Ligi Kuu Thread

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

KAGERA SUGAR YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI.​

AVvXsEitjlCZY-c7puJjSApYU1ieuKrV6PGDryFuh9Sg_EYQEGyMMtutwnuz21CkDyUeBNCNCKxpLTHokoVBsul954WtcL_EP44Vjy4T5SiAkpD0g07D9jN6_a9Qfh3aW9UqRKceW1UMAPredNv76Jh9RtWQ0yfN8jVMu1FF--M1870SL-ltpdHknGDZ06OP=w640-h640


WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamechapwa mabao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Kagera Sugar inayopata ushindi wa kwanza baada ya mechi sita yote yamefungwa na mshambuliaji Hassan Mwaterema dakika ya 31 na 76, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Issa Abushehe dakika ya 67.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 12 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 10, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 13 nafasi ya saba.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MBEYA KWANZA CHUPU CHUPU KWA KMC, SARE 1-1 SOKOINE.​

AVvXsEiav8hyd8hpxb3wxsgytnBC8UtFNtA-BSrHtEbYx_eyxbt3a57Os06Sya4Bv9md9Tb7sWtoazcz-bTP30yLJivsKCcA5NEByq7oqhDwXyQ6ZvigdG71Zwd6ZrfSZBLLjjpPco3CvAtFOzW6PsVfF6mURIb8wtkjitOB6sPKWTFmBDYaC_vvqXd7eSg1=w640-h444

WENYEJI, Mbeya Kwanza wamelazimishwa sare ya 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Matheo Anthony alianza kuifungia KMC dakika ya pili tu, kabla ya mshambuliaji mwenzake, Habib Kyombo kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 90 na ushei.
Kwa sare hiyo, Mbeya Kwanza wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa 13 ingawa wanabaki nafasi ya 11 na KMC wanatimiza pointi 15 katika mchezo wa 13 pia na kusogea nafasi ya nane.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Yanga Wampigia Simu Muuaji wa Simba SC.​

NONGA.jpg

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Paul Nonga, amefichua kuwa kitendo cha kufanikiwa kuwafunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kimesababisha apokee simu nyingi za pongezi, zikiwemo za baadhi ya watu wa Yanga.
Nonga, ambaye pia aliwahi kuchezea Yanga, bao lake la Jumatatu iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, lilitosha kumchinja Mnyama na kuipa Mbeya City ushindi wa bao 1-0. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Simba wanafungwa kwenye ligi msimu huu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nonga alisema baada ya mchezo huo, alipokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali wa timu hiyo wakiwemo watu wa Yanga ambao wamekuwa ni mahasimu wakubwa wa Simba katika Ligi Kuu Bara.
“Kitu kikubwa ambacho kilitokea baada ya matokeo ya ushindi dhidi ya Simba, ni kwamba nilipokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali wa Mbeya City, kwa sababu tulijiandaa kupata matokeo ingawa sikupokea simu za wadau wa Mbeya City peke yake, kwani hata watu wa Yanga wapo wengi ambao walinipigia simu za pongezi kutokana na ushindi ambao tuliupata.
“Unajua Yanga na Simba ni mahasimu halafu inakuwa ni kawaida ikitokea Simba au Yanga ikifungwa na hizi timu nyingine, mashabiki kuchekana na kwangu ilikuwa hivyo kwa kuwa kwao wao ni jambo la kawaida halafu ndiyo maisha ya soka jinsi yanavyokwenda wakati wote ila jambo kubwa kwa sasa tunaangalia mechi nyingine ambazo zipo mbele yetu,”
alisema Nonga.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Beki wa Kazi Prisons Kuikosa Azam FC.​

kiemnya.jpg

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Tanzania Prisons, Salum Kimenya hatakuwa sehemu ya kikosi kitachomenyana na Azam FC leo Uwanja wa Nelson Mandela kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Kimenya ataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kimenya alisema: “Sipo sawa kwa sasa kwa kuwa ninasumbuliwa na nyama za paja, lakini ambacho ninashukuru Mungu ni kwamba ninaendelea vizuri na nimeanza mazoezi mepesi.”
Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 na kukusanya pointi 11 ikiwa nafasi ya 13, Kimenya ameanza kikosi cha kwanza kwenye mechi saba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Abdi Banda Aomba Radhi.​

Abdi-Banda.jpg

Beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda amewaomba radhi wadau wa soka nchini Tanzania kufuatia kauli aliyoitoa dhidi ya wachezaji wa Simba SC.
Banda alitoa kauli ya kuwakejeli kwa wachezaji wa Simba SC, baada ya mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Manungu Complex Jumamosi (Januari 22) na timu hizo kwenda sare ya 0-0.
Beki huyo ambaye amewahi kucheza soka Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini msimu huu 2021/22, ameomba radhi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
“Tuanze wiki mpya yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Huenda niliwaudhi au kuwakera wengi kila mmoja kwa nafasi yake naomba mnisamehe sana.
“Kwenye mpira au kwenye mchezo wowote kuna maneno ya kejeli na dharau kwa mpinzani wako au hata mchezaji mwenzako lakini hamaanishi kuna uhasama kama wengi walivyopokea maneno yangu. Michezo ni furaha na ajira basi tusichukulie kila kitu personal/serious sana.
“Naomba mnisamehe sana maana kila mtu ana upokeaji wake na tafsiri yake. Sikuwa na lengo la kumbagua Henock Inonga au wachezaji wengine wa Simba SC. Tusahau yaliyopita, tupo kwa ajili ya kujenga na kuutangaza mpira wetu na sio chuki wala ubaguzi wowote hasa kwa wachezaji wanaokuja kucheza hapa kwetu,” amesema Banda.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Kukiwasha na Kagera Sugar Kaitaba Leo.​

SIMBA-2-4.jpg

UONGOZI wa Simba umesema kuwa wana furaha kubwa kwenda kucheza Bukoba kwenye uwanja wa kisasa
na wenye hadhi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Timu hizo leo Jumatano zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara majira saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba mkoani Kagera.
Uwanja wa Kaitaba wenye nyasi bandia, ni kama ule wa Simba wanaoutumia katika mazoezi yao uitwao Simba Mo Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
SIMBA-11.jpg

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa kiwanja hicho kitawapa fursa wachezaji kuonesha kiwango bora ambacho Wanasimba wanakitaka.
Ally alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia mia moja baada ya jana asubuhi kusafiri kwa ndege kuelekea Bukoba tayari kwa mchezo huo.
SIMBA-1-4.jpg

“Kikubwa tunachofura– hia ni kwamba tunawenda Bukoba kucheza katika kiwanja chenye hadhi yetu, kiwanja ambacho kinawapa fursa wachezaji wetu kuonesha ubora wao.
“Hakuna asiyefahamu uwezo wa wachezaji wetu walioipa ubingwa wa ligi kwa miaka minne mfululizo siyo kitu kidogo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Yanyooshwa na Kagera Kaitaba, Kiiza Atupia.​

kagerasugarfcofficial_272660469_348790176842291_3175460259108721405_n.jpg

Uwanja wa Kaitaba dakika 90 zimekamilika mbinu ya Pablo Franco imekwama mbele ya Kagera Sugar.
Ni Hamis Kiiza dakika ya 70 aliwatungua Simba baada ya safu ya ulinzi kufanya makosa katika kuokoa shambulizi la kushtukiza.
Hakuna sababu nyingine kwa Franco ambaye alikuwa kwenye uwanja mzuri wa kapeti wa Kaitaba kakwama kushinda ugenini.
Simba inabaki na pointi zake 25 ikiwa imecheza mechi 13 na vinara ni Yanga wenye pointi 35.
Kiiza alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano Ikumbukwe kwamba Kiiza amewahi kucheza ndani ya Simba na kwa sasa ni ingizo jipya ndani ya Kagera Sugar.
Huu ni mchezo wa pili kwa Simba kupoteza baada ya ule wa kwanza kuwa mbele ya Mbeya City na bao walilofungwa ni moja.
Hakuna kiporo kwa sasa na ni tofauti ya pointi 10 kati ya Simba na Yanga ambao ni vinara wa ligi.