AFCON Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

REFA KOMBA MAZOEZI CAMEROON KUJIANDAA NA AFCON.​

1641457706573.png
REFA wa Tanzania, Frank Komba akiwa kwenye mazoezi viwanja vya Japoma nchini Cameroon kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Komba ni miongoni mwa marefa walioteuliwa na CAF kuchezesha mashindano hayo yatakayoanza Januari 9, 2022.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Mnyarwanda Salima Mukansanga anatarajia kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuchezesha michuano ya AFCON kama mwamuzi wa kati itakayoanza Jumapili hii nchini Cameroon.
Mukansanga amewahi kuwa mwamuzi wa michuano ya Olimpiki, Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake, AWCON na CAFWCL
#TotalEnergiesAFCON2021
1641459428233.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Katika kuhakikisha timu ya Taifa ya Cameroon
πŸ‡¨πŸ‡²
inafanya vyema katika michuano ya AFCON 2021, Rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo Samuel Eto'o alihudhuria mazoezi ya timu hiyo siku ya jana kama sehemu ya hamasa kwa Wachezaji
Zimesalia siku moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
1641633380296.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

WAMBURA WA TFF KATIKA JOPO LA WARATIBU AFCON 2022.​

1641719058699.png
MKURUGENZI wa Sheria, Habari na Masoko wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura (katikati) akiwa na Maofisa wenzake, Inas Mazhar wa Misri (Kulia) na Yousseif Guireh wa Djibouti katika kikao na timu ya Nigeria ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Jijini Garoua nchini Cameroon.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CAMEROON YAICHAPA BURKINA FASO 2-1 UFUNGUZI AFCON.​

1641792519859.png

WENYEJI, Cameroon wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaounde.
Mabao yote ya Cameroon yamefungwa na mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Vincent Aboubakar kwa penalti dakika ya 40 na 45 baada ya Burkina Faso kutangulia kwa bao Gustavo Sangare dakika ya 25.
Mechi nyingine ya Kundi A leo, bao pekee la JΓΊlio Tavares dakika ya 45 na ushei liliwapa Cape Verde ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia hapo hapo Uwanja wa Paul Biya.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
πŸŸ₯
kadi nyekundu ya kwanza AFCON ilitolewa kwa mchezaji wa Ethiopia, Yared Baye. Jana usiku kwenye mechi ya Ethiopia na Carpe Verde.
1641795694312.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SADIO MANE AING’ARISHA SENEGAL AFCON.​

1641877153772.png
TIMU ya taifa ya Senegal imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa y Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe bao pekee la nyota wa Liverpool, Sadio Mane dakika ya mwisho katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Bafoussam mjini Bafoussam, Cameroon.
Mane alifunga kwa penalti dakika ya saba ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 baada ya beki Kelvin Madzongwe kuunawa mpira.