Hadi sasa timu ya Yanga imeanza mazoezi ya pre-season, katika usajili wa msimu huu naona Yanga imeingia katika mtego ambao uliukuta Simba, wa kujaza wachezaji wa nafasi moja kwa idadi kubwa huku kuna maeneo hayana mbadala. Simba walikuwa wanawajaza mawinga kibao jambo naliona kwa Yanga kujaza viungo washambuliaji kibao, msimu uliopita walikuwa na viungo washambuliaji wa kutosha huku upande wa kiungo mkabaji wenye viwango akiwa ni Aucho jambo ambalo lilileta taharuki baada ya Aucho kuumia mechi ya klabu bingwa dhidi ya Mamelodi simanzi zilitawala juu ya ni nani atalichukua dimba la Aucho kikamiliifu, ndipo akaonekana mwamba Mkude kulitendea haki kwa mechi dhidi ya Mamelodi. Huyu Mkude sielewi hatima yake ipoje ndani ya kikosi cha Yanga msimu huu. Lakini hata kama bado anasalia jangwani bado kuna umuhimu wa kuletwa mtu atakayekuwa mbadala wa Aucho. Aucho anaweza kuumia, kupata adhabu au kuchoka kutokana na kutumika sana hivyo ni muhimu upande wake kuwa na mbadala uliokuwa na kiwango kikubwa pia.
Kwa anayejua, je Yanga mpaka sasa itakuwa na viungo wakabaji wangapi kuelekea msimu huu mpya?
Kwa anayejua, je Yanga mpaka sasa itakuwa na viungo wakabaji wangapi kuelekea msimu huu mpya?