KAMATI YAIPA USHINDI WA MEZANI NAMUNGO DHIDI YA MBEYA KWANZA
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipa ushindi Namungo FC baada ya wapinzani, Mbeya Kwanza kugomea mechi ya Ligi Kuu Ijumaa Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Pamoja na hilo, Kamati imechukua hatua mbalimbali juu ya masuala tofauti ya ukiukwaji kanuni katika mechi za hivi karibuni.