Ligi Kuu Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

RUVU YAITANDIKA COASTAL 3-1 MKWAKWANI​

WENYEJI, Coastal Union wamechapwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Ruvu Shooting leo yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 19, Haroun Chanongo dakika ya 31 na Samson Joseph dakika ya 79, wakati la Coastal limefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 22.
Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 11, ikizidiwa pointi moja na Coastal baada ya wote kucheza mechi 18.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KAGERA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE​


BAO pekee la Hassan Mwaterema dakika ya 20 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya sita,ikizidiwa pointi moja na Mbeya City inayoendelea kushika nafasi ya tano baada ya timu zote kucheza mechi 18.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

DODOMA JIJI YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0 JAMHURI​


WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Joram Mgeveke dakika ya 26 na Anuary Jabir dakika ya 48 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya 11, wakati Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao 14 katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 18.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MTIBWA SUGAR YAICHAPA GEITA GOLD 2-0 MANUNGU​


WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Nzigamasabo Steve dakika ya 27 na Mululi Mayanja dakika ya 76 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 12, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 21 katika nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 18.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Prisons wajikoki kiafande kuikabili Biashara​

prisons-3.jpg

KIKOSI cha Tanzania Prisons, kimejiweka sawa kuelekea mchezo wao dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho Jumanne kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, Biashara itakuwa nyumbani kuwakaribisha maafande hao wa Magereza wanaoburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo.

Prisons na Biashara zote zipo katika hatari ya kushuka daraja, hivyo kila timu itahitaji pointi tatu muhimu ili kujiweka eneo salama.

Prisons ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo ikiwa na pointi 13 huku Biashara ikiwa nafasi ya 13 kwa alama 16. Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Prisons, Jackson Luka Mwafulango, amesema kikosi chao kipo tayari kuweza kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

“Tunacheza na Biashara, maandalizi yapo vizuri na kikosi chote kilichosafiri kipo salama na tumejipanga kuchukua alama tatu muhimu kwenye mchezo huo ili tuweze kuwa kwenye nafasi nzuri Ligi Kuu Bara,” alisema Mwafulango.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TFF YAANZA KUTOA LESENI ZA KLABU MWAKA MPYA​



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) jana limeanza rasmi kutoa fomu za maombi ya leseni za klabu kwa mwaka 2022-2023 na tarehe ya mwisho ya kuchukua ni Aprili 23, mwaka huu.


 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BIASHARA YAICHAPA PRISONS 2-1 MUSOMA​


WENYEJI, Biashara United wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Mabao ya Biashara United yote yamefungwa na Deogratius Mafie dakika ya 26 na 34, wakati la Prisons limefungwa na Ezekiah Mwashindilindi dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Biashara inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 13, wakati Prisons inaendelea kushika mkia na pointi zake 13, baada ya wote kucheza mechi 18.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MCHAKATO UJENZI UWANJA WA KISASA DODOMA WAIVA​


WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema kuwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo na kutengwa kwa asilimia tano ya fedha za Bahati Nasibu kumesaidia maendeleo ya michezo nchini.
Kauli hiyo imetolewa Machi 16, 2022 Mji wa Serikali-Mtumba Jijini Dodoma Waziri Mchengerwa alipokuwa akieleza mafanikio ya wizara yake kwa kipindi cha mwaka mmoja madarakani mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
“Hadi Februari mwaka huu kiasi cha TZS Bilioni 1.55 kimepokelewa kutoka Hazina. Fedha hizi zimeanza kusaidia maendeleo mbalimbali ya michezo nchini na zitasaidia pia katika programu za uendelezaji wa miundombinu.”



Sambamba na hilo Mheshimiwa Mchengerwa alibainisha kuwa katika mwaka mmoja huu, serikali imekamilisha hatua muhimu za ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo kukamilika usanifu wa uwanja wa soka wa Dodoma, kukamilika usanifu wa ujenzi wa viwanja vya mazoezi na kupumzikia wananchi vitakavyojengwa Dar es Salaam, Dodoma na Geita.
Akiyataja mafanikio mengine ya wizara hii alisema kuwa jumla ya TZS Bilioni 19 zitatumika kukarabati shule 58 za michezo na kuwekewa miundombinu mbalimbali ya kisasa.
Waziri Mchengerwa alisema kuwa nchi ya Tanzania, Novemba mwaka 2021 ilipata bahati ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (CANAF-2021) ambapo pamoja na kupokea takribani nchi 13 kutoka Afrika, Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Walemavu, Tembo Warriors, ilikuwa miongoni mwa Timu nne zilizofuzu kutoka Afrika kwenda Kombe la Dunia Uturuki Oktoba mwaka huu.

 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

PUMZIKA KWA AMANI JOHN POMBE MAGUFULI​

6584C47E-8D24-467B-800B-9608F9134EF2.jpeg

MACHI 8 mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK John Pombe Joseph Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika pambano la watani wa jadi, Yanga ikifuta uteja uliodumu kwa miaka minne mbele ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Shujaa wa Yanga SC ni leo kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 44 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 25.
Morrison, mchezaji wa zamani wa Heart of Lions, Ashanti Gold za kwao Ghana, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Delhi Dynamos FC ya India na Orlando Pirates ya Afrika Kusini alifunga bao hilo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kungo Jonas Gerlad Mkude.
Baada ya msimu huo, Morrison akahamia kwa watani wa jadi, Yanga.
Machi 26, mwaka 2021 Magufuli akafariki dunia na leo Watanzania wanaazimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mpendwa wao huyo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KLABU ZAADHIBIWA KWA MAKOSA TOFAUTI KATIKA LIGI​

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa adhabu kwa klabu mbalimbali za Ligi Kuu kwa makosa tofauti.


 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Gofu European Tour Aprili 7​

WhatsApp-Image-2022-03-22-at-4.02.41-PM.jpeg

SERIKALI kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Gofu Tanzania (TGU), kimethibitisha kuwa wenyeji wa mashindano ya Gofu Europe Tour yatakayofanyika Aprili 7 hadi 10 mwaka huu katika viwanja vya Kilimanjaro Jijini Arusha.
Mashindano hayo yana lengo la kuunga mkono wa juhudi ya serikali chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan kuendeleza utalii nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TGU, Chris Martin alisema ni mara ya kwanza Tanzania kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yatashirikisha mataifa mbalimbali.
Alisema wachezaji 156 wamethibitisha kushiriki mashindano hayo ambapo Tanzania imetoa wachezaji 12, Kenya, Uganda, Rwanda na Malawi kumetoa wachezaji wawili.
“Hapa nchini tutakuwa na wawakilishi 12 kutoka katika klabu tofauti, watakuwepo wachezaji wengine kutoka bara la Ulaya, Asia na mataifa mengine nina imani mashindano haya yatatoa fursa kwa kutangaza utalii wa Tanzani,” alisema Martin.
Alisema TGU imeomba Tanzania kuandaa mashindano haya ambayo mwaka jana yalifanyika nchini Kenya yanatarajia tena kufanyika mwakani kwa mara ya pili kuwa wenyeji.
“Tunaendeleza kampeni ya Royal Tour ambayo Rais wetu Mama Samia ameianzisha kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na vitu vinavyopatikana hapa nchini,” alisema Martin.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo alisema ni jambo nzuri kuona mashindano hayo yanatangaza utalii wa taifa, lakini serikali itakutana na Chama cha TGU kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mashindano hayo.
“Kwa sasa hatuwezi kuzungumza lolote kwa sababu serikali tuna mpango wa kukutana na uongozi wa Chama cha gofu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano baada ya hapo tutatoa tamko kuhusu uwenyeji wa mashindano hayo,” alisema Singo.
Katibu wa maandalizi ya mashindano hayo, Enock Magile alisema sifa za wachezaji ambao watashiri lazima wawe na kiwango kizuri katika rekodi ya mchezo huo.
Alisema watacheza ambao watakuwa na viwango hivyo watapita bila tatizo lolote lile kwa ajili ya kuitangaza taifa na kuonyesha uwezo wao.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Serikali yasema VAR haikwepeki Tanzania​

msigwa-3.jpg

Serikali imetilia mkazo kuwa kwa namna matumizi ya teknolojia yanavyozidi kupiga hatua hakuna kipingamizi kwamba Tanzania inahitajika kuileta teknolojia ya usaidizi wa video itakayowawezesha Waamuzi kuona matukio tata ambayo kwasasa yamekuwa yakiwaweka matatani.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ni wazi kuwa wameyasikia malalamiko mengi yanayohusisha maamuzi yenye mkanganyiko kwenye mechi za Ligi Kuu jambo ambalo hayawafurahishiwao wakiwa ni wadau namba moja ya mchezo huo.

”Kwa hali ilivyo sasa na Teknolojia ilipofika hatuna namna tunaweza kuiepuka VAR, inawezekana tusiwenayo leo kwasababu uwekezaji wake ni gharama kubwa sana, lakini ni kitu ambacho tunakihitaji, tunajua Waziri wa fedha ni mwanamichezo na angependa hizi dosari tunazoweza kuziondoa kwa kutumia VAR zisiwepo”

“Hata mimi ni mwanamichezo nisingependa ziendelee kuwepo ,kwahivyo ni dhamira ya Serikali baadaye tunakokwenda huko kadri ya uwezo wetu ili tuwe na VAR, ili kuondoa haya malalamiko ya magoli ya mkono, goli sio goli, penati sio penati, kashika hajashika,” amesema Gerson Msigwa Msemaji Mkuu wa Serikali.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAMBO YAZIDI KUNOGA KITUO CHA TFF KIGAMBONI​

E9C2ECED-C8DB-499A-A903-D9324D14B76E.jpeg


ZOEZI la utandikaji nyasi bandia kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam linaendelea vizuri kama inavyoonekana pichani.


 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KONGAMANO LA MICHEZO MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA​

41E6A549-9273-4EEA-B318-64A4B95412AC.jpeg

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeandaa kongamano la Michezo kuazimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan madarakani.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIGI KUU YAREJEA LEO, UHONDO WOTE AZAM TV​

442020D0-DE41-4189-BF20-B5DA16E60FEE.jpeg

BAADA ya mapumziko ya wiki moja na ushei kupisha kalenda y mechi za kimataifa, Ligi Kuu ya Tanzania Bara inarejea leo kwa mchezo mmoja, Polisi Tanzania wakiwakaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambayo itaonyeshwa LIVE na Azam Sports 1 HD kuanzia Saa 10:00 jioni.
85AE9C70-5F13-4DD4-A68D-57249AF4FAF1.jpeg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO ZAISHA KWA SARE​

F12EFABB-34DC-4E49-BA00-0C56776AD70B.jpeg

MECHI zote za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo zimemalizika kwa sare, 1-1 Mtibwa Sugar na Kagera Sugar mkoani Morogoro na 0-0 na KMC na Namungo FC Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo uliotangulia mchana, George Chota alianza kuwafungia wenyeji, Mtibwa Sugar dakika ya 37 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, kabla ya Erick Mwijage kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 69.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 13, wakati Kagera Sugar inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 19.
KMC baada ya sare ya leo inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya nane, wakati Namungo FC inatimiza pointi 26, ingawa inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 19 pia.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

PRISONS YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-2 SOKOINE​


WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jumanne Elfadhili dakika ya 18 na Benjamin Asukile dakika ya 78 na 90 na ushei, wakati ya Dodoma Jiji yamefungwa na Anuary Jabir dakika ya sita na Salmin Hoza dakika ya 32.
Kwa ushindi huo, Prisons wanafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 21, nafasi ya 12 baada ya timu zote kucheza mechi 19.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

WAZIRI MKUU MGENI RASMI KIKAO CHA MAAFISA MICHEZO​


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kesho Aprili 5, 2022 anatarajia kuwa Mgeni Rasmi kwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo Aprili 4, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara. Dkt, Hassan Abbasi wakati akiwa Mwenyekiti wa kikao kazi hicho.
Dkt Abbasi amesema kada za maafisa Utamaduni na Michezo ni kada za kimkakati kwa maendeleo ya nchi yetu.
Aidha, amesema kikao kazi hicho kimekuja katika wakati mwafaka ambapo lugha adhimu ya kiswahili imepata msukumo mkubwa duniani na sanaa imekuwa kazi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ajira kwa vijana.
Kwa upande wa Michezo amesema ni wakati ambapo michezo imepiga hatua kubwa.
Ameyataja baadhi ya mambo kuwa ni pamoja na kushiriki kwenye mashindano makubwa ya jumuiya ya madola na mashindano ya dunia ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu.
Ametumia muda huo kuipongeza timu ya simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika.
Kikao hicho kinahudhuriwa pia na wataalam wa kutoka TAMISEMI na kesho wakati wa ufunguzi rasmi kitarushwa mbashara na TBC.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

WIZARA YA MICHEZO YAANZISHA TAMASHA​



WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanzisha Tamasha la kimkakati la Mtaa kwa Mtaa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana na kuviendeleza na kutoa ajira kwa vijana nchini.
Wizara imekuja na mkakati huo kuhakikisha nchi nzima kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa kunakuwa na uwakilishi kutoka mikoa yote nchini na hatimaye Taifa Cup ambayo itahusisha mikoa yote nchini ili kuimarisha uzalendo na uchumi miongoni mwa jamii.
Akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo Aprili 4, 2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo ni ya kimkakati na ni muhimu kwa taifa ambapo amewahimiza washiriki hao kuchapa kazi kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya 2020-205, Dira ya Maendeleo ya Taifa na Miongozo ya Viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
"Twendeni tukachape kazi, tukatangaze utamaduni wetu ili kuuendeleza kwa vijana wetu, kuongeza mapato na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla" amesema Dkt. Abbasi.
Akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo, Mkutugenzi wa Maendeleo ya Michezo mchini Bw. Yusuph Singo amesema dhana ya mtaa kwa mtaa katika sekta ya michezo imegawanyika katika maeneo matatu.
Mitaa hiyo ni mtaa iliyoainishwa kwa mujibu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), mtaa wa pili unahusisha michezo katika taasisi ikiwemo UMITASHUMTA, UMISSETA, SHIMIWI, UMISEVUTA, SHIMUTA na mtaa wa tatu unajumuisha mashirikisho ya michezo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

POLISI NA SIMBA SASA APRILI 15 MOSHI​




MECHI ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya wenyeji, Polisi Tanzania dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC itachezwa Aprili 10, mwaka huu kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Machi 15, lakini ukaahirishwa kutokana na Simba kukabiliwa na michuano ya Afrika.