Ligi Kuu Thread

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MECHI NNE ZA LIGI KUU KESHO ZAAHIRISHWA KWA SABABU...​

MECHI nne za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe kesho zimeahirishwa kwa sababu timu nne zipo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
1641793707394.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BODI YAFANYA MAREKEBISHO MENGINE RATIBA LIGI KUU.​

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko machache kwenye ratiba ya Ligi Na ya NBC yakiathiri tarehe za michezo 12, muda wa kuanza kwa michezo sita na kuipangia tarehe michezo mitatu ambayo haikuwa na tarehe kwenye ratiba ya awali pamoja na rmchezo wa kiporo kati ya Kagera Sugar na Simba SC.
Mabadiliko hayo yamelenga kuepuka uwepo wa michezo ya viporo kutokana na ushiriki wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) huku michezo mitatu ikipangiwa tarehe baada ya kufaharnika kwa hatma ya ushiriki wa klabu nne (Yanga, Simba, Azam na Namungo) katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
Ratiba ya awali ya Ligi Kuu ya NBC ilizingatia ushiriki wa klabu nne (Sirnba, Yanga, Azam na Biashara United) kwenye michuano ya CAF kwa kuzipatia nafasi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi, safari na kucheza mechi za michuano hiyo nyumbani na ugenini.
Kuondolewa kwa klabu za Yanga, Azam na Biashara United kwenye michuano ya CAF, kumeilazimu Bodi ya Ligi kupitia upya ratiba ya Ligi na kufanya mabadiliko haya iii Ligi iendelee kuchezwa bila kuwa na mechi za viporo kwa timu yoyote ikiwerno Simba ambayo inaendelea na mashindano hayo.



tff

Jedwali lifuatalo limeainisha mabadiliko hayo kwa kina;

18/12/2021 kuchezwa 26/01/2022, Kagera vs Simba

14/01/2022 kuchezwa 17/01/2022, Polisi Tanzania vs Namungo

16/01/2022, Costal Union vs Yanga

18/01/2022, Mbeya Kwanza vs Azam

17/01/2022, Mbeya City vs Simba

05/02/2022 kuchezwa 03/02/2022, Ruvu Shooting vs Mbeya Kwanza

06/02/2022 kuchezwa 03/02/2022, Simba vs Mbeya Kwanza

23/02/2022 kuchezwa 22/02/2022, Biashara United vs Azam

02/03/2022 kuchezwa 03/03/2022, Simba vs Biashara United

03/03/2022 kuchezwa 27/02/2022, Yanga vs Kagera Sugar

03/03/2022 kuchezwa 01/03/2022, Azam vs Costal

05/03/2022 kuchezwa 07/03/2022, Simba vs Dodoma Jiji

06/03/2022 kuchezwa 04/03/2022, Kagera vs Namungo

06/03/2022 kuchezwa 05/03/2022, Azam vs Polisi Tanzania

15/03/2022 kuchezwa 27/03/2022, Polisi Tanzania vs Simba
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA 1-1 MABATINI​

1642228325387.png

WENYEJI, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Ruvu walitangulia kwa bao la Abalkassim Suleiman Ali dakika ya 78, kabla ya Ibrahim Ame Mohamed kuisawazishia Mtibwa dakika ya 82.
Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 11 baada ya mechi 12, Mtibwa ikiwa nafasi ya 11 kutokana na kuizidi Ruvu wastani wa mabao, ambayo inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
NBC PL baada ya Mapinduzi Cup:
Ruvu Shooting 1-1
Mtibwa Sugar Biashara Utd 3-3 Kagera Sugar
Dodoma Jiji Fc 1-1 Geita Gold Fc
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

BIASHARA YALAZIMISHWA SARE 3-3 NA KAGERA MUSOMA​


WENYEJI, Biashara United wamelazimishwa sare ya 3-3 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
Mabao ya Biashara yamefungwa na Collins Opare kwa penalti dakika ya 49, Baron Oketchi dakika ya 81 na Ambrose Awio dakika ya 83, wakati ya Kagera yamefungwa na Meshack Mwamita dakika ya kwanza, Erick Mwijage dakika ya 33 na David Luhende dakika ya 90 na ushei.
Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 10, Kagera inaendelea kushika mkia mechi 11 na Biashara juu yake nafasi yake ya 15 mechi 12 sasa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

DODOMA JIJI YATOA SARE NA GEITA 1-1 JAMHURI​

WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Geita walitangulia kwa bao la Daniel Lyanga dakika ya 75, kabla ya Waziri Junior kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 17 katika nafasi ya tano na Geita Gold inatimiza pointi 13 katika nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 12.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

YANGA YAIZIMA COASTAL MKWAKWANI,YAIPIGA 2-0​

1642401865919.png
VIGOGO, Yanga SC wamerejea na moto wao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji, Fiston Kalala Mayele dakika ya 41 kwa kichwa akimalizia krosi ya Mkongo mwenzake waliyetoka naye AS Vita ya kwao, Kinshasa msimu huu, beki Djuma Shabani na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 90 akimalizia pasi ya winga mzawa, Farid Mussa Malik.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mtunisia Mohamed Nasreddine Nabi inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 12 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
Coastal Union inayofundishwa na kocha Mmarekani, Melis Medo inabaki na pointi zake 17 za mechi 12 pia katika nafasi ya nne.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Mbeya City Fc hawajashinda wala kutoa sare katika mechi tano za mwisho dhidi ya Mnyma Simba Sc.
Leo wanakutana tena katika dimba la Sokoine Mbeya, mkeka wako unampa nani?
1642414785842.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

FULL TIME​

Mbeya City 1-0 Simba Sc​

20' Paul Nonga​

Alama tatu​

Clean Sheet​

Wakiwa pungufu​

Mbeya City wanamng'oa meno Mnyama Simba Sc aliyevamia kwenye jiji la kijani​



Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAICHAPA MBEYA KWANZA 1-0 SOKOINE​

Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, anacheza spoti na nyasi

BAO pekee la mshambuliaji Mzambia, Rodger Kola dakika ya 45 na ushei, limetosha kuipa Azam FC dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa ushindi huo, Azam FC iliyo chini ya kocha Mmarekani mzaliwa Somalia, inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tano, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 11 za mechi 12 katika nafasi ya 11.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Ruvu Shooting Inautaka Ubingwa Ligi Kuu.​

Ruvu-Shooting-2.jpg

UONGOZI wa Ruvu Shooting, umebainisha kuwa lengo lao kuu ni kufanikisha timu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22.
Timu hiyo ambayo kabla ya mechi za jana Jumatatu ilikuwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Januari 20, mwaka huu itacheza dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa jambo la kwanza wanalohitaji msimu huu ni kuchukua ubingwa.
โ€œUongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanafahamu umuhimu wa kufanikisha malengo ya klabu
japo tulipitia changamoto ya kuondoka kwa wawekezaji na wachezaji tisa, lakini hiyo haitokuwa sababu ya kuifanya
timu isifike hatua tunayohitaji kwa sababu nafasi hiyo ina fursa kubwa na nyingi zaidi kuliko nafasi zingine zote kwenye msimamo,โ€ alisema Bwire.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Wababe wa Simba Mzigoni tena Leo.​

MBEYA-CITY-1.jpg

LIGI Kuu Tanzania Bara bado inaendelea na leo Januari 20 kutakuwa na mchezo mmoja kwa timu kusaka pointi tatu muhimu.
Mbeya City ambayo imetoka kutibua rekodi za Simba kwa kuwatungua kwenye mchezo uliopita Januari 17 kwa bao 1-0 leo itamenyana na Ruvu Shooting.
Mbeya City iliweza kusepa na pointi tatu mazima kwa ushindi huo na bao pekee lilifungwa na Paul Nonga ilikuwa dakika ya 19.
Inakutana na Ruvu Shooting wazee wa mpapaso wakiwa wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao wa ligi uliopita, Uwanja wa Mabatini.
Kwenye msimamo wa ligi Mbeya City imejijimbia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 14 na pointi 11.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Polisi, Yanga Kukipiga Jijini Arusha Jumapili.​

YANGA-5-1.jpg

UONGOZI wa timu ya soka ya Polisi Tanzania FC umethibitisha kupeleka mchezo wao dhidi ya Yanga SC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha baada ya uwanja wao wa Ushirika uliopo mjini Moshi kuwa na matumizi mengine.
Mchezo huo ulipangwa kupigwa Jumapili katika uwanja wa Ushirika lakini siku moja kabla ya mchezo yani Jumamosi kutakuwa na tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hivyo imeilazimu uongozi wa timu hiyo kuhamishia mechi hiyo Arusha.
Inaweza kuwa ni habari njema kwa Yanga kwani wenyewe wameweka kambi jijini hapa kujiandaa na mchezo huo na tayari juzi wametumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mechi moja ya kirafiki dhidi ya Mbuni FC inayoshiriki ligi daraja kwanza (First league), ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Makamu mwenyekiti wa Polisi Tanzania FC, Robert Munisi amesema awali walipanga kutumia uwanja wao wa nyumbani wa Ushirika katika mchezo huo lakini baada ya kuona itatumika kwenye matamasha la Utamaduni wameona wahamie Arusha ambapo itatoa urahisi kwa wapenzi wao kujitokeza kwa wingi na kuisapoti timu.
267275041_238268688446130_2493836917464305964_n.jpg

Alisema athari za kuhamishia mchezo huo jijini Arusha kutoka Moshi ni kubwa sana kwa sababu Ushirika ni uwanja ambao wameizoea pia maandalizi tayari walishafanya ya kucheza hapo ikiwemo kuboresha sehemu ya kuchezea (pitch), na sasa wanaenda katika uwanja mwingine ambao nao watakuwa kama wageni.
โ€œKatika kanuni mnaulizwa kama ikitokea dharura uwanja wenu wa pili ni upi na sisi uwanja wetu wa pili ni Sheikh Amri Abeid tunakwenda kupambana kushinda hili kubakisha alama tatu nyumbani โ€œ
โ€œTumefanya jitihada zote za kuhakikisha mchezo huo unasogezwa mbele lakini mpaka asubuhi ya leo jitihada hizo zimeshindikana sasa tunasubiri taarifa rasmi kutoka bodi ya ligi lakini asilimia za kwenda kucheza Arusha ni kubwaโ€ amesema Munisi.
Ameongeza kuwa wanatambua Yanga tayari jijini Arusha wamekuwa kama wenyeji hasa baada ya kuweka kambi na kupata nafasi ya kutumia uwanja ambao utapigwa mchezo huo lakini na wao wala hawana wasiwasi kwani timu hiyo haina historia ya kushinda dhidi ya kushinda ugenini.
ri Abeid ilikuwa ni Machi 7 mwaka 2021 ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1. Bao la Yanga likifungwa na Fiston Abdul Razak dakika 42 huku la Polisi likifungwa na Pius Buswita dakika ya 89.
Katika msimamo wa Ligi Kuu NBC Yanga ndio vinara kwa alama 32 baada ya michezo 12, imeshinda 10, sare mbili, ikiwa imefunga mabao 22 na kufungwa goli nne pekee, utofauti ya alama 14 na Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo kwa alama 18.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MBEYA CITY YAIPIGA RUVU, SASA YAIPUMULIA SIMBA.​

AVvXsEhLkE1mBkBFp6KpFIxDiSHueCohrKhDc8mZ3OHCgn3yIl7blXWHv2RwGrskeA-GQ37TwePevht-okx4ugljsFFztQmM6H1TKSxxHYuiM8fxj8YotwXmJR6rfWz648Y1zhlqGr1TpuYbdQdKu5HbW7e09azCWSDww6Eyid8YeXYQLIYJ2FLohBsEQyUy=w640-h428

TIMU ya Mbeya City imeendeleza wimbi la ushindi nyumbani katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Bao pekee la โ€˜Wana Koma Kumwanyaโ€™ leo limefungwa na Aziz Andambwile dakika ya 54 na kwa ushindi huo MCC wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya tatu, wakizidiwa pointi mbili tu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
Ruvu Shooing kwa upande wao baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 pia katika nafasi ya 14.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mtibwa Yawaita Simba Manungu Tuliani.​

SIMBA-3-1.jpg

THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa Simba wasiwe na mashaka kwa kuwa wanachokitaka wao ni mchezo huo uchezwe Uwanja wa Manungu.
Kesho, Januari 22 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar v Simba katika Uwanja wa Manungu.
Habari zinaeleza kuwa Simba wamewaeleza bodi kuwa wao wana mashabiki wengi jambo litakalokuwa tofauti kwao kutokana na uwanja huo kuwa na uwezo wa kubeba mashabi wachache.
Uwezo wa Uwanja wa Manungu ni kuingiza mashabiki 2,500 jambo ambalo limekuwa likileta mvutano kwa upande wa Simba.
Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco kimewasili Morogoro kwa maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kifaru amesema:โ€Tunataka kuona mchezo unachezwa kwenye uwanja wetu wa Manungu hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka tupo tayari na uwanja wetu ni mzuri, Simba wasiwe na wasiwasi,โ€.



 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MECHI YA POLISI NA YANGA YAHAMISHIWA ARUSHA.​

MECHI ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Polisi Tanzania na Yanga SC iliyopangwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi kesho imehamishiwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

AVvXsEi-P1YZcV8kS9nU1ZNGbyU-WdoryRIBUWHCmBJjr6hzLxof7l3eZoyYd_oxCnVwR0pVxVx4Pq5FPwUvfGfLyT6Naxb3gJokekIq4wm-dQP_o74wvN8wjLCMWmQEU_ZcslUoPJK08YZ6C5AwI5xFnqX10VNPQu0_1OWY4Sn8iQVLN8qZeebmJKXQyPCs=s1080