AFCON Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

NIGERIA YASONGA MBELE, MISRI YAZINDUKA AFCON.​

1642397846251.png 1642398519889.png
TIMUya taifa ya Nigeria imefuzu hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.
Mabao ya Super Eagles yamefungwa na Samuel Chukwueze dakika ya tatu, Taiwo Awoniyi dakika ya 45 na Moses Simon dakika ya 46, wakati bao pekee la Sudan limefungwa na Walieldin Khedr kwa penalti dakika ya 70.
Mechi nyingine ya kundi hilo, bao pekee la Mohamed Salah dakika ya 69 liliipa Misri ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea-Bissau hapo hapo Roumdé Adjia na kuweka hai matumaini ya kusonga mbele kuelekea mechi ya mwisho dhidi ya Sudan.
Sasa Nigeria ina pointi sita, ikifuatiwa na Misri pointi tatu, wakati Guinea-Bissau na Sudan kila moja ina pointi moja kuelekea mechi zao za mwisho.
 
Last edited:

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

ALGERIA WAWEKA KOMBE REHANI AFCON, IVORY COAST...​

1642398136358.png 1642398870849.png
MABINGWA watetezi, Algeria wamejiweka njia panda baada ya kuchapwa 1-0 na Equatorial Guinea bao la Esteban Obiang dakika ya 70 katika mchezo wa Kundi E usiku wa Jumapili Uwanja wa Douala nchini Cameroon.
Mechi nyingine ya kundi hilo, Ivory Coast ililazimishwa sare ya 2-2 na Sierra Leone hapo hapo Douala.
Mabao ya Ivory Coast yalifungwa na Sébastien Haller dakika ya 25 na Nicolas Pépé dakika ya 69, wakati ya Sierra Leone yalifungwa na Musa Noah Kamara dakika ya 55 na Alhaji Kamara dakika ya 90.
Sasa Ivory Coast inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Equatorial Guinea pointi tatu, Sierra Leone pointi mbili, wakati Algeria yenye pointi moja inashika mkia.
Mechi nyingine za Jumapili AFCON, Gambia ilitoa sare ya 1-1 na Mali, wakati Tunisia iliitandika Mauritania 4-0 zote za Kundi F Uwanja wa Limbe.
Mali ilitangulia kwa bao la Ibrahima Koné dakika ya kabla ya Musa Barrow kuisawazishia Gambia dakika ya 90, wote wakifunga kwa penalti wakati mabao ya Tunisia yalifungwa na Hamza Mathlouthi dakika ya nne, Wahbi Khazri dakika ya nane na 64 na Seifeddine Jaziri dakika ya 66.
Sasa Gambia una Mali zinafikisha pointi nne, zikifuatiwa na Tunisia pointi tatu na Mauritania ambayo haina pointi na imeshatolewa.
 
Last edited:

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Ratiba ya mechi za leo Jumatatu:
AFCON2021
19:00 Burkina Faso
🇧🇫
vs. Ethiopia
🇪🇹

19:00 Cape Verde
🇨🇻
vs. Cameroon
🇨🇲

1642408869129.png
 
Last edited:

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

CAMEROON YAMALIZA MAKUNDI BILA KUPOTEZA MECHI​


WENYEJI, Cameroon wamekamilisha mechi zao za Kundi A bila kupoteza hata moja baada ya kutoa sare ya 1-1 na Cape Verde usiku wa Jumatatu Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.
Vincent Aboubakar alianza kuwafungia Cameroon dakika ya 39, kabla ya Garry Rodrigues kuisawazishia Cape Verde dakika ya 53.
Mechi nyingine ya Kundi hilo, Burkina Faso pia ilitoa sare ya 1-1 na Ethiopia Uwanja wa Bafoussam .
Cameroon inamaliza na pointi saba, ikifuatiwa na Burkina Faso pointi nne ambayo pia inafuzu Hatua ya mtoano kwa kuizidi wastani wa mabao Cape Verde, wakati Ethiopia imeshika mkia na pointi yake moja.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Salima Rhadia Mukansanga (33)
🇷🇼
hii leo atakuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa AFCON2021 kati ya Zimbabwe
🇿🇼
dhidi ya Guinea
🇬🇳

Ndiye mwamuzi wa kwanza mwanamke kuwahi kuchezesha michuano hii mikubwa barani Afrika
Mechi ni saa 1:00 usiku.
#AFCON21
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na anacheza spoti
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, anacheza spoti, amesimama na nyasi
Inaweza kuwa picha ya Watu 2 na watu wanasimama
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

REFA MTANZANIA KAZINI AFCON GABON NA MOROCCO​

AVvXsEhWDZp0Awsegqv-PId9rw92hZN-HMzopG8XtgBAkH9OMMlu_4WotBjO8ntrZK-IVR8nDEnjC2vqSzB9nlHsBYOp3BHJCeght-RVsxb-3zwFePZgBMJxqfuMD1qLOxqxtTIEoSK9mx_nAh9hqjs0hqm8pHUL3sDPTQrl36sMsoIrQQZPg9qtzUbuPVv5=w640-h544


MWAMUZI Mtanzania, Frank Kombe leo atapeperusha kibendera chake kwenye mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baina ya Gabon na Morocco kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon.
Katika mchezo huo, Gabon watawakosa nyota wao wawili, Pierre-Emerick Aubameyang na Mario Lemina ambao wamerejeshwa kwenye klabu zao baada ya kupatwa na matatizo ya moyo ‘heart lesions’, au vidonda vya moyo wakiwa kwenye AFCON.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Gabon imesema kwamba, Aubameyang, mshambuliaji wa Arsenal ya England na Lemina, kiungo wa Nice ya Ufaransa, watakwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi na klabu zao.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

COMORO YAICHAPA GHANA 3-2 NA KUITUPA NJE AFCON.​



TIMU ya taifa ya Comoro imeitupa Ghana nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa mabao 3-2 katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku wa Jumanne Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.
Mabao ya Comoro yalifungwa na El Fardou Mohamed Ben Nabouhane dakika ya nne na Ahmed Mogni mawili, dakika ya 61 na 85, wakati ya Ghana iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Andre Ayew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25, yalifungwa na Richmond Boakye dakika ya 64 na Alexander Djiku dakika ya 77.
Mechi nyingine ya Kundi C, Gabon imetoa sare ya 2-2 na Morocco Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé.
Mabao ya Gabon yamefungwa na Jim Émilien Ngowet Allevinah dakika ya 21 na Nayef Aguerd aliyejifunga dakika ya 81, wakati ya Morocco yalifungwa na Sofiane Boufal dakika ya 74 kwa penalti na Achraf Hakimi dakika ya 84.
Morocco inamaliza kileleni kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Gabon pointi tano na zote zinasonga mbele, wakati Comoro iliyomaliza na pointi tatu nafasi ya tatu na Ghana pointi moja mkiani zote zinarejea nyumbani.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MISRI YAICHAPA SUDAN 1-0 NA KUSONGA MBELE AFCON​


TIMU ya taifa ya Misri imefanikiwa kufuzu Hatua ya mtoano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la beki wa kati, Mohamed Abdelmoneim dakika ya 38 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D usiku wa Jumatano Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon.
Mechi nyingine ya Kundi D, Nigeria imeendeleza ubabe kwa kuichapa Guinea-Bissau 2-0, mabao ya Umar Sadiq Mesbah dakika ya 56 na William Paul Troost-Ekong dakika ya 75.
Nigeria inamaliza kileleni na pointi zake tisa, ikifuatiwa na Misri pointi sita na zote zinasonga mbele, wakati Sudan na Guinea-Bissau zilizomaliza na pointi moja kila moja zinarejea nyumbani.


Image
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

ALGERIA YAVULIWA UBINGWA AFCON, TUNISIA YAPENYA MLANGO WA DHARULA.​


RASMI, Algeria jana wamevuliwa ubingwa baada ya kuchapwa 3-1 na Ivory Coast katika mchezo wa mwisho wa Kundi E Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku wa Alhamisi Uwanja wa Douala nchini Cameroon.
Mabao ya Tembo wa Ivory Coast yamefungwa na Franck Kessie dakika ya 22, Ibrahim Sangare dakika ya 39 na Nicolas Pepe dakika ya 54, wakati la Algeria waliotwaa taji hilo mwaka 2019 nchini Misri limefungwa na Sofiane Bendebka dakika ya 73, kufuatia Riyad Mahrez kukosa penalti dakika ya 60.
Mechi nyingine ya Kundi E, bao pekee la Pablo Ganet dakika ya 38 limeipa Equatorial Guinea ushindi wa 1-0 dhidi ya Sierra Leone Uwanja wa Limbe.
Ivory Coast inamaliza na pointi saba kileleni, ikifuatiwa na Equatorial Guinea pointi sita na zote Sina kwenda 16 Bora, wakati Sierra Leone iliyomaliza na pointi mbili na Algeria pointi moja safari inaishia hapa.
Na mechi za Kundi F, vigogo wengine barani, Tunisia wametupwa nje baada ya kuchapwa 1-0 na Gambia bao pekee la Abdoulie Jallow dakika ya 90 Uwanja wa Limbe.
Nayo Mali ikaichapa Mauritania 2-0, mabao ya Massadio Haïdara dakika ya pili na Ibrahima Koné kwa penalti dakika y 49 Uwanja wa Douala.
Mali imemaliza na pointi saba, sawa na Gambia na zote zinakwenda 16 Bora, wakati Tunisia inafuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bira kwa kumaliza na pointi tatu na Mauritania iliyomaliza mikono mitupu inaaga mashindano.
Hatua ya 16 Bora itaanza Jumapili kwa Burkina Faso kumenyana na Gabon, Nigeria na Tunisia, Jumatatu ni Guinea na Gambia na Cameroon dhidi ya Comoro.
Januari 25 ni Senegal na Cape Verde na Morocco dhidi ya Malawi, wakati Hatua hiyo ya 16 itakamilishwa Januari 26 kwa mechi mbili kali tupu; Ivory Coast na Misri na Mali dhidi ya Equatorial Guinea.


Image


Image
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Mechi za hatua ya 16 bora: Je nani atatoboa robo fainali?
Burkina Faso
🇧🇫
v Gabon
🇬🇦

Cameroon
🇨🇲
v Comoros
🇰🇲

Egypt
🇪🇬
v Ivory Coast
🇨🇮

Morocco
🇲🇦
v Malawi
🇲🇼

Senegal
🇸🇳
v Cape Verde
🇨🇻

Guinea
🇬🇳
v Gambia
🇬🇲

Mali
🇲🇱
v Equatorial Guinea
🇬🇶

Nigeria
🇳🇬
v Tunisia
🇹🇳

Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Polisi Wakesha Kulinda Nyumba ya Mchezaji Isichomwe.​

kamara.webp

Polisi mijini Free Town nchini Siera-Leone wamekesha kulinda nyumba ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya nchi hiyo Kei Kamara aliekosa penati kwenye mchezo dhidi ya Equatorial Guinea.
Mashabiki hao walitaka kuichoma moto nyumba hiyo kwasababu tu mchezaji huyo alikosa penati na kusababisha timu yao ya Taifa kutolewa kwenye michuano ya AFCON huko nchini Cameroon.
Katika mchezo huo Sierra Leone walihitaji anagalau sare kuweza kufuzu kwa hatua ya 16 bora.