Wazir Jr Anafaa Sana Pale Simba Sc Kwa Washambuliaji Wazawa

Mshua

Mgeni
May 27, 2024
34
24
5
WAKATI maboresho ndani ya kikosi cha Simba yakiendelea inatajwa kwamba kuna hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa KMC, Wazir Junior ambaye ni kinara kwa wakali wakutupia eneo la ushambuliaji.

Ikumbukwe kwamba Wazir ndani ya KMC ni mabao 12 alitupia na katika hayo mawili aliwafunga Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex langoni alianza mwamba Ayoub Lakred.

Inatajwa kuwa Simba inahitaji kupata mshambuliaji wa kazi ambaye atakuwa mzawa akishirikiana na wengine ambao watakuja kwenye dirisha la usajili ambalo lilifunguliwa Juni 15 2024. Anatosha Kurejesha Makali Ya Simba Msimu Ujao?
 
  • Wow
Reactions: Maiko

Scott

Mpiga Chabo
Jun 19, 2024
1
0
0
Mmh wazir anajua ila shd wachezaji wetu wa bongo huwa wakifika timu kubwa hawajitumi bali wanaridhika kisa wanapata mshahara wa maana...ila ngj tuone
 
Roby Simba

Mgeni
Jun 11, 2024
21
11
5
Anafaa nahisi atakuwa amejifunza ukienda kwenye timu kubwa inatakiwa uchezej maana alienda yanga akachemsha so Kwa wakati huu akienda Simba Wenda akaonyesha kitu alichonacho
 
kapikulila Alex

Mpiga Chabo
Jun 5, 2024
5
0
0
WAKATI maboresho ndani ya kikosi cha Simba yakiendelea inatajwa kwamba kuna hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa KMC, Wazir Junior ambaye ni kinara kwa wakali wakutupia eneo la ushambuliaji.

Ikumbukwe kwamba Wazir ndani ya KMC ni mabao 12 alitupia na katika hayo mawili aliwafunga Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex langoni alianza mwamba Ayoub Lakred.

Inatajwa kuwa Simba inahitaji kupata mshambuliaji wa kazi ambaye atakuwa mzawa akishirikiana na wengine ambao watakuja kwenye dirisha la usajili ambalo lilifunguliwa Juni 15 2024. Anatosha Kurejesha Makali Ya Simba Msimu Ujao?
Huyo hawezi kuchezea timu kubwa km Simba , Yanga au Azam kwa sababu uwezo alio nao hawezi kuwa mchezaji huru kiwanjani tofauti na anspochezea timu km kmc na zinginezo nafikiri watu wa mpira watajua Nini na maanisha na ndiyo maana hata akina Nkane uliwaona walivyopoteana pale yanga