewahi kuwafanyia unyama huo, tuliwahi kuwaumiza kwa kumsajili Omary Hussein Kevin Keegan, tukashangalia kuanzia uwanja wa shamba la bibi hadi mitaa ya keko tukiimba Omary Hussein Kevin Keegan.Nakumbuka kabisa nikiwa na umri wa miaka 9 tu.
Kwa hiyo kama Chama kama amewazidishia mzigo mshukuruni kwa kazi nzuri aliyoifanyia klabu na maisha yaendelee.
Yupo kiungo fundi anafanana kabisa na Chama anaitwa Maroun Tchakei, huyu mwanaume sio wa kawaida, kwanza yuko strong, anajua mpira, ana nguvu, hana uoga wa kutumbukiza mguu kama Chama, Chama kimguu chake anakilindi kama nini.
Waambieni ukweli wana Simba kuwa Chama hatunaye basi, yeye kwenda Yanga ameona kuna fursa mwacheni aende.